Basi mwigizaji huyo amefunguka na kuwajia juu wale wote wanaomchafua
na kudai kuwa hakuna kama baba wa mtoto wake Mose Iyobo.
Mwigizaji huyo mahiri alienda mbali
zaidi na kuwapiga mkwara watu wote wanaotumia jina lake kuchafuana kisiasa na
kuongeza kuwa kama wamejipanga hayo basi ni bora wakafanya mambo yao bila
kumwingiza yeye.
“Naona kama kuna kitu nyuma ya
pazia, kwa kuwa nimesikia hadi bungeni imezungumziwa. Ni kitu cha ajabu na aibu
mtu amechaguliwa na wananchi kujadili masuala yao, anajadili mambo ya Aunt!
Akizungumza na Mwananchi, huku
akionyesha kukerwa na uzushi huo alisema kuwa, watu wanatumia kukutana kwake na
kiongozi huyo nje ya nchi kama fimbo ya kumchapia katika wakati huu wa mambo ya
siasa ambao kila mtu anajisafisha kupitia jina la mwingine.
Aunt Ezekiel alieleza kuwa akiwa
Marekani kwenye shughuli zake binafsi, alikwa kwenye tafrija na ndipo
alipokutana na waziri huyo kama ambavyo angeweza kukutana na mtu mwingine
yeyote, lakini anachoshangaa kilichotokea kuanzia hapo hadi mada ikabadilishwa
na kuelezwa kuwa walikuwa na uhusiano.
“Ninachofahamu siyo kila unayekutana
naye nje ya nchi ni mpenzi wako au unatembea naye. Hili suala linanikera sana
kwa sababu linatengeneza kitu ambacho hakipo na wala hakifikiriwi kutokea,”
alisisitiza Aunt Ezekiel, huku uso ukionyesha wazi kuchukizwa na kitendo hicho.
“Wazungu wana msemo wao usemao,
‘kama hujafanya utafiti huna haki ya kusema’, kwa jinsi alivyojiamini bungeni
ina maana alikuwa na uhakika? Mimi namshauri aje na ushahidi ... Bila kufahamu
kuna matatizo gani anayasababisha kwa wahusika.”
Kwa mujibu wa Aunt, baba halali wa
huyu mtoto ni Mose Iyobo na kwamba anampenda kwa dhati na kumjali na kwamba
hajawahi kupenda kama anavyompenda mwanaume huyo hivyo anahitaji kuheshimiwa
mambo yake.
“Nina uhusiano wangu pia Waziri ana
mke na familia yake suala hili linamwathiri kama ambavyo linaniathiri mimi,
sitaki kujadiliwa kwa mambo ya kinafiki. Mimi ni msanii lakini hiyo siyo
bendera ya kuwa kila ninayekutana naye tuna uhusiano, huko ni kunivunjiana
heshima na kunidhalilisha,” alisema Aunt Ezekiel.
No comments:
Post a Comment