Leo katika mfululizo wa stori zangu za kukuwezesha kuvuka kutoka daraja ulilopo kwenda la juu nimeongea na entrepreneur Fred Kirya ambaye alikuwa mwalimu hapo kabla lakini sasa ana media company. Nikamuuliza amevukaje? Akaniambia alivyokuwa mwalimu alijishughulisha pia na kuandaa program za vijana walioathirika na mambo mbalimbali, watukutu na hata wanajeshi waliotoka vitani halafu vichwa vikavyatuka kiana. Kutoka huko baadhi wa vijana walioweza kuachana na hali hizo wakawa wanaenda kuongea kwenye vituo mbalimbali vya redio. Hapo ndipo Fred alipojenga interest na media na akafungua media company yake ambayo anarekodi nyimbo za kwaya, singles za wasanii, program za watoto na vipindi vya vijana kwenye vituo vya redio. Fred anasema kwa kufanya kazi kwenye kampuni yake mwenyewe ana furaha ya kufanya anachokipenda, kuwa makini zaidi kwa mfano matumizi na utunzaji wa vifaa vya kazi na kubwa zaidi financially amekuwa na wise spending...... Kaa standby kusoma stori nyingine itakayofuata...
No comments:
Post a Comment