Mwimbaji mahiri wa muziki wa
Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee
Yusuph amefunguka na kusema kuwa lazima aache muziki na kufanya kazi zingine
nje ya muziki.
Mzee Yusuph alisema hayo
alipohojiwa na mtangazaji wa Tam Tam za Mwambao ya East Africa Radio, Mwanne
Othman.
Mzee Yusuph alisema kuwa kwa sasa
anataraji kutoa album mbili za mwisho ili aweze kuachana na muzuki kwa swababu
ana mambo mengi ya kufanya hasa siasa na kazi zake na badala yake atakuwa boss
tu kwa wasanii wenzake katika kundi lake hilo ila si uimbaji tena.
"Muda ikifika nitaacha,
lazima niache muziki kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya nje ya muziki, na
kama hivyo nikipita katika nafasi ya ubunge itabidi tu nicahgue moja itabidi
kwenye muziki nisipatikane kwa asilimia mia moja vivyo wapenzi wa muziki wangu
lazima waelewe kuwa naacha muziki kwa sababu ya siasa na kazi zangu zingine
ambazo ni nyingi na zinahitaji uwepo wangu hivyo lazima niache muziki ili
niweze kukamilisha mambo mengine nikiwa nje ya muziki."
Lakini mzee Yusuph aliweza kuweka
wazi suala la yeye kutaka kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Fuweni
Zanzibar na kusema kuwa anataka kulipa fadhila kwa namna ambavyo mashabiki wake
walivyoweza kumpenda na kumjali na kuweza kumfanikishia mambo mengi kupitia
njia ya muziki, hivyo yeye anaamini ubunge ni wito anaona bora awe mbunge ili
jamii iweze kumtuma na kuwawakilisha wananchi katika mambo yao kwa kuwa
wananch9o hao wameweza kumletea mabadiliko katika maisha yake ya kawaida.
Mbali na hilo Mzee Yusuph
ameeleza kuwa yeye kuingia katika siasa si lengo ya kutafuta kutoka kimaisha
bali anaamini anaweza kuwafanya jambo wananchi kwa kujitolea maana lengo lake
ni kuwatumikia wananchi.
"Mimi sina ndugu sina baba
ambaye ni kiongozi bali nimeingia katika siasa ili wananchi waweze kunituma
maana mimi naamini hii kazi ni ya wito tu hivyo wananchi wasiangalie majina ya
viongozi bali waangalie mtu mwenye dhamira njema ya kutaka kufanya jambo kwa
manufaa ya wananchi na kwa kujitolea. Mimi naanzia kwenye ubunge ikiwezekana
huko baadaye mpaka kwenye urais nitafika tu"
No comments:
Post a Comment