Friday, May 20, 2016

HAPA NA PALE NYUMBANI: FREMU ZA UKUTANI, KUSAFISHA FRIJI, MAUA YA KUTUNDIKA

Unaweza kufremu nukuu unazozipenda na kupendezesha ukuta wako kama hivi. Tena hii itakuwa ni gharama nafuu kwani hutakuwa na haja ya kununua michoro, ni wewe tu kuprint na kununulia fremu ambapo ni rahisi zaidi.

Angalau mara moja kwa mwezi toa shelfu na droo za friji lako uzisafishe kwa maji ya uvuguvugu sponji na sabuni. Zisuuze acha zikauke na zirudishie taratibu bila kulazimisha usije ukavunja.

Picha hii inakupa wazo la unavyoweza kutengeneza hanger za kutundikia maua ya angani nje ya nyumba yako.

Kwa dondoo zaidi endelea kutembelea blog yangu. Pia kama unayo ungependa kushea nijulishe 0755 200023. Kuna aliyeniambia anaosha sufuria kwa vim kitu ambacho sikuwahi kujua, ukishea ujuzi unajisikia vizuri.

No comments:

Post a Comment