MWENYEKITI wa Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA), Profesa Penina Mlama ametoa mwito kwa wasanii kuchangamkia
kuchangia ujenzi wa nyumba unaoratibiwa na Mtandao wa Wasanii Tanzania
(SHIWATA) ili kujiandalia makazi.
|
|
Akizungumza baada ya
kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za wasanii katika kijiji cha Mwanzega,
Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Profesa Mlama alisema makazi ni sehemu ya
maisha ya binadamu hivyo wasidharau mradi huo ni faida kubwa kwao.
|
|
Alisema nyumba ambazo
ameziona ni nzuri, imara na zinauzwa bei ya chini ambayo huwezi kuzipata
sehemu nyingine yoyote nchini na kuongeza kuwa kujenga kwa lengo la kuishi
pamoja, kunatoa fursa ya wasanii kubuni njia nyingine ya kuanzisha miradi
mbalimbali.
|
|
Profesa Mlama alitaka
Shiwata isikate tamaa, bali iendelee kuwashawishi wasanii wajiunge na
kuchangia ujenzi wa nyumba ili baadaye wasitafute visingizio kuwa hawakupewa
fursa hiyo.
|
|
Naye Katibu Mtendaji wa
Basata, Godfrey Mngereza alisifu Shiwata kubuni njia ya kuwasaidia wasanii
kupata makazi na kuahidi kuwa baraza hilo litatoa ushirikiano na kutoa
ushauri kila unapohitajika.
|
|
Mwenyekiti wa Shiwata,
Cassim Taalib alisema mpango wa ujenzi wa nyumba za wasanii utaendelea kote
nchini na kuwataka wasanii waungane kufanya kazi zao kwa pamoja.
|
|
Alisema mpaka sasa nyumba
38 zimekabidhiwa kwa wasanii waliochangia ujenzi katika kijiji cha Mwanzega
Mkuranga na nyingine 21 zinatarajiwa kukabidhiwa mwezi ujao.
|
|
Shiwata mbali ya
kusimamia ujenzi wa nyumba hizo, inasimamia matamasha ya wasanii wachanga,
kuendesha makongamano ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya na kutoa elimu
na maadili kwa wasanii.
Chanzo cha habari hii ni kutoka magazetini
|
Sunday, February 9, 2014
News Zihusuzo Makazi/Nyumba: Wasanii watakiwa kuchangamkia nyumba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment