MWANA Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amekabidhiwa
hundi ya zaidi ya milioni 14 kwa ajili ya kufidia ujenzi wa upande wa nyumba
yake uliodondoka.
Wakati akikabidhiwa mfano wa hundi hiyo na Kampuni ya
Bima ya UAP kwa ushirikiano na Benki ya CRDB, Diamond alisema ukuta wa nyumba
yake ulianguka wakati akiwa anamuuguza mama yake aliyekuwa katika hali mbaya.
“Ilikuwa ghafla ukuta wa nyumba yangu ya Tegeta ukaanguka
wakati huo nilikuwa natakiwa kulipia fedha kwa ajili ya kurekodi wimbo wangu
mpya.
“Hivyo nisingekuwa nimejiunga na bima sijui sasa
ningekuwa kwenye hali gani? Ni kipindi kigumu sana kwangu,’’ alieleza Diamond
huku akiwataka Watanzania wajiwekee bima kwa kuwa ina msaada mkubwa unapopatwa
na majanga mbalimbali ya vitu ulivyokatia bima hiyo.
Naye, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa UAP, Raymond
Komanga, aliwasisitizia Watanzania waondoe fikra za kwamba bima inayokatwa ni
ya gari pekee bali wakate bima za aina mbalimbali.
CHANZO: MTANZANIA
No comments:
Post a Comment