Saturday, January 17, 2015
---vitu vizuri--- Hizi fremu ni cute kwa ajili ya picha za familia
fremu hizi zinafaa kuwekwa kwenye chumba chochote nyumbani, kama ni jikoni au dining unaweza kuweka michoro/picha za matunda, juice na vyakula
Thursday, January 15, 2015
my article for newspaper: mwavuli wa kwenye bustani
Fahamu haya
kabla ya kununua mwavuli wa kwenye bustani
Kwa
kawaida ya binadamu anafurahia zaidi akiwa amepumzika nje ya jengo, ndio maana
utaona kuwa sehemu nyingi za burudani iwe ni kwenye migahawa wengi wanapendelea
kukaa nje kuliko ndani. Ukishafungia watu ndani tu, wanahama kuelekea pengine
ambapo watakaa nje. Sasa basi ni nani asiyependa kuwa na wakati mzuri akiwa katika
mazingira ya nje ya nyumba yake? Imekuwa ni burudani kwa binadamu toka enzi kwa
hivyo kuwa tu na meza na viti kwenye bustani bila mwavuli hailipi.
Samani
za kwenye bustani zimetengenezwa na wataalam, na wao wanajua zaidi, kwa hivyo
nimewauliza ushauri na wakanieleza ni
aina gani za samani zinazotakiwa kwa matumizi ya wazi kwenye bustani na katika
makala hii tutatizama zaidi mwavuli wa kwenye bustani.
Mwavuli wa
kwenye bustani zaidi ya kutumika pia ni pambo eneo la nje ya nyumba Mwavuli huu
ni sahihi kwa kuwapa wenyeji na wageni kivuli siku za jua kali. Na zaidi ni
kuwa unaboresha afya, Aisha anaanza kueleza.
Kwanza
kabisa ni lazima kuwa makini sana na malighafi iliyotengenezea mwavuli. Mwavuli
wa kwenye bustani unatakiwa kuwa imara sana kwani unatumika nje ya nyumba. Unatakiwa
uwe imara vya kutosha kuhimili jua la kiangazi, mvua kubwa na upepe mkali.
Miavuli hii ni mikubwa
tofauti na ile ya kubeba mkononi na inapatikana kwa maumbo, rangi na vitambaa
mbalimbali.
Kuamua ni aina
gani ya mwavuli wa bustani utakufaa inakupasa uijue kwa undani ndipo unapoweza
kufanya uchaguzi. Eneo la kitambaa la mwavuli huu ni lile linalowakinga jua na
mvua wale walio chini yake. Mwavuli unafaa uwe wa kufunga na kufungua mithili
ya ule wa mkononi na fremu zake zipo za aluminiam, mbao na chuma. Mlingoti wa
mwavuli unene wake ni kati ya inchi moja hadi tatu. Vipande vya fremu vinavyoupa mwavuli umbo lake
na kubeba kivuli ukiwa umefunguliwa vinapaswa kuwa imara. Mbavu za mwavuli (zile
zinazoshikilia kitambaa) pia zinatakiwa ziweze kuhimili pepo za wastani hadi za
kasi. Kitako cha mwavuli kiwe na uzito wa kutosha kubeba sehemu yote ya mwavuli
iliyobakia. Ukifahamu sehemu hizi za mwavuli wa bustani itakusaidia kupata
mawazo ya kuweza kununua mwavuli sahihi na wenye vigezo na malighafi utakazo,
anasema Aisha.
Nunua mwavuli ambao
unatosha eneo unalotaka kufunika na kukupa kivuli unachotaka. Miavuli ya kwenye
bustani inasimama yenyewe, na pia haijalishi ni mtindo upi, rangi na ukubwa
miavuli hii inapatikana kwenye maduka yanayouza samani za bustanini, anasema
Aisha.
Miavuli ya
bustani inauzwa yenye milingoti ya kati ya futi 6 hadi 13 japo mzunguko wa kivuli
hauhusiani na urefu wa mwavuli. Mwavuli wa bustani mdogo sana haupendezi,
mkubwa unafaa zaidi japo unategemea na ukubwa wa eneo lako. Pima ukubwa wa
samani zako au eneo litakalofunikwa na mwavuli husika kabla ya kununua mwavuli
wenyewe.
Kwa unene wa
mlingoti, wateja wenye meza zenye tobo la mwavuli katikati wanapaswa kupima kwanza
ukubwa wa tundu kabla ya kuamua unene wa mlingoti ili kujiridhisha kuwa sio
dogo sana au kubwa zaidi. Miavuli mikubwa inahitaji uimara zaidi, na milingoti
yake inakuwa minene.
Hakuna ubishi kuwa kitambaa cha
mwavuli ndicho kinachoonekana zaidi. Wenye nyumba wengi wanapenda kuchagua
kitambaa hiki kwa kutizama rangi. Wengine hupenda kuoanisha rangi ya kitambaa hiki
na rangi nyingine za nje ya nyumba zao. Wakati hili nalo ni muhimu, wanunuzi
wanapaswa pia kuchagua kivuli cha mwavuli kuendana na malighafi za kitambaa.
Zaidi ya kuamua
rangi au michoro fulani ya kitambaa, chagua mwavuli wa bustani wenye malighafi
zitakazohimili matumizi yako, wapo ambao wanauweka mwavuli bustanini kwa
kipindi cha matumizi tu na wapo ambao mwavuli upo hapo kila siku hautolewi. Malighafi
na rangi ya kitambaa utakayochagua isiwe inapauka au kuota ukungu.
Utakapoweka
mwavuli wa bustani nje ya nyumba yako huenda ukabadili mfumo wa maisha wa mwenzi
wako akajikuta badala ya kwenda baa mnatengeneza nyama choma na kula hapo hapo
nyumbani!
Makala hii
imeandaliwa na Vivi Machange. Vivi ni mjasiriamali upande wa usafi wa magari,
nguo na mazulia; pia ana mapenzi makubwa ya muonekano wa nyumba. Kwa maoni au
maswali tuma kwenda 0755 200023 au christinesdaughter@yahoo.com
hiki kideski hiki kama una denti nyumbani ukikinunua utatamani kukibusu
basi nilikuwa naangalia jinsi denti mdogo anavyoweza kuteseka wakati wa kufanya home work yake mara apige magoti kwenye coffee table mara umwekee mito ili aifikie dining table aweze kuandika vizuri, nikafikiri ni nini suluhisho? Nikasema wacha nitembee, nikaenda keko furniture nikakutana na hiki kideski na kiti chake. Yani toka nikinunue maisha ya homework yamekuwa rahisi mno, na kila nikikiangalia natamani kukibusu yani...kama na wewe unapata shida kama nilivyokuwa mimi basi kideski kama hiki kinakuhusu...
bila kusahau alphabet na chati ya table ya kuzidisha
and Iam done with my homework, goodnight...
hayo matundu pembeni unaweza kufungua screw zake ukaongeza au kupunguza urefu wa kiti au kimeza kulingana na ukubwa wa mtoto
pia kina droo cha kuhifadhi mazagazaga yote ya skulibila kusahau alphabet na chati ya table ya kuzidisha
and Iam done with my homework, goodnight...
Sunday, January 11, 2015
Friday, January 9, 2015
balbu inapokuwa si balbu tu....
When it’s also a speaker, a WiFi repeater or a camera, obviously. All of Sengled’s special bulbs can be controlled by an app, and to save you clogging up plug sockets around the home, each serves a dual purpose.
The Pulse is a dimmable LED light that also serves as a Bluetooth speaker made by JBL. A starter pack comprising a master and a satellite bulb costs EUR179.99, and comes in three colours – red, white or silver. Once paired, you can dim and brighten all the bulbs simultaneously, and play songs from all the bulbs at the same time.
Just twist the bulb into any standard light socket, and adjust the brightness and volume from the iOS/Android app.
Alternatively, the Boost, EUR50, is another app controlled and dimmable light, but it can also increase the range of your WiFi. Just place it where you have a reasonable signal and it can throw it into ‘dead zones’ up to 100ft away.
Finally, the yet-to-be-released Snap incorporates a camera, microphone and speaker into the bulb. Snap records video and stores it in the cloud, so you can use it as a home monitor either inside or outside. Available in March 2015, it’s priced at $200, with European and UK pricing yet to be confirmed.
---vitu vizuri---hii nywele hii, kaipata toka kwa mama yake
yani Mungu anavyoumba bwana....wakati mwingine ana kipilipili cha kufa mtu (kumbuka hakuna kosa alilofanya...kakipata toka kwa wazazi wake hivi hivi wala si sawa kulaumu) mwingine anapata kama hivi...
nywele zake toka kwa mama yake na sio za kununua
anasema anatumia revlon na inauma hiyoo
steaming mara mbili kwa mwaka tu eti...watu na bahati zao
sikudanganyi ona...ni zangu na wala mama hakuchepuka na wale masingasinga waliokuwa wakitengeneza barabara....ha haaaaaa oops
magugu ni adui wa bustani yako
ukiyalazia macho magugu yanaharibu bustani nzima...... leo nimestuka jinsi mvua ilivyoyafanya yashamiri kwenye bustani yangu. halafu usijidanganye kuwa nitakapokata majani hayataonekana, bila kuondoa mizizi gugu lipo pale pale...
aina hii ya magugu yana majani mapana kuliko majani ya bustani ambayo ni aina ya canadian
haya ni magugu aina nyingine ambayo kwenye jua yanafanana kabisa na canadian grass, jinsi ya kuyagundua tu ni asubuhi wakati wa umande, huwa yenyewe magugu yanakuwa yameweka ukungu wakati canadian zinakuwa hazina, kwahivyo ukiona hivyo unajua eneo hili lina magugu.
hizi ni canadian grass ambazo hazina magugu kabisa, raha ya majani haya ya bustani huwa yanashona na ni ngumu kweli kwa gugu geni kuota, yanayokuwepo ni yale tu ambayo toka mwanzo wa kuotesha bustani mizizi ya hilo gugu ilibaki ardhini
aina hii ya magugu yana majani mapana kuliko majani ya bustani ambayo ni aina ya canadian
haya ni magugu aina nyingine ambayo kwenye jua yanafanana kabisa na canadian grass, jinsi ya kuyagundua tu ni asubuhi wakati wa umande, huwa yenyewe magugu yanakuwa yameweka ukungu wakati canadian zinakuwa hazina, kwahivyo ukiona hivyo unajua eneo hili lina magugu.
hizi ni canadian grass ambazo hazina magugu kabisa, raha ya majani haya ya bustani huwa yanashona na ni ngumu kweli kwa gugu geni kuota, yanayokuwepo ni yale tu ambayo toka mwanzo wa kuotesha bustani mizizi ya hilo gugu ilibaki ardhini
gardener wangu Claud aking'oa mzizi wa gugu
finally nimebakiwa na gugu free bustani
Thursday, January 8, 2015
my article for newspaper: chumba cha kufulia
Umuhimu wa kuwa na chumba maalum cha kufulia
ndani ya makazi yako
Nafahamu
Watanzania wachache sana (labda na wewe ni mmojawapo) ambao wamejenga nyumba
zao wakaweka chumba cha kufulia. Badala yake wanafulia nje na kwa ufinyu wa
eneo baadhi utakuta dada wa kazi kakaa juu ya sakafu ya shimo la maji taka
anafua, na hata wakati mwingine pakiwa na harufu mbaya lakini hana mahali
pengine pa kufulia maskini. Au kwa baadhi ya wale wenye mashine za kufulia
aidha wameziweka kwenye varanda uani au bafuni lakini sio kuwa pametengenezwa
maalum kwa kufulia.
Baadhi hawataki kukubaliana moja kwa
moja kuwa kuna umuhimu wa kuwa na chumba cha kufulia kwenye makazi yao. Lakini
wewe mwenye nyumba utakapoamua kujumuisha chumba cha kufulia kwenye makazi yako
ndipo utakapogundua ni nini ulichokuwa unakosa! Utakiona chumba hiki kama moja
ya vyumba muhimu zaidi kwako.
Ni
mazoea ya wengi kuwa na mahali pa kufulia “huko nje” na lugha inayotumika ni peleka nje hizi nguo
za kufua. Kwa miaka mingi kwa Watanzania walio wengi kuwa na chumba cha kufulia kwenye makazi yao ni jambo
lisilotiliwa maanani, limedharaulika au na pia kusahaulika, na mahali pa kufulia
ni popote tu hapo nyumbani ambako wewe
mfuaji utakapoona panakufaa kwa wakati husika…iwe ni uani, juu ya karo la maji
taka, chini ya mti na wakati mwingine bafuni.
Asante
kwa teknolojia na utandawazi ambapo baadhi ya wenye nyumba wameanza kutenga
chumba cha kufulia kwenye nyumba zao.
Kwa miaka ya karibuni baadhi ya wenye nyumba na wajenzi wanatizama uwezekano wa
kujumuisha chumba cha kufulia kwenye makazi. Chumba hiki kinatakiwa kiwe na
eneo la kuhifadhia, sinki, uwezo ukiwepo mashine ya kufulia na bila kusahau
mahali pa kunyooshea.
Umuhimu wa sinki bado ni mkubwa hata kama utaweka mashine kwani si kila nguo
itafuliwa kwenye mashine na pia kuna swala la kuloweka na kuosha viatu vyenye
udongo.
Lakini haijalishi ni maridadi namna gani chumba hiki kinavyoonekana, jambo la msingi linabaki lilelile kuwa ni mahali pa mchakato mzima wa kubadili nguo chafu ziwe safi na kuvalika tena ambapo ni pamoja na kuloweka, kufua, kunyoosha na kuhifadhi kwa muda.
Je, unaonaje kama kwenye eneo la makazi yako iwe unajenga sasa au ni makazi ya zamani ukawa na chumba cha kufulia? Na je unafahamu kuwa unaweza kukidizaini mwenyewe? Chumba cha kufulia kina majukumu yote ya kufanya mchakato wa kufua nguo uwe rahisi, pia kumbuka ni muhimu kiwe jirani na kamba za kuaniakia.
Hakikisha kwenye chumba chako hicho maalum cha kufulia una mahali pa kutundika nguo na tumia hanger za plastiki, hizi zinafaa zaidi kwani hazipati kutu au kujikunja pale nguo inapokuwa nzito.
Kwa matumizi mazuri ya nafasi unaweza kujenga kaunta la zege juu ya mashine ya kufulia ambapo ndipo utakapokuwa unanyooshea nguo. Kwa maana hiyo mashine yako inabidi iwe ni ile ya kujazia nguo kwa mlango wa mbele (front load) na sio juu (top load). Hii itaokoa eneo ambalo ungeweka meza ya kunyooshea.
Msisitizo
maalum uwekwe kwenye muundo wa chumba hiki kuhakikisha kuwa kila mahali kuna
mwanga wa kutosha, kwa mfanyo huwezi kufua kwa mikono penye mwanga hafifu na
pia huwezi kunyooshea pasipo na mwanga wa kutosha. Ikiwezekana kuweka mlango wa
kioo ni njema zaidi.
Chumba cha kufulia kinafaa kiwe na
mvuto! Rangi nzuri za mwanga ukutani kama bluu au njano isiyokoza itaongeza
muonekano. Sakafu yake iwe kavu na pia chumba hiki hakitakiwi kuwa kimepooza.
Kuweka chanzo cha burudani kama vile radio inaweza kukifanya kiwe sehemu ya
burudani zaidi kuwepo na kutomchosha mfuaji wakati nguo zikiendelea kutakata.
Chumba chako cha kufulia
kinatavyokuwa na mvuto huenda kikamfanya mwenzi wako asiyependa kufua aanze
kufua. Na kama ndio hivyo, ni ukweli kuwa kinaweza kuwa chumba kizuri zaidi
hapo nyumbani!
Makala
hii imeandaliwa na Vivi O. Machange. Vivi ni mjasiriamali upande wa usafi wa
magari, nguo na mazulia; pia ana mapenzi makubwa ya muonekano wa makazi. Kwa
maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au christinesdaughter@yahoo.com
habari ya mtambo wa kubadilisha maji kutoka kwenye chumvi kwenda yasiyo na chumvi ni njema kuliko!
Yani nilipoona habari hii nimetamani kama wangezindua pia vimtambo vidogo kwa ajili ya majumbani. Watu wengi wengi hawana uhakika wa maji safi na salama, na huwa naamini suluhisho kamili na la kudumu ni kuchimba kisima, ila tatizo sasa linakuja kuwa asilimia kubwa ya maji ya visima ni ya chumvi. Sasa hili la kuweza kuwa na mtambo wa kuyabadilisha toka kwenye chumvi kwenda yasiyo na chumvi (safi na salama) ni njema sana kwakweli. Process ya kubadili maji ya chumvi kwenda yasiyo na chumvi inaitwa desalination.
soma hapa:
Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (Gavu)akitoa hotuba wakati alipofungua mtambo wa kubadilishia maji kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.kulia yake nimuakilishi wa Taasisi ya Mork Water Solution ya Ujarumani Mikalen na kushoto yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Idriss Muhsin Hijja.
Wananchi mbalimbali wakinywa maji yaliobadilishwa kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama baada ya kufunguliwa huko Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar
soma hapa:
Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (Gavu)akitoa hotuba wakati alipofungua mtambo wa kubadilishia maji kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.kulia yake nimuakilishi wa Taasisi ya Mork Water Solution ya Ujarumani Mikalen na kushoto yake ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Idriss Muhsin Hijja.
Wananchi mbalimbali wakinywa maji yaliobadilishwa kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama baada ya kufunguliwa huko Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar
Wednesday, January 7, 2015
--nitavukaje--Wajasiriamali waombwa kuchangamkia fursa
haya tena kwa wewe unayetaka kuvuka daraja hilo chukua hatua fastaaa.
Wednesday, January 7 2015, 0 : 0
Wednesday, January 7 2015, 0 : 0
WAJASIRIAMALI mbalimbali nchini wameombwa kuchangamkia fursa kwa
kuchukua fomu za kushiriki programu ya shindano la ujasiriamali linalojulikana
kama 'Safari Lager Wezeshwa' ili waweze kujinyakulia vitendea kazi vya aina
mbalimbali ikiwemo trekta lenye thamani ya sh. milioni 220.
Wito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Meneja Mpya wa Bia ya Safari
Lager, Edith Bebwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu programu
hiyo ya awamu ya nne ambayo imelenga zaidi kwa wajasiriamali nchini kujitokeza
kuchukua fomu hizo.
"Awali tuliwaeleza wajasiriamali kuwa na subira wakati fomu hizo
zikiandaliwa lakini tunachoweza kusema ni kwamba hivi sasa fomu ziko tayari
wanaweza kuzipata katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mabohari ya
TBL,"alisema Bebwa.
Alisema pia fomu hizo ziko kwa mawakala wa kusambaza bia, kwenye
mitandao na kusema kuwa ni wakati mwafaka kwa wajasiriamali kuchukua fomu hizo
na kuzijaza tayari kwa kushiriki rasmi shindano hilo.
Bebwa alisema kuwa mara baada ya wajasiriamali hao kumaliza kujaza fomu
hizo ni vyema wakazirejesha kwenye vituo vilivyotajwa au maeneo
walipozichukulia na kusema kuwa wajasiriamali wadogo wadogo nchini kuhakikisha
wanachangamkia fursa hiyo kwani hiyo ni hazina tosha.
"Ninasema hivi kutokana na kwamba hii itarahisisha kazi kwa kuwepo
kwa vitendea kazi bila ya kutumia nguvu nyingi kwao kutokana na kwamba kwa
wajasiriamali ambao wamefanikiwa kushiriki na kushinda wamepata mafanikio
makubwa,"alisema.
Kiongozi wa wataalam wa Ushauri wa Biashara kutoka Kampuni ya TAPBDS
Joseph Migunda, alisema kuwa programu hiyo inatarajia kufanyika takribani mikoa
yote ambapo itawapa fursa wajasiriamali wa aina zote fursa bila kujali fani, kabila
wala jinsia bali wanatakiwa kujaza fomu kwa usahihi na umri usiopungua miaka
18-40.
Alisema kwa wale wenye nia ya kufika mbali kibiashara na wenye malengo
ya kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite kuchangamkia fursa hiyo na kwamba
kwa wale watakaofanikiwa kuibuka kidedea watapata mafunzo mafupi ya awali
pamoja na kukabidhiwa ruzuku zao.
Tuesday, January 6, 2015
Monday, January 5, 2015
laundry talk : umuhimu wa kuwa na chumba maalum cha kufulia
Nafahamu watu wachache sana (labda na wewe ni mmojawapo) ambao
wamejenga nyumba zao wakaweka chumba cha kufulia. Badala yake wanafulia nje
wengine utakuta dada kakaa juu ya sakafu ya shimo la maji taka anafua, na hata
wakati mwingine pakiwa na harufu mbaya lakini hana mahali pengine pa kufulia
maskini. Au kwa baadhi ya wale wenye mashine za kufulia aidha wameziweka kwenye
varanda uani au bafuni lakini sio kuwa pametengenezwa maalum kwa kufulia.
Je, unaonaje kama kwenye eneo la makazi
yako iwe unajenga sasa au ni makazi ya zamani ukajumuisha chumba cha kufulia?
Na je unafahamu kuwa unaweza kukidizaini mwenyewe? Ni Kiasi tu cha kuwa na eneo la kunyooshea,
kutundika nguo zilizonyooshwa na vishelfu viwili vitatu vya kuweka nguo
zilizokunjwa.
Kwenye chumba hiki kama utakuwa na washing mashine, plumber
atakufungia miundombinu yake, au kama haipo basi jenga laundry sink linatosha
sana tu (japo kidogo kikubwa ni majaliwa…ha ha haa). Zaidi ya yote usisahau
eneo la kuweka kapu la nguo chafu.
Heri ya mwaka mpya rafiki…ujumbe huu utakutia moyo. “ If 2014 didn’t
end the way you planned don’t lose hope. Just remember God has created 2015 for
you to start again. The best is yet to come, for sure life never seems to be
the way we want, but we live in it the best way we can. There is no perfect life but we can fill it
with perfect moments.”
my everyday life: mtoto shule mzazi shule
yani mchaka mchaka wa watoto kwenda shule ni kama na mzazi unasoma vilevile....watu wangu wadogo wameshazianza mbio za 2015, usingizi wa asubuhi iz no more...
jamani ni mambo ya wake up with giza yameanza tena, masikitiko mweee
kweli na kimvua mvua hiki kweli, usingizi ungenoga sana
any way wacha tu twende ni kwa faida yetu
Saturday, January 3, 2015
Friday, January 2, 2015
nimemalizia mwaka kwa kutembelea waterfalls za kinukamori
Basi sikukuu hii nilifanikiwa kwenda kupumzika na kusheherekea katika eneo nilipokulia, shughuli zilikuwa ni mbili tu ambazo ni kulala na umbea bhaaasi. Kunako stori stori kukawa na hili lililonishtua la wanafunzi wawili binti na kaka yake waliokutwa wamefariki mtoni huko Marangu. Kukawa na maneno mengi kuwa walienda kuogelea wakavutwa na chunusi. Nikajisemea wacha niende nikajionee mambo hayo. Nikafikia kwenye eneo moja la mto marangu ambapo kuna waterfalls zinazoitwa Kinukamori.
Nikataka kujua historia ya eneo hili na nikaambiwa kuwa ni juu ya binti mmoja Makinuka, wa kabila la kichaga aliyepata mimba kabla ya ndoa kwa hivyo kwa jinsi mila zilivyokuwa zinalaani jambo hilo akaamua kwenda mahali hapo ili ajiue. Tour guide akaendelea kunieleza kuwa kwa kichaga Kinuka inamaanisha pori, na Mori ndio huyo chief aliyekuwa anamiliki hilo pori.
Twenda pamoja basi uone picha na maelezo ya tukio zima na huenda ukitembelea Moshi utavutiwa kwenda Kinukamori waterfalls...
Kinasanamu kinakuambia huruhusiwi kukojoa hapa, usipokuwa makini unaweza kudhani ni mtu kweli anamwaga susu..
Sanamu la Makinuka kashaingia porini kwa Mori akitaka kujiua. Hapo aliposimaa mbele yake kuna shimo kubwa lililofanya haya maporomoko, na ndipo alipojirusha akafa.
Baba yake Makinuka akitazama mwanaye alipofia.
Mama Makinu akisikitika kifo cha bintiye.
Ngazi za kushuka kuzunguka kuona maporomoko, ni mwendo wa kati ya dakika kumi hadi kumi na tano ndipo ufike chini.
waterfalls yenyewe..ukitazama kwa juu kule unamuona makinuka akiwa tayari kujirusha. tg alisema urefu wa haya maporomoko ni kama mita mia, ni parefu eti
hapa ni upande wa juu wa mto kabla ya maporomoko, ni eneo hatari hili, ukiteleza ama mtoto akiwa anakimbia Mungu pitishia mbali anadumbukia kwenye lile shimo, kwakuwa kwa mbali unaona tu ni kama mto unapita lakini kwa mbele ni shimo kubwa sana, hadi uzunguke kwenye zile ngazi ndio unaweza elewa mbele kuna nini. Sasa watembeleaji wanakazana kupiga picha na Makinuka ndio wanaanguka na kufa pale na sio chunusi wala nini. Pameandikwa usikatize, lakini wengine hawasikii na pia wapo wanokuja wakiwa wamelewa.
baadhi ya wageni wanakuja na magodoro na matents na kuweka camp
yeiiii, nimefika...happy 2015, ujumbe wangu kwako ni usikubali mtu akuibie furaha yako....
mambo ya utalii wa ndani, hawa wote wamekuja kushangaa kinukamori falls
wageni ni wengi mnapishhana tu kwenye ngazi kupandisha na kushuka
cottage ipo ila wengi wanapendelea kufunga tents....mwisho
Nikataka kujua historia ya eneo hili na nikaambiwa kuwa ni juu ya binti mmoja Makinuka, wa kabila la kichaga aliyepata mimba kabla ya ndoa kwa hivyo kwa jinsi mila zilivyokuwa zinalaani jambo hilo akaamua kwenda mahali hapo ili ajiue. Tour guide akaendelea kunieleza kuwa kwa kichaga Kinuka inamaanisha pori, na Mori ndio huyo chief aliyekuwa anamiliki hilo pori.
Twenda pamoja basi uone picha na maelezo ya tukio zima na huenda ukitembelea Moshi utavutiwa kwenda Kinukamori waterfalls...
naianza safari
Kinasanamu kinakuambia huruhusiwi kukojoa hapa, usipokuwa makini unaweza kudhani ni mtu kweli anamwaga susu..
Sanamu la Makinuka kashaingia porini kwa Mori akitaka kujiua. Hapo aliposimaa mbele yake kuna shimo kubwa lililofanya haya maporomoko, na ndipo alipojirusha akafa.
Baba yake Makinuka akitazama mwanaye alipofia.
Mama Makinu akisikitika kifo cha bintiye.
Ngazi za kushuka kuzunguka kuona maporomoko, ni mwendo wa kati ya dakika kumi hadi kumi na tano ndipo ufike chini.
waterfalls yenyewe..ukitazama kwa juu kule unamuona makinuka akiwa tayari kujirusha. tg alisema urefu wa haya maporomoko ni kama mita mia, ni parefu eti
hapa ni upande wa juu wa mto kabla ya maporomoko, ni eneo hatari hili, ukiteleza ama mtoto akiwa anakimbia Mungu pitishia mbali anadumbukia kwenye lile shimo, kwakuwa kwa mbali unaona tu ni kama mto unapita lakini kwa mbele ni shimo kubwa sana, hadi uzunguke kwenye zile ngazi ndio unaweza elewa mbele kuna nini. Sasa watembeleaji wanakazana kupiga picha na Makinuka ndio wanaanguka na kufa pale na sio chunusi wala nini. Pameandikwa usikatize, lakini wengine hawasikii na pia wapo wanokuja wakiwa wamelewa.
baadhi ya wageni wanakuja na magodoro na matents na kuweka camp
yeiiii, nimefika...happy 2015, ujumbe wangu kwako ni usikubali mtu akuibie furaha yako....
mambo ya utalii wa ndani, hawa wote wamekuja kushangaa kinukamori falls
wageni ni wengi mnapishhana tu kwenye ngazi kupandisha na kushuka
cottage ipo ila wengi wanapendelea kufunga tents....mwisho
Tuesday, December 23, 2014
My Article for Newspaper: Malengo ya 2015 Nyumbani Kwako
Mazingira
ya nyumbani kwako yasaidie kufanikisha maazimio yako ya mwaka mpya
Ni wakati
mwingine tena wa mwaka ambao wengi wetu wanapenda kufanya mabadiliko kwenye
maisha yao . Je
umeshafikiria mabadiliko ya mwaka mpya kwa ajili ya kiota chako? Japo mabadiliko
haya yanajulikana na wengi zaidi kama
maazimio, kwa kutia msisitizo zaidi makala hii itayaita malengo. Malengo
yanatamkwa kwa kusisitiza wakati uliopo ni nini tamanio lako (kwa mfano kuamua
kubadili mpangilio wa fenicha za sebuleni kwako ili kuwezesha kunogesha zaidi
mazungumzo) wakati maazimio yanatamka ni nini ungependa huko mbeleni ya kuwa
unaenda kufanya nini wakati ujao.
Mara
nyingi malengo (au maazimio) ya mwaka mpya yanatupiliwa mbali hata kama nguvu za kutosha ziliwekwa ili kuhakikisha
yanafanikiwa. Moja ya sababu za malengo kutofanikiwa ni mazingira ya nyumbani
kwako kutosaidia kuwezesha mafanikio ya malengo hayo. Kama
unataka kufanya mabadiliko ndani ya maisha yako bila kuhusisha mazingira yako
kufanikiwa ni mbinde. Kwa maana ya kwamba kama unaweka malengo yako ya mwaka
2015 kwa ajili ya makazi yako na ukayaacha mazingira yalivyo, ni ngumu sana
kubadili chochote. Hata matangazo kwa mfano ya kujikinga na maambukizi ya VVU
yanaonyesha uhusiano kati ya maambukizi na mazingira fulani ambayo yanachochea
maambukizi hayo.
Kanuni ya
malengo kuwa na uhusiano na mazingira inahusika karibia katika kila kitu. Kama unataka mwaka huu uwe tofauti basi unatakiwa kuweka
mazingira ya kuwezesha malengo yako.
Je
mazingira yako yanakusaidia kupata kile unachokihitaji? Kwenye mazingira ya
nyumbani kwako vitu ambavyo havijakaa mahali pake au vimekaa mahali ambapo
havifanyi kazi yake au havitumiki tena vinakukwamisha kutimiza malengo yako
hapo nyumbani. Tembelea kwenye makabati ya nguo na vyombo angalia kwa umakini
kuona ni vitu gani vya kuhifadhi, vya kugawa ama vya kutupa. Fanya hivyo kwa
nia ya kupata nafasi ya kile tu kitakachosaidia kufanikisha malengo yako.
Pengine
lengo lako la mwaka mpya ni kutokula hovyo kwa nia ya kupungua uzito. Je mara
zote unaingia nyumbani kwa kupitia mlango wa nyuma ambapo unaingilia moja kwa
moja jikoni? Kumbuka kanuni kuwa unachokiona mwanzo kinagusa zaidi akili yako,
kwa hiyo kama mara ungiapo ndani unakutana na jokufu, chakula na kadhalika
utapata hamu ya kula hapo hapo.
Mahusiano
mengi yanaweza kuboreshwa kwa mapambo ya nyumbani hasa katika swala la
kuwasiliana. Je chumba cha kulala cha wakuu wa familia ni mahali patakatifu kwa
wawili? Hakikisha vitu kama taa, vimeza, na
viti kwenye chumba hicho viko viwili viwili.
Au lengo
lako mwaka mpya ni kuwa na wageni wengi zaidi nyumbani? Hakikisha basi mlango
wa mbele unaonekana na kuna njia ya wazi ya kuingilia. Taa zinazomulika njia ya
kuelekea mlango huo ziwe zinafanya kazi. Pitia mlango wa mbele kama mgeni
mtarajiwa uone kama kila kitu kiko sawa. Je
njia hiyo inakaribisha? Na sebule yako je nayo inavutia kwa ajili ya wageni
wako wengi ambao unapenda kuwaalika nyumbani mwaka mpya ?
Kwa wale ambao
azimio lao kuu la mwaka 2015 ni kupamba nyumba zao hakikisha unachagua rangi
kwa umakini, fikiria mpangilio wa fenicha je zinawatendea haki watumiaji wa
chumba husika. Angalia vitu ambavyo inabidi uvifanyie kazi ili kuboresha
muonekano wa makazi yako. Kama kwa mfano sakafu ya sebule yako ni ya marumaru
na unachoka kusugua na kusafisha kila siku na unakiri kuwa ni ngumu kuifanya
iwe safi; basi weka zulia kubwa ambapo utasafisha kwa mashine ya upepo mara
mbili au tatu kwa wiki.
Ikiwa
unaazimia kutojaza vyombo vichafu kwenye karo basi mwaka ujao lenga kuosha
chombo mara baada ya kukitumia. Na hata hakikisha wanafamilia wengine pia
wanafanya hivyo.
Huenda
kijani kinakubariki lakini huna eneo kubwa ya kuweza kuwa na bustani za
ardhini. Otesha basi bustani za kwenye vyungu walau ukifungua pazia la chumba
cha kulala kunapopambazuka ukutane na kijani. Azimia kupamba ndani mwako kwa maua freshi japo mara moja
kwa mwezi.
Kweli,
baadhi ya mabadiliko ya nyumbani kwako unaweza kuhitaji kutafuta msaada, lakini
kuna mabadiliko mengi sana ambayo hayahitaji gharama lakini yanahitaji muda na
nguvu ( na pengine kaujuzi) kwahiyo kwa
2015 kwa nini usiazimie kupamba mwenyewe? Unaonaje? Ni azimio moja zuri kwa
ajili ya makazi yako ambalo unaweza kutekeleza. Fanya usafi mkubwa ndani ya
nyumba yako mara moja kwa mwezi ( weka tarehe kwenye kalenda yako na
isismamie). Mwanamke unatakiwa upende usafi na usiwe mvivu. Shirikisha na
wanafamilia wengine pia.
Hii
inaweza isikubalike kwa baadhi ya watu ila ni mawazo binafsi kuwa azimia kila
anayeingia ndani avue viatu mlangoni. Viatu vya wanawake vilivyo na visigino
vya ncha kali mara nyingine vinakwaruza sakafu za marumaru na mbao na
kuacha alama na vile vya wanaume baadhi vina soli zinazoacha rangi sakafuni na
hivyo kufanya sakafu ionekane zee kuliko kawaida.
Mwaka huu
lenga kuweka nyumba yako nadhifu kila mara kama
vile unategemea mgeni wa heshima!
Makala hii imeandaliwa na Vivi O. Machange. Vivi
ni mjasiriamali upande wa usafi wa magari, nguo na mazulia; pia ana mapenzi
makubwa ya muonekano wa makazi. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au
christinesdaughter@yahoo.com
Monday, December 22, 2014
Laundry Talk: Umuhimu wa Kutumia Bleach
As ninafanya biashara ya dry cleaning na laundry nimeona kuwa hakuna mbaya nikiwa na share na wewe tips za mambo hayo. So kuna mambo elfu moja na moja kidogo ya kuongelea kuhusu usafi wa nguo tatizo nadhani ni muda mchache uliopo!
Naanza na kwanini tutumie bleach? Nyeupe zizidi kuwa nyuepe zaidi, inaondoa udongo na inaua vijidudu.
Zaidi ya maelezo ya kwenye chupa bleach inatakiwa kuchanganywa na maji kabla ya kusweka nguo endapo unafua kwa mkono, baadhi ya watu kwa kutojua wanaweka nguo kwanza halafu wanamimina bleach juu ya nguo, hii ni makosa as inaweza kuunguza nguo endapo utaimimina moja kwa moja juu ya nguo.
Of course, kama unatumia mashine una ile sehemu ya ku dispense bleach, kwa hivyo unamimina tu pale kwa maana hiyo huna haja ya kuchanganya maji na bleach manually.
Kabla hujatumia bleach kwenye nguo hakiksha kwanza unasoma label ya nguo, kwa ajili kuna baadhi zinasema kabisa "No Bleach" - kwa maana hiyo usitumie bleach kwenye nguo yenye label inayosema hivi.
Na usisahau kuwa kuna bleach za kutumia kwenye nguo za rangi pia ...watu wengi hawajui hili, kwa mfano unaona zile chupa za jik za rangi ya bluu? hizi ni kwa ajili ya nguo za rangi.
TAHADHARI wakati wa kutumia bleach - kuna dondoo mbalimbali zinatolewa kwa ajili ya kufua nguo zitakate zaidi kama vile kutumia limao, vinegar na kadhalika. Kuchanganya vitu hivi na bleach kunaweza kuzalisha kemikali zitakazoharibu nguo zako, ambapo usingependa litokee hili.
Subscribe to:
Posts (Atom)








