Friday, January 2, 2015

nimemalizia mwaka kwa kutembelea waterfalls za kinukamori

Basi sikukuu hii nilifanikiwa kwenda kupumzika na kusheherekea katika eneo nilipokulia, shughuli zilikuwa ni mbili tu ambazo ni kulala na umbea bhaaasi. Kunako stori stori kukawa na hili lililonishtua la wanafunzi wawili binti na kaka yake waliokutwa wamefariki mtoni huko Marangu. Kukawa na maneno mengi kuwa walienda kuogelea wakavutwa na chunusi. Nikajisemea wacha niende nikajionee mambo hayo. Nikafikia kwenye eneo moja la mto marangu ambapo kuna waterfalls zinazoitwa Kinukamori.

Nikataka kujua historia ya eneo hili na nikaambiwa kuwa ni juu ya binti mmoja Makinuka, wa kabila la kichaga aliyepata mimba kabla ya ndoa kwa hivyo kwa jinsi mila zilivyokuwa zinalaani jambo hilo akaamua kwenda mahali hapo ili ajiue.  Tour guide akaendelea kunieleza kuwa kwa kichaga Kinuka inamaanisha pori, na Mori ndio huyo chief aliyekuwa anamiliki hilo pori.

Twenda pamoja basi uone picha na maelezo ya tukio zima na huenda ukitembelea Moshi utavutiwa kwenda Kinukamori waterfalls...
 naianza safari


Kinasanamu kinakuambia huruhusiwi kukojoa hapa, usipokuwa makini unaweza kudhani ni mtu kweli anamwaga susu..
Sanamu la Makinuka kashaingia porini kwa Mori akitaka kujiua. Hapo aliposimaa mbele yake kuna shimo kubwa lililofanya haya maporomoko, na ndipo alipojirusha akafa.
 Baba yake Makinuka akitazama mwanaye alipofia.
 Mama Makinu akisikitika kifo cha bintiye.
Ngazi za kushuka kuzunguka kuona maporomoko, ni mwendo wa kati ya dakika kumi hadi kumi na tano ndipo ufike chini.
 waterfalls yenyewe..ukitazama kwa juu kule unamuona makinuka akiwa tayari kujirusha. tg alisema urefu wa haya maporomoko ni kama mita mia, ni parefu eti
 hapa ni upande wa juu wa mto kabla ya maporomoko, ni eneo hatari hili, ukiteleza ama mtoto akiwa anakimbia Mungu pitishia mbali anadumbukia kwenye lile shimo, kwakuwa kwa mbali unaona tu ni kama mto unapita lakini kwa mbele ni shimo kubwa sana, hadi uzunguke kwenye zile ngazi ndio unaweza elewa mbele kuna nini. Sasa watembeleaji wanakazana kupiga picha na Makinuka ndio wanaanguka na kufa pale na sio chunusi wala nini. Pameandikwa usikatize, lakini wengine hawasikii na pia wapo wanokuja wakiwa wamelewa.
 baadhi ya wageni wanakuja na magodoro na matents na kuweka camp


 yeiiii, nimefika...happy 2015, ujumbe wangu kwako ni usikubali mtu akuibie furaha yako....
mambo ya utalii wa ndani, hawa wote wamekuja kushangaa kinukamori falls
 wageni ni wengi mnapishhana tu kwenye ngazi kupandisha na kushuka
cottage ipo ila wengi wanapendelea kufunga tents....mwisho

No comments:

Post a Comment