Msemo
kuwa nyumbani ndipo moyo ulipo una ukweli usiopingika. Nyumbani ni mkusanyiko
wa maisha, kumbukumbu na upendo. Kama unatafuta njia za kufanya nyumba yako iwe
nyumbani, kuna vitu virahisi na
vidogodogo unavyoweza kufanya. Na hii
haihusiani na kununua vitu vingi vya gharama kubwa. Fuatilia njia hizi ili
uanze leo:
Pamba
kwa picha
Wanasema
picha inaongea maneno elfu moja. Kuongeza kumbukumbu ya picha kwenye mashelfu,
juu ya meza na kuta za nyumba yako kutaifanya iwe nyumbani. Hii inaipa nyumba
muonekano na hisia kuwa mtu fulani anaishi hapo, badala ya kuonekana kama
nyumba tu. Pia ni njia nzuri za kuondoa hizo picha kutoka kwenye simu yako au
kamera ili kuzipa lengo halisi.
Weka
eneo la kukaa
Nyumba
inageuka nyumbani pale kunapokuwa na eneo na viti vizuri vya kukaa kwa wenyeji
na wageni. Kuwa na eneo la kutosha kwa ajili ya kukaa kutaleta mvuto wa mahali
pa kuishi.
Fanya
chumba cha kulala kiwe kama mahali patakatifu
Usingizi
mzuri wa usiku ni kipaumbele kwa watu wa kila umri. Hakikisha usingizi mwororo
kwa kuwa na kitanda na godoro linalofaa kwa kadri iwezekanavyo. Hii ni pamoja
na malazi na mwanga wa chumba.
Usafi
Kila nyumba ina upekee wake na mahitaji tofauti kuendana na
wakaaji wake.
Nyumba safi ni ile ambayo hakuna vyombo
vinavyoachwa vichafu iwe ni kwenye sinki, karo, beseni, ndoo, popote pale pa
kuoshea vyombo kuendana na maisha unayoishi na nguo chafu hazijazagaa kila
mahali sakafuni.
Ni kujitahidi kupambana na uchafu palepale unapotokea ikiwa ni
pamoja na kusafisha sakafu na kushughulikia madoa hasa palepale yanapotokea.
Nyumba safi ni nadhifu nje na ndani na kuna kanuni
mlizojiwekea hapo nyumbani ili kuiwezesha kuendelea kuwa safi.
Kuweka mapambo ya msimu
Kwenda na wakati kwa kuiweka nyumba katika hali ya wakati
uliopo kwa mfano wakati wa sikukuu kuweka mapambo yanayoendana na wakati huo
ambapo pia inaifanya nyumba igeuke kuwa nyumbani na kuwapa hisia waliomo juu ya
sikuuku hiyo.
Jiko litumike
Hapa ina maana kuwa ndani ya nyumba kupikwe. Kuna baadhi ya
nyumba ambazo hakupikwi ni watu wa kula barabarani tu. Ili nyumba yoyote ile
igeuke kuwa nyumbani ni muhimu sana kuwe na chakula kila wakati. Jiko
linapotumika kuandaa vyakula na harufu yake nzuri inaifanya nyumba kuwa na uhai
wa kuitwa nyumbani.
No comments:
Post a Comment