Tuesday, February 24, 2015

Mwanaume jela miaka 1,535 kwa kubaka wanawake 29

Hii miaka itakuacha ucheke na maandishi..
Mahakama ya Afrika Kusini imemfunga jela miaka 1,535 mwanaume mwenye umri wa miaka 35 ambaye alibaka wanawake  katika kipindi cha miaka mitano, vyombo vya habari viliripoti jana.

Kwa mujibu wa mtandao wa deccanchronicle jana, uhalifu huo wa jamaa huyo Albert Morake wa eneo la Tembisa katika Jimbo la Gauteng ulianza mwaka 2007 na kukoma mwaka 2012 wakati alipokamatwa na polisi.

Alihukumiwa kifungo cha miaka 1,535 jela na Mahakama ya Juu ya Johannesburg kutokana na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili ya jela miaka 30 kwa matukio 30 ya ubakaji, miaka 360 jela kwa matukio ya uporaji na miaka mingine mia kadhaa kwa mashtaka mengine zaidi ikiwemo kujaribu kuua, kuteka watu na ukabaji.

Vyombo vya habari vilisema kuwa, Morake ni mmoja wa watu waliofanya matukio ya ubakaji mabaya mfululizo nchini Afrika Kusini na kifungo dhidi yake ni moja ya vifungo adimu.

Watu waliowahi kubakwa, waliohudhuria sehemu ya adhabu aliyopewa mshtakiwa, walicheza kwa furaha na kukumbatiana kila mmoja.
Morake alikanusha mashtaka 175, ikiwemo kubaka watu 30, kuteka watu 41 na kukaba watu wengine 24.

Hata hivyo, alipatikana na hatia katika makosa 144. Hukumu hizo atazitumikia kwa wakati mmoa.
Jaji Rean Strydom alisema kuwa, Morake hakuonesha masikitiko na aliendelea kukanusha kuhusishwa katika matukio hayo ya uhalifu.


"Alikuwa mjinga kwa kuwashauri aliowatendea uhalifu jinsi ya kujilinda dhidi ya kubakwa siku zijazo," alinukuliwa jaji huyo akisema. Strydom alisema, wengi wa wahanga wa Morake walifanyiwa uhalifu kwa kushtukizwa na walishikwa mihemko wakati walipokuwa wakitoa ushahidi dhidi yake.

No comments:

Post a Comment