Tuesday, February 24, 2015

KUTOKA KWANGU: Aina ya taa za chumbani

OK, hiyo picha nzuri hapo juu ni mfano wa taa za bedroom. Ndani ya bedroom unahitaji mchanganyiko wa taa kwa ajili ya kufanikisha kila unalofanya ukiwa chumbani. Kwa ajili kama tujuavyo sio kuwa ukiwa bedroom umefumba macho tu, kuna wakati unasoma kitabu au gazeti, kuna wakati unaangali muvi na kadhalika.
Taa za kwenye ceiling ni kwa ajili ya kuangaza chumba kizima – zinafaa sana wakati unasafisha ama umepoteza soksi..ha ha haaaa, imo hiyo.

Kama unasoma kitandani, taa nzuri ni  za kivuli za mwanga wa kurekebishika pembeni mwa kitanda. Hakikisha unatumia balbu zisizokuwa na joto sana. Taa hizi zinakusaidia kusoma ukiwa umelala bila kumbughudhi mwezi wako kwa mwanga wa taa.

Huenda unawahi kuamka mapema zaidi ya mwenzi wako kuwahi kazini, kama una kabati la nguo chumbani je utavaaje kwenye giza pasipo kumsumbua mwenzako? Suluhisho ni kuweka taa kwenye kabati la nguo, unawasha unaona nguo zako unachagua unayotaka kuvaa. Taa za namna hii zipo zile ukifungua kabati zinawaka, ukifunga zinazimika automatically huna haja ya kufanya mwenyewe.

Na kama unavaa gauni la mtoko na vitupio vyake ili kujiamini utaonekanaje suluhisho ni kutumia taa za pembeni mwa kioo.


Upo hapo? Kwahivyo mwisho wa siku kutokana na lifestyle yako unajikuta bedroom kuna taa nyingi tofauti kwa matumizi mbalimbali. Kumbuka unaishi mara moja tu, raha jipe mwenyewe.

No comments:

Post a Comment