Wednesday, March 25, 2015

STUDY: Homework nyingi ni ugonjwa kwa mwanao.....MUDA WA MASOMO HAYO UKIZIDI SAA MOJA NI SHIDA....NA MTOTO HAPASWI KUSAIDIWA HOMEWORK ZAKE

Utafiti uliofanywa hivi karibuni na wanasayansi umegundua kwamba masomo ya nyumbani apewayo mwanafunzi baada ya saa za shule inashauriwa aifanye si zaidi ya dakika sitini sawa na saa moja tu ili aifanye kwa ufanisi mkubwa.

Na endapo itamchukua dakika tisini kuyafanya masomo hayo ya nyumbani matokeo yake hayatakuwa mazuri, utafiti umebaini. Utafiti mpya nao umeng’amua kwamba watoto hawapaswi kusaidiwa na walezi ama wazazi wao kufanya masomo hayo ya nyumbani.

Nao wanafunzi mara zote wamekuwa wakilalama kuwa masomo ya nyumbani yakiwa mengi ni mbaya kwao, watafiti baada ya tafiti zao wanakubaliana na malalmiko ya wanafunzi.

Kwa watoto walio katika ukuaji na wanaojisomea kwa juhudi ili kupata matokeo mazuri,waalimu hawapaswi kuandaa kazi ngumu kwa wanafunzi hao,lakini kazi ikiwa katika daraja ya kati humfanya mwanafunzi kuelewa zaidi.

Dr Javier Suarez-Alvarez anasema kwamba utafiti wao umeainisha kwamba hakuna sababu ya mwalimu kumlimbikizia mazoezi mwanafunzi,lakini ni muhimu mazoezi ya nyumbani yawe katika mpangilio ufaao kwa lengo la kumfanya mwanafunzi awe na mazoea ya kujifunza hata baada ya masomo ya darasani na hii itamsaidia kupenda,uhuru na tabia ya kujisomea yeye binafsi hata baada ya maisha ya shule .

Utafiti wa hivi karibuni,uliofanywa na chuo cha Stanford umegundua kuwa mwanafunzi afanyapo masomo ya nyumbani kwa zaidi ya saa tatu kwa usiku mmoja humfanya mwanafunzi augue.

Utafiti huo uliwahusisha wanafunzi elfu nne na mia tatu kwa wanafunzi kumi bora wa shule za serikali hata za binafsi katika jimbo la Califonia,na kuweka bayana kuwa masomo mengi ya ziada humletea mwanafunzi msongo wa mawazo na kuleta matatizo mengine ya kiafya.


Moja ya matatizo yanayotajwa ni msongo wa mawazo, lakini pia masomo ya nyumbani yakiwa lukuki humletea mwanafunzi vidonda vya tumbo,kukosa usingizi ama kupata usingizi wa mang’amung’amu,kupungua uzito wa mwili ,na kuwa mchovu muda mwingi,huu ni utafiti alioufanya Denise Pope.
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment