Fahamu
faida na changamoto za maeneo mawili ya kuweka luninga
Uko
kwenye mchakato wa kuweka luninga na unafikiria uiweke juu ya kabati la luninga
au uisimike ukutani? Kuna mengi ya kujua kwenye kuchagua haya maeneo mawili
kabla hujafanya uamuzi wa mwisho.
Unapoamua
kama
uitazame luninga yako kupitia ukutani au kwenye kabati kuna mambo kadhaa
ya kuzingatia. Kuangalia faida na changamoto nitakujuza ukweli unachopaswa
kufahamu ambapo utapata jibu la njia utakayochagua ili iwe sawa kwa mtindo wako
wa maisha na unadhifu wa nyumba vilevile.
Tangu
kuingia kwa matoleo ya luninga flati, kuzisimika ukutani imekuwa ni njia mbayo
inafanya zionekane na kutizamika vizuri zaidi. Vilevile kusimika ukutani siku
hizi imekuwa hata maarufu zaidi kwa sababu huhitaji kuweka chochote sakafuni
kwa ajili ya kuishikilia. Namna hii inakifanya chumba ambacho luninga imewekwa
ukutani kuonekana kuwa na nafasi kubwa. Pia ni njia salama kwa watoto
wanaopenda kuchezea waya au kupanda juu ya kabati na pengine kuidondosha na kuivunja
luninga yako ya gharama. Zaidi ya muonekano wa kiwango na mvuto, njia ya
kusimika luninga ukutani ni sahihi hasa kwa wale wenye nyumba ndogo.
Faida
nyingine ya kuwa na luninga ukutani ni kwamba unaweza kutumia spika ndogondogo
za kuweka darini kwenye kona za chumba. Hii ina faida sana kwani waya zote
zinajificha hakuna inayoonekana wazi.
Tukija
kwa upande wa njia ya kuweka luninga juu ya kabati ni kuwa inachukua nafasi
kubwa kuliko ile ya kusimika ukutani. Makabati ya kuwekea luninga yanakuja kwa rangi
nyeupe, nyeusi na hata katika finishing mbalimbali za mbao na chuma. Ni ukweli kuwa
makabati ya luninga yanachukua nafasi kubwa ya sakafu na chumba. Kwa miundo
yake mengi yameongezewa maeneo ya hifadhi kama vile droo na shelfu ambapo kwa
upande mwingine ni faida kwamba unaweza kuhifadhia humo muvi, vitabu na hata michezo
ya kwenye luninga na hii inakusaidia kuweka mpangilio wa mahali luninga ilipo.
Ni
vyema upate majibu ya maswali haya matatu wakati wa kuchagua njia sahihi kati
ya hizi mbili ya kwamba usimike luninga ukutani au uiweke juu ya kabati.
·
Chumba
unachotaka kuweka luninga kina ukubwa kiasi gani?
·
Ni
kiasi gani cha hifadhi kinahitajika kwa ajili ya muvi na michezo ya video?
·
Je,
kuna hatari yoyote ya kusababisha luninga ianguke na kuvunjika?
Jambo
la muhimu ni kuwa, kwa njia yoyote utakayochagua, usalama iwe jambo la
kuzingatia zaidi. Baada ya hapo, hifadhi nayo ni muhimu. Na pia usisahau
muonekano, ambapo unachangia kukupa msukumo wa kuchagua kabati la luninga au
ukutani. Kila mmoja anataka ndani ya nyumba yake kuonekane kusafi na kuwa na
mpangilio ili kuvutie.
Kwa
hii elimu ndogo, yeyote anaweza kuamua atizame luninga yake ikiwa kabatini au ukutani.
Simu 0755 200023
No comments:
Post a Comment