Jinsi
ya kupata sinki la jikoni litakalokufaa
Jiko linaweza kuwa moyo wa nyumba lakini sinki ndilo
linabeba dhamana kubwa ya kazi ya jikoni. Hii ni kwa sababu ndani ya sinki ni mahali
pekee panapotumika kwa shughuli ya
mwanzo na ya mwisho kwa chochote kinachofanyika jikoni. Ni mahali panapotumika
zaidi wakati wa kuanza kupika na kumalizia kusafisha baada ya kupika. Sinki ni
kiungo muhimu kwa jiko lolote. Linakuwezesha kufanya shughuli kadhaa kama vile
kuosha vyombo, kujaza sufuria maji na kuosha mikono yako. Pia ni muhimu kwa
muonekano wa jiko na linafanya chumba cha jiko kionekane maridadi.
Ingawa sinki imara linaweza kudumu hadi miaka 15
lakini huwa linachakaa, anasema muuzaji Awadh Hafidh. Rangi yake kwa mfano yale
masinki ya rangi ya bati laini lisiloruhusu kutu inaanza kufifia, na kuvujisha
maji kwa kuudhi kunaanza kutokea baadhi ya maeneo. Na kama unafikria
marekebisho ya jiko ni busara kubadilisha sinki na bomba zake.
Masinki ya jikoni sokoni yapo ya maumbo mbalimbali
ila aina kuu mbili za kawaida sana ni masinki yenye karai moja na yale yenye
karai mbili. Sinki la karai moja linakupa karai pana zaidi. Hili linafaa zaidi
kama utakuwa na vyombo vingi vya kuosha kwa wakati mmoja na masufuria
yanayotumika kwenye jiko husika ni makubwa. Sinki lenye karai mbili za pembe
nne zilizolingana ukubwa linafaa zaidi kwa kuoshea na kusuuzia vyombo hasa kama
unaosha kwa mikono. Kwa hivyo unatakiwa kujua ukubwa wa chumba cha jiko lako na
jinsi utakavyolitumia sinki lenyewe. Umbo na ukubwa wa sinki ni muhimu, na wakati unapoangalia
ukubwa wa sinki tupia jicho kwenye kina chake pia. Kutegemea na matumizi ya
jiko, sinki lenye kina kirefu ni bora zaidi kwa kuoshea vyombo na masufuria.
Watengenezaji
wanazalisha sinki za jikoni zilizotengenezwa kwa vifaa na mitindo mbali mbali
kutoka bati la kung’aa lisiloshika kutu hadi vifaa kadhaa vya kisasa zaidi,
anasema Awadh. Pia sinki la jikoni ni mojawapo kati ya kifaa cha bei rahisi
kinachojumuika kwenye ujenzi wa jiko. Ingawa kuna masinki ya jikoni za kifahari
ya bei kubwa, kuna utajiri wa masinki mengi ya jikoni ya bei nafuu.
Cha muhimu msomaji ni kujipatia sinki imara ambalo halitatikisa bajeti yako. Kwa kuwa sinki hili linauzwa pekee kama lilivyo bila kujumuisha bomba, basi katika hatua itakayofuata utaweza kujichagulia bomba la sinki la jikoni la rangi na staili unayopenda.
Cha muhimu msomaji ni kujipatia sinki imara ambalo halitatikisa bajeti yako. Kwa kuwa sinki hili linauzwa pekee kama lilivyo bila kujumuisha bomba, basi katika hatua itakayofuata utaweza kujichagulia bomba la sinki la jikoni la rangi na staili unayopenda.
Mara unapochagua umbo na ukubwa wa
sinki unalotaka kuendana na mahitaji yako, uamuzi wako unaofuata ni kuamua juu
ya vifaa mbalimbali vilivyotumika kutengenezea sinki hilo iwe ni bati lisiloshika
kutu au enameli. Aina ya kifaa kilichotengenezea sinki utakachochagua kati ya
hizi mbili itategemea zaidi na ladha binafsi na mfuko wako.
Masinki ya bati lisiloshika kutu
ndio ya kawaida zaidi kwa ajili ya jikoni. Ni gharama nafuu, yanadumu na rangi
yake ya silva inaendana sana na vifaa na vyombo vingine vya jikoni. Wakati
unanunua sinki la aina hii chagua lile la bati nene kwani litadumu zaidi. Sinki
la bati nene limetulia kwa hivyo kupunguza hata kelele za vyombo na kufanya
mchakato wa kuandaa chakula kuwa wa kimya kimya.
Usisahau kuzingatia vitu vya ziada ambavyo
huenda ukahitaji viwepo kwenye sinki lako la jikoni kwa mfano pampu ya sabuni. Baadhi
ya masinki yatakuwa na alama hizo wakati mengine hayana.
Nakutakia uchaguzi mzuri wa sinki
lako la jikoni.
Makala
hii imeandaliwa na Vivi O. Machange.
Vivi ni mjasiriamali upande wa usafi wa nguo, mazulia na magari; pia ana
mapenzi makubwa ya mitindo na mapambo ya nyumbani. Kwa maoni au maswali tuma
kwenda 0755 200023 au viviobed@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment