Mpangilio
ndani ya nyumba unagusa vitu na maeneo mengi. Unapokuwa na mifumo ambayo
umejiwekea bila shaka itakusaidia kuwa na nyumba nadhifu, safi yenye mpangilio
na hivyo kurahisisha maisha. Katika makala hii tunaangalia vitu na maeneo mbalimbali
nyumbani yanayohitaji kuwa na mpangilio na jinsi ya kuwa na mfumo wa
kukuwezesha kufanikisha azma hiyo.
Karatasi
Mbali
na karatasi za bili zinazoingia nyumbani ambazo kwa kawaida ni chache, sijui
kama kuna nyumba inayoingia karatasi nyingi kama nyumba yenye watoto wa
shule.
Mara unapogundua ni kiasi gani cha karatasi kinaingia nyumbani kila siku ni
vyema kuwa na mfumo wa kuziweka kwenye mpangilio badala ya kusambaa kila kona.
Kinachotakiwa ni kuweka mfumo wa kutunza karatasi hizo kwa kutumia mafaili.
Kila mwanafamilia anayeingiza karatasi nyingi nymbani ni vyema awe na faili
lake la boksi na liwe na jina. Kila karatasi inayomhusu inapoingia ihifadhiwe
kwenye faili hilo. Zile karatasi za ujumla kama bili na barua nyingine za
kawaida kama za toka kwa wajumbe na za namna hiyo hifadhi kwenye faili la peke
yake.
Jikoni
Sasa,
kama wanavyosema jiko ni moyo wa nyumba, na pia ni mahali pa mwanzo ambapo kweli
panaweza kuvurugika mno kama hapana mfumo mzuri wa kuweka mpangilio! Kwenye
nyumba nyingi pia jikoni ni njia ya kuingilia vyumba vya ndani na hata kuna
wakati wageni wanapita kwenda sebuleni.Uwepo wa vifaa vingi, vyombo na hata
dawa na sabuni mbalimbali za kusafishia, makabati na madroo yanaweza kujaa mara
moja.
Njia
ya kwanza kabisa ya kukuwezesha kuweka mfumo wa mpangilio ni kuondoa kwanza
vitu usivyohitaji na tumia kitu chenye manufaa zaidi ya moja. Kwa mfano kama
una kipasha chakula (microwave) kinachoweza kuchoma pia, basi huhitaji jiko
lenye tanuri (oven). Baada ya hapo jaza kabati na droo kwa vitu unavyohitaji
huku ukipanga vile unavyotimia mara kwa mara maeneo ya karibu na vile
unayotumia mara chache maeneo ya juu.
Tumia
kabati la chini ya sinki kwa kuhifadhia sabuni na dawa za kusafishia na
karatasi za chooni za akiba endapo kule hakuna eneo la kuhifadhia.
Chakula
Wakati
tukiongelea jiko, chakula pia inapaswa kiwe kwenye mpangilio. Hifadhi vyakula
vikavu kwenye stoo ya jikoni ambayo kama ina mashelfu ni vizuri zaidi. Huko
unaweza kutumia mchanganyiko wa mifumo ya vikasha, vikapu na vikontena vyenye
majina.
Kwenye
jokofu ni eneo la pili la kuweka mpangilio wa vyakula baada ya lile la stoo.
Pangilia kwa kutumia nafasi vizuri huku ukihusisha vikontena ulivyochagua kwa
makini na kuweka vyakula sahihi kwenye maeneo sahihi yaliyoainiswa tayari ndani
ya jokofu.
Nguo
Nguo
ni kitu kingine kinachoweza kuchukua kila eneo chumbani iwe ni kwenye kiti,
kitandani, kabatini au kwenye droo. Baada ya kubakiwa na nguo unazohitaji
ainisha zile za kukunja (kunja kwa njia ya wima) na za kutundika. Mpangilio
wote huo uendane na aina ya nguo. Kwa mfano eneo la mashati, la magauni,
suruali na kadhalika.
Vifaa na nguo za
kazi za tope
Tunaishi
maeneo mbalimbali ya nchi mijini na vijijini na vilevile majira ya baridi na ya
joto. Ni vyema kuwa na eneo la kuhifadhia nguo, kofia na viatu vinavyotumika
kwenye shughuli na nyakati hizo.
Midoli na
michezo
Kama
una watoto wadogo, midoli inaweza kuwa ni moja ya vitu vinavyokupa changamoto
kubwa ya kuweka kwenye mpangilio. Michezo na midoli inaweza kusambaa kila mahali
hata ikafikia hatua ya kuvunja watu miguu (fikiria unaingiza mguu kwa bahati
mbali kwenye gari la toi lenye chuma). Cha kufanya ni kuweka mfumo wa
kuhifadhia kama vile vitenga vikubwa kwa vidogo kwenye vyumba vyote vya watoto
pamoja na maeneo yao ya kuchezea. Kama unaamua kwenda mbele zaidi unaweza
kuwajengea shelfu za wazi ukutani kuwa wakimaliza kucheza wahifadhi michezo yao
hapo.
Sasa
basi, baada ya kutaja maeneo, vitu na mifumo yake ya kuweka mpangilio ni vyema
tufahamu kuwa hakuna mfumo ambao ni sahihi zaidi kwa kila familia au nyumba ila
kama lengo lako ni kuwa na mpangilio ndani ya nyumba, natumai orodha hii
inaweza kukusaidia pa kuanzia kwa kujua kuwa ni maeneo yapi ya kipaumbele ili
kurahisisha maisha hapo nyumbani.
Je
kuna maeneo mengine ambayo ungependa kuongezea kwenye orodha hii? Ningependa
kuyafahamu.
Simu 0755200023
No comments:
Post a Comment