-
paulmakondaNdg zangu Watanzania. Leo tumeanza jambo Jipya litakalosaidia na kutatua kwa kiwango kikubwa migogoro ya Aridhi. Nimeamua kutumia Mshahara wangu zaidi ya 75% Kuwalipa Wanasheria 5 watakaotoa Elimu ya SHERIA kwakila MWANAKINONDONI ili asizurumiwe tena na kupoteza kiwanja chake kwa sababu hana pesa ya kulipa mawakili au uelewa wa sheria. Kwani nimebaini zaidi ya 80% ya wananchi wanaofungua kesi wanashindwa.Huduma hiyo itatolewa bure kuanzia 15/06/2015 ofcn kwangu.
Pili kuanzia mwezi ujao nitahamia kwenye ofc za kila kata na kuhakiki maeneo ya Wazi na kupitia nyalaka za kila Mtu . Lengo nikujiepusha na migogoro endelevu na kurejesha maeneo ya wazi kwa matumizi ya umma. E Mwenyezi Mungu naomba unisaidie.
No comments:
Post a Comment