Wednesday, February 18, 2015

Mzee Yusuph kuoa tena mke wa tatu, wake zake watupiana vijembe mtandaoni

Mwimbaji mahiri wa muziki wa taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke wa tatu hivi karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito wakitupiana vijembe mtandaoni.

Akipiga stori na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa anatarajia kuoa mke huyo ambaye anaishi huko visiwani Pemba na kwamba mipango ikiwa tayari kila kitu kitakuwa hadharani. Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni malkia Leyla Rashid ambaye pia ni mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa kuandikiana status za vijembe.
Mzee Yusuph akiwa na mke wake wa pili, Chiku

Habari zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee Yusuph hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha chuki kwa mwenzake akiwa nao.

"Waache tu warushiane vijembe tena ndio vizuri na dawa yao nawaletea mke wa tatu na wala sina mpango wa kuwapatanisha" alisema Mzee Yusuph.

CHANZO: CLOUDS FM

Napenda uimbaji wa Leyla Rashid, ni kama anamumunya peremende mdomoni..utapenda






No comments:

Post a Comment