Ni
swali ambalo hatujiulizi sana lakini inabidi tujiulize. Ni vizuri tuwekane sawa
kuwa tendo la kupamba nyumba ni la kibunifu na ni muhimu. Lina nia ya kuleta
mpangilio kwenye maisha ili kujitoa kwenye mvurugano na machafuko ya jumla ya duniani,
kuweza kuweka nguvu zetu za kupamba hata hapo padogo tunapoishi ambapo tuna uwezo
napo.
Kwa
kufanya hivyo tunaonyesha na
kuwafundisha watoto wetu somo zuri. Kama vile: umuhimu
wa kuweka na kuacha vitu kwenye mpangilio mzuri kuliko walivyovikuta, kwa
ukweli kwamba kila kitu kinaweza kubadilishwa kwa uzuri zaidi, kwamba kuweka mpangilio
kwenye maisha ni muhimu, kwamba vitu vinavyoonekana kwa macho vinahusika na kwamba
baada ya kukamilisha lolote una cha kujivunia.
Ni
sanaa ya kutengeneza mahali petu wenyewe pawe kama patakatifu na kushirikishana
eneo letu na wengine.
Kama muundaaji wa makala hii, huwa nafurahishwa ninapotembelea makazi ya watu na kuona jinsi nyumba ya mtu mmoja inavyoweza kutofautiana kabisa kimpangilio na ya mtu mwingine ingawaje maeneo ya msingi ni yale yale.
Tukijua
ni kwanini tunapamba itatufanye tupende kuendelea kupamba. Kupamba nyumba ni
kama kitu kingine chochote kwenye maisha. Ni kama unavyouweka mwili na nguo zako
katika usafi na mpangilio. Ukishajua mkakati wako utapata mwelekeo.
Badala
ya kubuni ni kwanini unataka hiyo rangi, ni kiti kipi kinakufaa au ni kwa namna
gani uweke fenicha zako – unatakiwa kuwa na sababu kubwa ya muongozo wa kwanini
unafanya chochote unachotaka kufanya.
Kwahivyo
baada ya kusema yote haya hizi hapa chini ni sababu za kawaida za kwanini tunapamba.
Zifurahie na elewa msukumo wako, na naamini itakusaidia kuwa mpambaji mzuri wa
mahali unapoishi.
Tunapamba
ili kufanya nyumba zetu ziwe rahisi kuishi ndani mwake na kurahisisha maisha
yetu.
Tunapamba
ili kuleta mazingira ambayo yanatamanisha kujifunza, upendo, furaha na mshikamano.
Tunapamba
kufurahisha wengine.
Tunapamba
kuonesha vipaji vyetu na kukamilisha ndoto zetu.
Tunapamba
ili kujiaminisha wenyewe kuwa tunaweza kufanya jambo na likaonekana.
Tunapamba
ili kuonyesha ladha zetu, tunachopenda na tusichopenda.
Tunapamba
ili kunogesha mazungumzo, watu wanapenda kufanyia mazungumzo yao mahali
panapovutia.
Tunapamba
ili kujipa changamoto.
Tunapamba
ili kuongeza thamani ya nyumba.
Tunapamba
kwa sababu tunatakiwa kufanya hivyo.
Tunapamba
kwasababu tunapenda vitu vizuri.
Tunapamba
kwasababu inatufanya tujisikie furaha.
Tunapamba
kwasababu tunataka watoto wetu wakulie kwenye mazingira mazuri.
Kiukweli
hizi zote ni sababu za kupamba nyumba zetu na huenda nawe masomaji wangu unazo
zako za kuongezea.
Sasa
kuna wale wanaopamba nyumba halafu wanaogopa hata kuitumia wenyewe. Kama
utapamba halafu ushindwe kutumia kuamsha furaha yako, mshikamano na burudani
sasa kuna raha gani? Kuna baadhi ya nyumba ambazo alama pekee za kwenye zulia
ni za mashine iliyosafishia, hakuna mtu anapita hapo! Ni vizuri kufahamu kuwa
nyumba yako uliyopamba inakuwezesha kutengeneza kumbukumbu za maisha.
Sio
lazima usafiri upigie picha kutengeneza kumbukumbu kwenye maeneo mbalimbali ya
dunia ambapo wengi hatumudu, unaweza kutengeneza kumbukumbu hapo nyumbani
kwako. Unakuwa na kumbukumbu kuwa nilishawahi kupaka rahi hii, kwa mfano, au
nilikuwa na sofa za aina hii kipindi fulani, na kadhalika.
Siku
ambayo kitanda chako kikubwa kinawasili na unahamishia kidogo kwa watoto ni
kumbukumbu tosha.
Kwahivyo
kwenye kupamba nyumba yako ili uweze kuifurahia zingatia vitu ambavyo hutakosa
uhuru wa matumizi. Kwa mfano huna haja ya kuwa na rangi ya kitambaa cha sofa au
zulia ambayo unaamini zitakunyima uhuru wa kufurahia nyumba. Kwa mfano rangi
zinazochafuka ndani ya muda mfupi. Unahitaji mapambo ya uhalisia wa maisha yako
zaidi, nyumba ambayo wakaaji wataifurahia. Nyumba ambayo unaweza kualika wageni
ndani na wakajisikia huru. Nyumba ambayo watoto wako wanaweza kualika wenzao
wakacheza na kufurahi wakiwa ndani.
Siku hizi ambapo ni ngumu kupata weza wanne kuwaalika nyumbani kwa wakati mmoja (kweli ni ngumu kwa ajili watu wana majukumu mengi ratiba zao zina mengi, unaweza kutumia mwezi mzima kutafuta watu kwa chakula cha usiku bila kuweza kuwapata kwa pamoja) ni vyema kuwa na tabia ya kusherehekea ndani ya familia zetu wenyewe.
Kwa hivyo usipambe kwa jinsi ambayo utashindwa kuifurahia nyumba, maisha ni mafupi na familia na marafiki ni zawadi.
Sasa nawe msomaji wangu niambie sababi za kwanini unapamba nyumba yako. Kweli ni vizuri kukuza uzuri na unadhifu katika kona yako ya dunia ambapo ndio nyumbani kwako, kwa sababu unaweza.
Siku hizi ambapo ni ngumu kupata weza wanne kuwaalika nyumbani kwa wakati mmoja (kweli ni ngumu kwa ajili watu wana majukumu mengi ratiba zao zina mengi, unaweza kutumia mwezi mzima kutafuta watu kwa chakula cha usiku bila kuweza kuwapata kwa pamoja) ni vyema kuwa na tabia ya kusherehekea ndani ya familia zetu wenyewe.
Kwa hivyo usipambe kwa jinsi ambayo utashindwa kuifurahia nyumba, maisha ni mafupi na familia na marafiki ni zawadi.
Sasa nawe msomaji wangu niambie sababi za kwanini unapamba nyumba yako. Kweli ni vizuri kukuza uzuri na unadhifu katika kona yako ya dunia ambapo ndio nyumbani kwako, kwa sababu unaweza.
No comments:
Post a Comment