Akizungumza kupitia vyombo
vya habari Jumapili ya leo, mwanasiasa mkongwe katika Chama cha Mapinduzi (CCM)
na aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali za chama na serikali ya Chama,
Kingunge Ngombare Mwiru ametangaza rasmi hivi punde kujiengua uanachama ndani
ya chama hicho.
Kingunge amesema ameamua
kufanya hivyo kwa kuamini kuwa CCM haifanyi yale yaliyoasisiwa na kujengewa
misingi bora na waasisi wa Chama.
Aidha amesema hakusudii
kujiunga na chama chochote cha siasa nchini.
Akitathmimi anavyoiona
hali ya sasa kisiasa nchini, amesema kila kundi katika jamii hivi sasa linataka
mabadiliko.
No comments:
Post a Comment