Saturday, November 28, 2015

PICHA: PATA IDEAS ZA JINSI YA KUPAMBA SEBULE KWA VIKOI

Hapa vikoi vimetupiwa kwenye sofa na coffee table, ila hapo kwenye meza kakikunja na kukitupia kwa mkato. Pia angalia jinsi rangi  nyeupe ya vikoi ilivyochangamsha hilo sofa jeusi, kwahivyo moja kwa moja utaona kuwa unaweza kutumia vikoi kubadili rangi sebuleni bila gharama kubwa. Halafu ukiangalia zaidi pattern za vikoi zinaendana na za carpet.

Kikoi hapa kwenye meza kimetupiwa kizima bila kukunjwa lakini nusu ya meza  na kimebaki kipande kinaning'inia

Hapa kikoi kimekunjwa na kutupiwa eneo la meza la kati tu

Licha ya vile kule kwenye sofa, hiki kikoi kizima bila kukunjwa kimetupiwa kwenye meza yote kikafunika kila mahali....kazi kwako mdau ideas hizoo cheza nazo upambe unapoishi..na ukimaliza naomba nirushie picha.

Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023




Friday, November 27, 2015

HOME DECOR YA LEO.....JIKO

Nimeguswa na hili jiko jinsi ambavyo ni dogo, yani liko kama ki corridor tu lakini sehemu zote za msingi kwa maana ya counter, sink na makabati yapo. Haijalishi nyumba yako ni kubwa kiasi gani kinachojalisha ni mpangilio na usafi.

Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023

Wednesday, November 25, 2015

UPI NI WAKATI SAHIHI WA KUWEKA NA KUONDOA MAPAMBO YA KRISMASI?


Chini ya mwezi mmoja ujao tutakuwa na sikukuu ya Krismasi na baadhi ya sehemu hasa kwenye maduka makubwa tayari wameshaweka mapambo ya krismasi ambayo ni pamoja na mti, taa za kumeremeta na kadi.

Lakini je, ni wakati gani unaweka mapambo yako ya Krismasi nyumbani? Na pia je, ni wakati gani unayaondoa? Je, unayaweka wiki kadhaa kabla au unasubiri siku chache tu kabla ya sikukuu?  Au labda hupambi kabisa,  huenda yanawaletea watoto ugomvi na wanakimbilia kuyanyofoanyofoa!

Tuesday, November 24, 2015

MAMBO 12 YA KUFANYIA NGUO CHAFU KABLA HUJAANZA RASMI KUZIFUA


 Umechoka na nguo zako kusinyaa, kupauka au kuchuja? Kuna suluhisho moja kuu: Acha kuziweka kwenye maji huku umefumba macho! Yafuatayo ni mambo 12 ya kufanya kusaidia nguo zako kudumu ziwe ni mpya au za zamani. Mambo haya unapaswa kuyafanya kwenye nguo unazotaka kufua kabla ya kuanza rasmi zoezi hilo, na haijalishi kama utazifua kwa mkono au kwa mashine.

Friday, November 20, 2015

RANGI 5 ZA MARBLE KWA AJILI YA KAUNTA ZA JIKO ZINAZOTAMBA KWA SASA


According to wauzaji wa marble za kaunta za majiko rangi hizi hapa chini ndio ziko kwenye chati.
Hii inafanana na ubwabwa...ukiwa unasafisha inabidi utoe jicho la nguvu

Marble zinaweza kupata madoa. Hii ya mchuzi mchuzi itawafaa wasiosafisha papo kwa papo

Kwa zile familia zenye mishe nyingi hii itawafaa kwa ajili hata mtu bahati mbaya akikatia kitu kwa kisu alama ni ngumu kuonekana.

Marble hii inapendelewa na wale wanaopenda jiko jeupe. Wengine huenda na weupe huo hadi kwenye makabati.

Kaunta za marble ni rahisi kutunza na kusafisha na pia ni maridadi ulinganisha na za malighafi nyingine.

Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023


HOME DECOR HAPA NA PALE: TILES ZA BAFUNI, MTO, JIKO

Angalia hizi tiles za bafuni za style ya mapovu (bubbles). Unapoamua kujenga au kufanya marekebisho ya nyumba yako fanya utafiti wa kutosha kwa ajili vitu vizuri ni vingi na vinakuja kila iitwapo leo.

Hii print kwenye huu mto inasemea msimu wa sikukuu. Hivi wajasiriamali wa hapa wanaweza kufanya mito yenye prints kama hizi kweli? Nadhani wangeuza hata kwenye showrooms kubwa na supermarkets.

Kama ndio unajenga au unajiandaa kujenga hebu fikira kuwa na jiko kama hili. Najua bongo yatakuwa machache sana. Jiko lina sehemu ya kulia na taa za kutosha kabisa.

Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023


Thursday, November 19, 2015

PICHA: DECOR YA LEO....CHANDELIER NA MIGUU YA MEZA

Nimeidondokea hiyo chandelier (taa ya ceiling) na base (miguu) ya hiyo meza. Wewe je, niambie ni nini kimekugusa hapa kwenye hii dining room?

Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023



-----VITU VIZURI------BAFU LA JACUZZI

Jacuzzi ni bafu kubwa lenye muundo wa mabomba kwa chini yake kwa ajili ya kuupa mwili masaji (Massage).Ni zaidi ya bafu la starehe kuwa nalo nyumbani kwa kuwa lina faida nyingi kiafya. Wataalam wa afya wanasema kuwa kukaa ndani ya bafu la Jacuzzi kuna faida za kimwili na kiakili.
Maji ya moto na presha kwenye Jacuzzi yanasaidia kuboresha msukumo wa damu na hewa mwilini hasa kwa wazee na hatimaye wanapata usingizi mnono wa usiku.
 Jacuzzi linaweza kuwa njia sahihi ya kuponyesha misuli na viungo (joints) vinavyouma. Maji kwenye mabomba ya Jacuzzi yanaruhusu presha kubwa ambapo unaweza kuyaelekeza kwenye eneo unalotaka kufanyia massage aidha kwa kusogea ili kupata ule msukumo mkubwa kabisa wa maji. Jacuzzi pia linasaidia kuondoa maumivu ya mwili yatokanayo na michezo.
Kwa wale wanaoteseka na ugonjwa wa rheumatism wanapata ahueni kwenye presha ya maji ya Jacuzzi baada ya kukaa ndani yake kwa dakika chache.

Kutumia bafu la Jacuzzi kunakuondolea msongo wa mawazo. Kama unataka kuburudisha mwili kwa muda tumia bafu la jacuzzi.

Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023

Wednesday, November 18, 2015

PICHA...VITU VIZURI: SWIMMING POOL

Wanasemaga living heaven on earth, eti...




Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023


HOME DECOR HAPA NA PALE: WINE RACK, PILLOW NA DINNER SET

Huu ni ubunifu ambao susu ya mvinyo imetengenezewa moja kwa moja kwenye meza yake. Ukiwa unasevia watu ni kiasi cha kutoa chupa na kuiweka juu ya meza papo kwa hapo.

Hapa nimeguswa na hiyo picha ya antellope kwenye huo mto. Rangi na uwepo wake umeongeza nakshi ya mto.

Hii arrangement ya dinner set kwenye hizi open shelves bila shaka umeipenda.


Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023

PICHA: BOMOABOMOA YA NYUMBA ENEO LA MWENGE DAR LEO


SHOWER CUBICLES/MABAFU YA BOMBA LA MVUA YALIYO KWENYE CHATI BONGO

Ha hahaaa...kuoga ni starehe eti, na kutokana na hilo nimeona niandike kidogo kuhusu hivi vijumba vya kuogea vilivyo ndani ya bafu
Haya mabafu yana mlango unaingia pale unaoga na maji yote yanaishia mulemule hakuna kutapakaa kila mahali bafuni. Na hii inasaidia hata kwenye usafi wa bafuni una deal zaidi na huo ukuta wa cubicle na eneo lake badala ya kuweka nguvu kubwa kila mahali.


Hizi cubical zina function nyingi. zipo zinazo act pia kama sauna. kwahivyo ni  bajeti yako tu

Za square nyingi milango inakuwa ya ku slide

Models ni nyingi na functions ni tofauti. Lazima kabla hujanunua utafiti ni nini hasa unataka

Kwako wewe unayependa faragha zaidi cubicle yenye kioo cha hivi itakufaa zaidi. Rahisi kutunza na kusafisha.

Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe kwenye 0755200023

Tuesday, November 17, 2015

PICHA: SEBULE YENYE MITO SAKAFUNI NA UPANDE MWINGINE MAKOCHI

Nimekutana na hii picha ya sebule ya mbelezzzz nikaipenga ghafla. Upande mmoja ina mito ya sakafuni kwa wale wapenda kukaa sebule isiyo na makochi na upande wa pili ina makochi kwa wale wa upande huo. Je, ungekaribishwa kwenye sebule hii ungechagua kukaa upande upi?


Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani na unataka Watanzania waijue? Nijulishe kwenye 0755200023

PICHA: IKIWA UNAPENDA VITU VIZURI HATA SHELFU LA VITABU UTALIPAMBA



Je wewe unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba na bustani ambayo unadhani ni muhimu Watanzania waijue? Nijulishe kwenye 0755200023

Monday, November 16, 2015

JINSI YA KUTANDIKA MAZULIA YA NYUMBANI

Mazulia ya nyumbani naweza kuyaweka kwenye makundi manne kutokana na ukubwa wake. Yapo yale ya wall to wall, yapo makubwa ambayo sio ya wall to wall, yapo madogo ya kutupia kwa mfano kwenye corridor ama pembeni kwa kitanda na yapo madogo ya kukanyagia mlangoni, bafuni na kadhalika. Kwenye utandikaji wa leo nitazungumzia kundi la yale makubwa lakini sio ya wall to wall.
Unapotandika carpet hakikisha fenicha zinakaa juu yake. Njia ya kwanza hapo juu ndio sahihi, Ya pili ni hapana.

Zingatia ukubwa wa carpet na ukapotaka kulitandika carpet lako kwa mfano kama ni dining hakikisha meza na viti vitatoshea juu ya carpet husika. Kwahiyo kuwa makini usijenunua ambalo ni dogo sana.

 Pia kama chumba tayari kina carpet la wall to wall basi lile la juu yake lisiwe
kubwa kiasi cha kufunika hilo cha chini.
Chagua carpet la rangi partten na maua kuendana na mapambo mengine ya unapotaka kuliweka.

BOMOA BOMOA NYUMBA ZA WANANCHI KURASNI LEO

Wananchi waishio kurasini shimo la udongo jijini Dar es Salaam walalamikia kubomolewa nyumba zao Mapema Leo na kuitaka serikali kuingilia kati suala hilo kwakuwa wanaona ni kama uonevu wanao fanyiwa.

Sunday, November 15, 2015

PICHA HIZI NDIO ZIMEPATA LIKES NYINGI INSTAGRAM WIKI HII

Nina kawaida ya kurudi nyuma kila wiki na kuangalia ni picha zipi nilizoweka instagram zimepata likes nyingi.

Hizi 2 ndio zimeibuka kidedea:
Hii ilikua na maelezo haya: Nilichopenda kwenye hii bedroom ni hii taa ya mezani na hiyo wallpaper. Wewe umependa nini? Kuna aliyecomment amependa kitanda ili alale..ha haaa

Na hii ilikuwa na maelezo haya: Chumba cha mtoto kinatakiwa kuwa na msisitizo wa rangi, udadisi na burudani. Hongera kwa picha hizi..

Nifuate instagram: vivimachangeblog