Monday, January 5, 2015

laundry talk : umuhimu wa kuwa na chumba maalum cha kufulia


Nafahamu watu wachache sana (labda na wewe ni mmojawapo) ambao wamejenga nyumba zao wakaweka chumba cha kufulia. Badala yake wanafulia nje wengine utakuta dada kakaa juu ya sakafu ya shimo la maji taka anafua, na hata wakati mwingine pakiwa na harufu mbaya lakini hana mahali pengine pa kufulia maskini. Au kwa baadhi ya wale wenye mashine za kufulia aidha wameziweka kwenye varanda uani au bafuni lakini sio kuwa pametengenezwa maalum kwa kufulia.

Je, unaonaje kama kwenye eneo la makazi yako iwe unajenga sasa au ni makazi ya zamani ukajumuisha chumba cha kufulia? Na je unafahamu kuwa unaweza kukidizaini mwenyewe? Ni  Kiasi tu cha kuwa na eneo la kunyooshea, kutundika nguo zilizonyooshwa na vishelfu viwili vitatu vya kuweka nguo zilizokunjwa.

Kwenye chumba hiki kama utakuwa na washing mashine, plumber atakufungia miundombinu yake, au kama haipo basi jenga laundry sink linatosha sana tu (japo kidogo kikubwa ni majaliwa…ha ha haa). Zaidi ya yote usisahau eneo la kuweka kapu la nguo chafu.

Heri ya mwaka mpya rafiki…ujumbe huu utakutia moyo. “ If 2014 didn’t end the way you planned don’t lose hope. Just remember God has created 2015 for you to start again. The best is yet to come, for sure life never seems to be the way we want, but we live in it the best way we can.  There is no perfect life but we can fill it with perfect moments.”


No comments:

Post a Comment