Kuna
kitu cha kipekee kuhusu bustani, maua -
mchakato wa kuotesha vitu hai kwa ajili ya kufurahisha nafsi na vilevile
kuongeza mvuto wa ndani ya nyumba kwa ujumla wake. Kama wewe ni mmojawapo ambaye bustani inakuhuisha
nafsi kiasi kwamba ungetamani kuwa nayo hata ndani kama ilivyo nje basi makala
hii ni kwa ajili yako. Ili
kufanikisha hilo zingatia dondoo zifuatazo:
·
Kuwa
makini na unapotaka kuweka ua au mmea wako
Linapokuja
swala la mvuto, maua au mmea fulani unapendeza zaidi ukiwa eneo fulani la ndani
ya nyumba. Kwahivyo fikiria eneo
unalolipenda na litakalokidhi mahitaji yako huku ukikumbuka kuwa mimea inapaswa
kuwa jirani na mwanga wa jua. Kama unachukua muda mwingi kukaa sebuleni
inawezekana ndipo unapenda kuongeza uhai kwa kupaongezea uzuri asili wa nje.
·
Jua
mahitaji ya mmea wa ndani
Unapokuwa
unafahamu vizuri mahitaji ya ua au mmea unaotaka kuotesha ndani itakusaidia kuuweka
mahali sahihi na vilevile kuchagua ile inayokidhi vigezo hivyo. Unaweza ukadhani
kuwa chumba kina giza sana haifai kuweka mmea lakini kumbe ukweli ni kuwa kuna
mimea na maua ambayo yanahitaji mwanga hafifu sana. Bila shaka umeshaona maua
ambayo yanahitaji kivuli kikubwa na yale ambayo ukiyaweka kivulini tu yanakufa.
Mgawanyo mzuri wa maua haya upo kwenye wale wauzaji wa bustani walizootesha
kando ya barabara. Utagundua kuwa yapo maua ambayo wameyaotesha juani kabisa na
yapo ambayo wameyaweka kule chini ya miti ambako hamna jua kabisa na mwanga ni
kidogo sana. Kwahivyo kwa namna hii hii unapaswa kufahamu juu ya hayo maua
unayotaka kuotesha ndani.
·
Mwagilia
kutokea chini
Huenda
kwenye umwagiliaji wako wote wa siku zote kwenye bustani za nje umezoea
kumwagilia juu kwenye majani. Kwa maua ya ndani unapaswa kumwagilia pale kwenye
udongo ndani ya chungu. Zipo pia kontena za kuoteshea maua haya ambazo zina
visahani. Unaweza kumwagilia kwenye kisahani na mizizi ya mmea huo ikajiloweka
yenyewe humo kufyonza hayo maji. Vilevile kuwa na ratiba na kipimo maalum cha
kumwagilia. Mimea mingi ya ndani inatosha kumwagiliwa maji glasi moja na mara 2
kwa juma ndani ya chungu kimoja.
·
Epuka
sehemu yenye joto sana au baridi sana
Mimea
ni vitu hai ambavyo ninadhurika na mabadiliko ya halijoto. Kama halijoto
itabadilika kuwa joto sana kwa mfano karibia na jiko au baridi sana labda kuna
kiyoyozi kikali muda wote ua likioteshwa kwenye mazingira kama hayo litakufa.
Epuka kuweka vyungu vyako vya maua karibia na maeneo hayo mawili.
No comments:
Post a Comment