Yani nilipoona habari hii nimetamani kama wangezindua pia vimtambo vidogo kwa ajili ya majumbani. Watu wengi wengi hawana uhakika wa maji safi na salama, na huwa naamini suluhisho kamili na la kudumu ni kuchimba kisima, ila tatizo sasa linakuja kuwa asilimia kubwa ya maji ya visima ni ya chumvi. Sasa hili la kuweza kuwa na mtambo wa kuyabadilisha toka kwenye chumvi kwenda yasiyo na chumvi (safi na salama) ni njema sana kwakweli. Process ya kubadili maji ya chumvi kwenda yasiyo na chumvi inaitwa desalination.
soma hapa:
Naibu Waziri wa Miundo mbinu na
Mawasiliano Issa Haji Ussi (Gavu)akitoa hotuba wakati alipofungua mtambo
wa kubadilishia maji kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama Uzi
Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya
miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar.kulia yake nimuakilishi wa Taasisi ya
Mork Water Solution ya Ujarumani Mikalen na kushoto yake ni Mkuu wa Mkoa
wa Kusini Idriss Muhsin Hijja.
Wananchi mbalimbali wakinywa maji
yaliobadilishwa kutoka kwenye chumvi na kuwa safi na salama baada ya
kufunguliwa huko Uzi Ng'ambwa Wilaya ya kati Unguja ikiwa ni shamra
shamra za maadhimisho ya miaka 51ya Mapinduzi ya Zanzibar
No comments:
Post a Comment