Friday, October 18, 2013

njia za kuboresha bafu lako

huwezi kukataa kuwa bafuni ni sehemu moja ndani ya nyumba ambayo inasahaulika. hata kama tunatumia muda mwingi hapo, ni rahisi kutoka kufunga mlango na kupasahau. lakini hivi karibuni nimekutana na post ambayo imeeleza jinsi rahisi ya kuboresha bafu lako.

jambo la kwanza ambalo limependekezwa ni kubadilisha taulo, vizulia na pazia kulipa bafu muonekano mpya. pia jaribu kubadilisha bomba lolote lenye kutu kwa mfano lile la mvua. ingawa hata kama utabadili pazia na kuweka taulo mpya kama vifaa vyako vya urembo vimetupwatupwa kila mahali vitalipa bafu ukakasi.
 vitu vyako vya urembo ambavyo unataka ukinyanyua mkono tu unachukua viweke pamoja itasaidia kuokoa muda na kufanya maeneo ya sinki yawe safi
kuwa na vifaa vya lazma vya usafi bafuni kama vile windex kwa ajili ya kusafishia kioo, harpic kwa kusafishia choo na vim kwa kusafishia sinki
tupa vifaa vilivyoisha muda wake na pia tosa vile ambavyo hutumii. kwa mfano utakuta kila ukinunua dawa ya meno kuna mswaki mpya, kwa hivyo usipokuwa makini unaweza kuwa na miswaki lukuki imezagaa
karatasi za chooni sio kitu maridadi cha kuonekana onekana hovyo, ila ni kitu muhimu sana. badala ya kusema uhifadhi stoo wakati ambapo huwezi kuzipata kirahisi wakati wa kutumia, weka chache ndani ya kikapu au ki bin maridadi. namna hii itaonekana nadhifu na rahisi kufikika.
hifadhi taulo za mgeni. kama hakuna mgeni kwa nini ujisumbue kuweka taulo maalum. weka bafuni zile ambazo unatumia na hizo na mgeni hifadhi mahali pengine.


No comments:

Post a Comment