Thursday, November 24, 2016

Faida za kutumia ukoka wa bandia kwenye bustani yako

Kwa siku za karibuni ukoka wa kutengeneza (artificial grass) umeanza kugusa mioyo ya baadhi ya Watanzania, anasema muuzaji Saleh Ahmed wa kampuni ya Aqua DΓ©cor iliyopo Kijitonyama simu 0712 792 909. Katika makala hii napenda wewe msomaji wangu uelimike kuhusu ukoka huu endapo utavutiwa kuwa nao.

Ni vyema ujue kwamba ni
muhimu ukoka wa kutengeneza unaotaka kununua uwe wa kiwango bora na pia upate mtaalam wa usimikaji ambaye anaifahamu vyema kazi hiyo.
Ukoka wa kutengeneza wenye viwango vyote vya ubora utakupa faida nyingi zaidi ya bustani ya asili ambapo faida moja kubwa ni kutokuhitaji kumwagiliwa. Ukiwekwa vizuri ni hakika kwamba bustani yako mpya ya ukoka wa kutengeneza itaongeza thamani ya nyumba yako huku ikiboresha maisha yako kwa kukupa eneo zuri la nje ya nyumba la kuweza kukaaa kila wakati unapohitaji kufanya hivyo.

Ni ukweli kuwa bustani kuweza kuwa ya kijani muda wote mwaka mzima ni gharama kubwa. Ambao wanatumia ukoka huu wanafuraha jinsi maisha yalivyobadilika kuwa mazuri kwani wanashangazwa na matokeo na faida ambazo hata mwanzo hawakuwa wanazijua zote. Fikiria bustani ambayo hakuna kukatia majani tena, hakuna kumwagilia tena, hakuna tope au mabaki ya majani yanayokuchafua miguu na pengine hata kuingia ndani, hakuna kuweka mbolea na wala hakuna kupiga magoti kung’olea magugu. Ukoka huu wa kutengeneza unaweza kukupumbaza kiasi kwamba ukadhani ni ukoka hai. Ni mkombozi kwa walioko kwenye maeneo yenye ukame lakini bado wanatamani kuwa na bustani isiyo na vumbi.

Kutokana na mvuto wake unaweza kutamani kuvua viatu kabla hujakanyaga humo. Ukoka wa kutengeneza ukiwa umesimikwa vizuri, hakuna jinsi unaweza kusema  bustani ni feki kama hujaambiwa au kugusa. Ni zulia la kweli la nje ya nyumba ambalo linaweza kudumu kati ya miaka 15 hadi miaka 25 hivyo kukufanya uwe na bustani ya gharama nafuu sana ukilinganisha na bustani hai.

Ni eneo zuri la watoto kucheza.
Faida zile zile zinazofanya ukoka wa kutengeneza kuwekwa kwenye baadhi ya viwanja vikubwa vya michezo, na vilele vya majengo ya biashara sasa utakuwa unazipata moja kwa moja nyumbani kwako.

Endapo unataka kununua ukoka wa kutengeneza chagua ambao hauachi alama za nyayo au viatu ukiwa umepita juu yake, ni rahisi kujaribu zoezi hili. Wenye ubora unaokubalika huwa umewekwa kizuizi cha mionzi ya jua kwa hivyo usiogope kuwa rangi ya kijani itachuja.

Wageni watakaokutembelea bila shaka wataona wivu kwani huhitaji kumwagilia, ila bado una bustani nzuri kushinda zao zilizokauka au zilizo chepechepe sana kwa ajili ya kumwagiliwa maji mengi hasa wakati wa kiangazi kiasi kwamba hata kukaa inakuwa ngumu.

Wewe  unaonaje kuhusu ukoka wa kutengeneza, ni mkombozi kwa wenye nyumba wapenda bustani  au sivyo?

No comments:

Post a Comment