Thursday, May 12, 2016

Uzoefu wangu katika ziwa Jipe

Kutembelea sehemu mbalimbali ambazo sijawahi kwenda ni kitu nakipenda sana, kwahivyo katika sikukuu za mwisho wa mwaka nilifanikiwa kutembelea ziwa Jipe ambalo liko Usangi wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Naamini utafurahia na kuhamashika pengine na
wewe ukapenda kupatembelea siku moja. Twende pamoja kwenye picha:
Hizi ni nyumba za wavuvi wa ziwa Jipe. Nilichogundua ni kwamba
nyumba za wavuvi dunia ya tatu ni zilezile, mazingira yanaelekea kufanana sana. Nilipokuwa Nungwi Unguja zilikuwa kama hivihivi.

Ziwa Jipe limevamiwa sana na magugu maji. Ukiwa kwa mbali unaweza usilione. Kinachofanyika ni kwamba kuna mitumbwi ya kupeleka watu wanaotaka kuona ziwa vizuri kule kati. Na hiki ni kinjia cha kwenda huko.

Abiria nikiwa ndani ya mtumbwi. "Dereva" huyoo kwa nyuma.

Hiki kinjia nacho kina foleni eti...ha ha haaa

Ziwe jipe hili hapa, huku kati kuna vinamaeneo kama kisiwa vile vya magugu maji ambapo inawezekana kupaki mtumbwi na kushuka kupiga picha. 

Hapa nimeshuka nikasimama kwenye tukisiwa twa magugu. Ziwa lilee kwa upande wa Tz hakuna lodge/mahotel etc ila kwa upande wa Kenya kuna majumba na tulitaka kwenda hadi huko lakini upepo ukawa mkali nikaogopa. Na pia ziwa lina viboko ambavyo ndivyo viliniogopesha zaidi visije kubinua mtumbwi. Ukiwa katikati ya ziwa unayaona kabisa majengo/lodge za Kenya

Mwisho kukawa na samaki walioingia kwenye mtumbwi. Hapa niliposimama ni tope lililokauka kwa juu tu kwahivyo unasimama kwa umakini. Maji ya ziwa yanafika hadi huku.

Je ungependa nipromoti biashara yako iwe ni hotel, restaurant, apartments, bidhaa za majumbani au yoyote ile halali kwa mfumo wa makala kama hii? Kama ndiyo nijulishe kupitia 0755 200023. 




No comments:

Post a Comment