nimetoka kumchukua mtu wangu mdogo shule na huko nimekutana na jambo lililonigusa mno. mdau jambo hilo ni kuwa baada ya kugeuza shingo yangu nimemwona mwanafunzi mvulana mdogo wa miaka kati ya 3-4 anaingia kwenye gari na magango mikono yote miwili. Eeh Mungu, nikajisemea hebu subiri dakika moja. nikaamua kumwuliza mwalimu kulikoni mwanafunzi huyo mdogo hivyo kutembelea magango.
mwalimu akaniambia kuwa mzazi wa huyo mtoto anasema kuwa mtoto wake alizaliwa mzima na akatembea vizuri kama watoto wengine ila baadaye kuna sindano aliyochoma ndiyo iliyosababisha miguu yake kukosa nguvu ndio maana anatembelea magango. kusema kweli nilivyomwona mtoto mwenyewe keshazoea miguu yake hiyo ya ziada kwa hivyo anacheka na yuko anafurahia kama watoto wengine tu.
sasa mdau wangu kutokana na hili hatuwezi kumhukumu yeyote kuwa ndio mwenye kosa lililomsababishia huyu mtoto awe melemavu maisha yake yote ila nilichojifunza ni kuwa ni vyema kuhakikisha kuwa mtoto wako mdogo anapoumwa ni vyema kumpeleka kwa daktari wa watoto (pediatrician) na hata ukiweza nenda extra mile kwa kupata referal ya daktari unayetaka kumpelekea mtoto wako kabla ya kumpeleka. ni hayo tu mdau ila moyo wangu kweli umesoneneka. tusisahau kumshukuru Mungu kila siku kwani kiburi cha uzima kinawafanya wengi wamsahau.
Uwe na valentine njema!
No comments:
Post a Comment