haya tena kwa wewe unayetaka kuvuka daraja hilo chukua hatua fastaaa.
Wednesday, January 7 2015, 0 : 0
Wednesday, January 7 2015, 0 : 0
WAJASIRIAMALI mbalimbali nchini wameombwa kuchangamkia fursa kwa
kuchukua fomu za kushiriki programu ya shindano la ujasiriamali linalojulikana
kama 'Safari Lager Wezeshwa' ili waweze kujinyakulia vitendea kazi vya aina
mbalimbali ikiwemo trekta lenye thamani ya sh. milioni 220.
Wito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Meneja Mpya wa Bia ya Safari
Lager, Edith Bebwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu programu
hiyo ya awamu ya nne ambayo imelenga zaidi kwa wajasiriamali nchini kujitokeza
kuchukua fomu hizo.
"Awali tuliwaeleza wajasiriamali kuwa na subira wakati fomu hizo
zikiandaliwa lakini tunachoweza kusema ni kwamba hivi sasa fomu ziko tayari
wanaweza kuzipata katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye mabohari ya
TBL,"alisema Bebwa.
Alisema pia fomu hizo ziko kwa mawakala wa kusambaza bia, kwenye
mitandao na kusema kuwa ni wakati mwafaka kwa wajasiriamali kuchukua fomu hizo
na kuzijaza tayari kwa kushiriki rasmi shindano hilo.
Bebwa alisema kuwa mara baada ya wajasiriamali hao kumaliza kujaza fomu
hizo ni vyema wakazirejesha kwenye vituo vilivyotajwa au maeneo
walipozichukulia na kusema kuwa wajasiriamali wadogo wadogo nchini kuhakikisha
wanachangamkia fursa hiyo kwani hiyo ni hazina tosha.
"Ninasema hivi kutokana na kwamba hii itarahisisha kazi kwa kuwepo
kwa vitendea kazi bila ya kutumia nguvu nyingi kwao kutokana na kwamba kwa
wajasiriamali ambao wamefanikiwa kushiriki na kushinda wamepata mafanikio
makubwa,"alisema.
Kiongozi wa wataalam wa Ushauri wa Biashara kutoka Kampuni ya TAPBDS
Joseph Migunda, alisema kuwa programu hiyo inatarajia kufanyika takribani mikoa
yote ambapo itawapa fursa wajasiriamali wa aina zote fursa bila kujali fani, kabila
wala jinsia bali wanatakiwa kujaza fomu kwa usahihi na umri usiopungua miaka
18-40.
Alisema kwa wale wenye nia ya kufika mbali kibiashara na wenye malengo
ya kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite kuchangamkia fursa hiyo na kwamba
kwa wale watakaofanikiwa kuibuka kidedea watapata mafunzo mafupi ya awali
pamoja na kukabidhiwa ruzuku zao.
No comments:
Post a Comment