WATU watatu wamekufa katika matukio matatu tofauti katika
Wilaya za Tarime na Rorya akiwemo mtu aliyeuawa wakati wanagombania mwanamke.
Waliokufa ni Chacha Mwita (24) aliyechowa kisu kifuani na
mwenzake wakigombea mwanamke wa baa huko Sirari.
Kaimu Kamanda wa Polisi Tarime Rorya ACP Swetbert Njewike
alisema kuwa matukio hayo matatu ya vifo yalitokea Julai mosi mwaka huu katika
Wilaya za Rorya na Tarime.
Akielezea tukio la baa ambalo Mwita aliuawa, alisema siku
hiyo marehemu akiwa baa moja katika mji wa Sirari, Tarime, nyakati za saa moja
jioni kulitokea ugomvi kati ya marehemu na mtu mwingine ambaye hajafahamika
jina lake wakigombania mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Dina.
“Jeshi la Polisi linafanya msako wa watuhumiwa wa mauaji
Chacha Mwita na watuhumiwa waliohusika katika mauaji ya Nguka ili waweze
kufikishwa katika vyombo vya Sheria,” alisema.
Aliwaonya wananchi kutojichukulia sheria mikononi ya kuwauawa
watu wengine badala yake wawafikishe katika vyombo husika vikiwemo vya Dola.
Aliwaomba raia wema kutoa taarifa mara watakapowaona watuhumiwa hao wa mauaji
hayo ii wakamatwe.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment