Askofu Severin Niwemugizi |
BAADHI ya Majimbo ya Kanisa Katoliki nchini, yametoa
ruhusa maalum kwa mapadri yakiwataka kuendesha ibada zao siku
ya Jumamosi ya Oktoba 24 badala ya Jumapili mwaka huu ili kutoa
nafasi kwa waamini wao kushiriki Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na
madiwani kwa uhuru.
Hatua hiyo inatokana na siku
ya Jumapili ambayo waamini wengi wa kanisa hilo huabudu
kuangukia Oktoba 25 ambayo ni siku ya Uchaguzi Mkuu.
Habari za uhakika
ambazo MTANZANIA imezipata mjini Dar es Salaam jana na
kuthibitishwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, zinasema kila askofu wa
jimbo ana mamlaka ya kutoa maelekezo ya aina hiyo kwa waamini wake.
Askofu Niwemugizi alisema
kila askofu katika jimbo lake anawajibika kufanya hivyo, kwani ni
haki ya msingi ya waamini wake kupiga kura.
“Kilitrujia siku ya bwana
inaanza Jumamosi jioni, kwa msingi huo wanaweza pia
kuadhimisha dominika bila tatizo lolote.
“Si utaratibu wa kawaida kwa sababu kama baraza hatujakaa, lakini kila askofu anawajibika ndani ya jimbo lake, hivyo anaweza kutoa fursa hiyo. “Hata mimi katika jimbo langu la Rulenge Ngara, nimetoa kibali hicho kwa makanisa yote… kwa wanaotaka wala siwalazimishi wote,” alisema Katika hatua nyingine, askofu huyo alizungumzia mwenendo wa kampeni za uchaguzi, alisema amesikitishwa na dharau na matusi yanayotolewa na wanasiasa katika
majukwa ya kampeni.
“Kumekuwa na lugha
chafu, hakuna anayeona kama amefanya vibaya kwa mwenzake,…. kwa
mfano unamwita mwenzako oil chafu, maana yake unamdharau
muumba aliyemuumba hata kama ana upungufu.
Alisema tabia hiyo ya
kutoleana lugha chafu ipo siku viongozi wa dini nao wategeukiwa.
MOSHI
Habari kutoka Jimbo Katoliki
la Moshi mkoani Kilimanjaro na Mbulu mkoani Manyara,
zinasema kanisa hilo limetoa ruhusa maalumu kwa waamini wa majimbo
hayo kusali ibada ya Jumapili Oktoba 24, ili kutoa fursa kwa waamini
hao kwenda kupiga kura.
Uamuzi huo unatokana na
waraka wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Mhashamu Isaac
Amani uliosambazwa katika makanisa yote ya majimbo hayo.
Waraka huo wenye
kumbukumbu namba PROT Na. BSH/2657/2015- VIII/B kwenda kwa mapdre,
watawa na waamini walei, uliosainiwa na Askofu Aman unawahimiza
waamini wake kushiriki Uchaguzi Mkuu.
“Wakati kampeni za
Uchaguzi Mkuu zikiendelea, ni muhimu wananchi wafuatilie hotuba za wagombea
ili hatimaye waweze kuchagua viongozi wenye sera na sifa za kuleta
maendeleo ya wananchi.
“Tunaendelea kumwomba
Mungu atujalie amani wakati wa kampeni, siku ya uchaguzi na baada
ya uchaguzi wagombea na wananchi wayapokee matokeo kwa utulivu
na raha ya kudumisha umoja na amani ya kitaifa.
“Kwa kuwa siku ya uchaguzi
ni Dominika, nawaletea tangazo la kuboresha mazingira ya
kupiga kura. Kwa waraka huu natoa kibali maalumu kwa mapadre
majimboni Mbulu, Moshi kufanya ibada ya Dominika ya 30 ya mwaka huu
siku ya Jumamosi Oktoba 24.
“Lengo la kibali hiki ni
kuwapa wapiga kura fursa ya kupata ibada Jumamosi jioni na Jumapili
asubuhi ili wakapige kura mapema. Hata Mapadre wanatakiwa
kushiriki zoezi hili la kitaifa.
Kwa hiyo ratiba za misa zipangiliwe
maparokiani na vigangoni kwa kuzingatia kibali kilichotolewa.
“Natumia fursa hii
kuwahimiza wale wote waliojiandikisha watumie haki na wajibu wa
kupiga kura ili tupate viongozi wazalendo tunaowapenda. Kura yako
ni muhimu katika harakati za kuwasaka viongozi, madiwani,wabunge na
rais.
“Usiachie wengine wakuchagulie viongozi wakati wewe unao wajibu wa kupiga kura. Ukishapiga kura yako rudi nyumbani ukangojee matokeo,”ilisema sehemu ya waraka huo.
“Usiachie wengine wakuchagulie viongozi wakati wewe unao wajibu wa kupiga kura. Ukishapiga kura yako rudi nyumbani ukangojee matokeo,”ilisema sehemu ya waraka huo.
Akizungumza na Mtanzania jana, Mhashamu Askofu Amani ambaye pia ni msimamizi wa kitume
wa Jimbo Katoliki la Mbulu alisema kutoa fursa hiyo ni
kuwataka waamini wake kutumia haki ya kidemokrasia ya kupata
viongozi.
Alisema ratiba za misa zote
za ibada zitapangwa kwa parokia zote na vigango vyote kwa mujibu
wa kibali kilichotolewa na kanisa hilo.
Uamuzi huo wa kanisa unakwenda sambamba na ushauri uliowahi kutolewa
siku za nyuma na Jukwaa na Katiba Tanzania (JUKATA) pamoja na wadau
wengine. Wadau hao waliwahi kupendekeza kuhusu haja ya siku ya
Uchaguzi
Mkuu ibadilishwe ili kutoa fursa kwa waamini ya dini ya Kikristu kutumia vizuri haki yao ya kupiga kura, ili siku ya jumapili waitumie kwa ajili ya ibada tu.
Mkuu ibadilishwe ili kutoa fursa kwa waamini ya dini ya Kikristu kutumia vizuri haki yao ya kupiga kura, ili siku ya jumapili waitumie kwa ajili ya ibada tu.
Utaratibu huo wa siku
maalum ya kupiga kura ulitumiwa na nchi ya Kenya katika uchaguzi mkuu
uliopita, uliomuweka madarakani Rais Uhuru Kenyatta.
No comments:
Post a Comment