Saturday, January 24, 2015

Nyumba safi ni ipi?



Naulizwa hili swali mara nyingi. Nyumba safi ni ipi? Na acha nianza kwa kusema kuwa hakuna jibu sahihi!

Kila nyumba ina upekee wake na mahitaji tofauti kuendana na wakaaji.

Kwa mimi najibu kuwa nyumba safi ni ile ambayo hakuna vyombo vinavyoachwa vichafu iwe ni kwenye sinki, karo, beseni, ndoo, popote pale pa kuoshea vyombo kuendana na maisha unayoishi na nguo chafu hazijazagaa kila mahali sakafuni. 

Nina ratiba yangu ya mambo ya kufanya kwa siku kwa wiki na kwa mwezi kufanya mazingira yaonekane safi, maridadi na nadhifu bila kufanya kazi kubwa kwa wakati mmoja.

Kuna usafi wa kufanya kwa kipindi (sio kila siku) kwa mfano ndani ya friji na microwave. Najitahidi kupambana na uchafu palepale unapotokea ikiwa ni pamoja na kupitisha fagio na kushughulikia doa hasa palepale linapotokea. 

Hata kama sipo nyumbani huo ni utaratibu uliopo na unaeleweka kwahivyo sitegemei kuja nikute doa kwa mfano kwenye carpet.

lla ukweli ni kuwa hakuna aliyekamilika. Kwangu mimi nyumba safi ni nyumba nadhifu. Kila kitu kina eneo na kimerudishwa eneo lake mara baada ya kutumika. Haimaanishi kuwa sakafu zinadekiwa tena baada ya chakula cha usiku – hapana sina muda huo kwakweli. 

Tafuta ratiba ambayo itawezekana kwako. Na kama una mwezni au watoto set “house rules” na mshirikishe kila mmoja hapo nyumbani.


Kadri ninavyopata muda nitakuwa nawashirikisha vidondoo vya jinsi ya kusafisha mahali unapoishi.

Super saturday for the boys


Friday, January 23, 2015

Jinsi ya kujiweka mazingira bora ya mafanikio kimaisha (1)

Nimekutana na makala hii na nikaamini kuwa nikiiweka hapa wapo watakaojifunza kitu hivyo kuwawezesha kuvuka kwenda level ya juu, tunajifunza kila siku. Mwandishi wake ambaye ni Dr. Chris pia ni marriage cousellor

Na DK Chris Mauki

Mafanikio ya kweli ya binadamu yanahusisha maeneo kama  mafanikio ya kiuchumi, kama vile kuwa na uwezo wa kujikimu na kumudu gharama za maisha ya kila siku.
Tunapozungumzia mafanikio binafsi, tunalenga kwa upana maisha ya mwanadamu. Unaposema mafanikio, wengi wanaelekeza mawazo yao kwenye kuwa na fedha, nyumba, magari na utajiri.

Mafanikio ya kijamii ni kama vile kuwa na mahusiano bora na wanaokuzunguka.
Mafanikio ya kiroho ni kama vile kuwa thabiti kwenye mambo ya kiimani.
Mafanikio ya kihisia ni  kama vile kuwa na uwezo wa kujimudu kihisia na kadhalika.

Ili kujiwekea mazingira bora katika kuyaelekea mafanikio yetu binafsi ni vyema ufahamu na kuweza kufanya yafuatayo.
Kutambua umuhimu wa muda na jifunze kuukomboa na pia kuwa na malengo na kuyatumia katika kuyatekeleza.
Jambo hili ni lazima kufahamu kuwa kamwe huwezi kuukomboa muda kama hujui umuhimu wake. 

Labda tuuangalie muda katika mitazamo tofauti.
Mtazamo wa kiimani ama kiroho, kuukomboa muda kumezungumziwa ndani ya vitabu vitakatifu kwa namna mbalimbali.
Baadhi ya maandiko yanaonyesha kuwa hata ibilisi mwenyewe anatenda kazi akijua kuwa wakati wake ni mchache sana.

Maeneo mengine katika misahafu imeeleza kuwa kati ya hatua za juu za busara ya mwanadamu ni  kujua umuhimu wa muda na kuukomboa.
Tukiangalia mtazamo wa kimaisha, watu wengi wameshindwa kufikia malengo yao waliyoyatamani kwa sababu ya kufikiri kuwa muda upo tele na kwa hivyo wangeweza kufanya walichokitaka wakati wowote na wakisahau ukweli kuwa muda ni mchache katika kila tunachotaka kukifanya.
Wenzetu Waingereza wana msemo usemao “There is little time for everything” wakiwa na maana kwamba kila sekunde, dakika inapaswa kutumiwa vizuri.

Kwa kutofahamu umuhimu wa muda wengi wetu wamekuwa wakifikwa na kihoro pale wanapokaribia kustaafu maana hamna walichokifanya wakiwa kazini.
Mara nyingi ninawashauri watu kuanza kuelekeza mawazo katika ile siku ya kustaafu mara tu unapoajiriwa.

Ukisubiri uwaze na kujiandaa kustaafu muda mchache kabla utajikuta unachanganyikiwa. Hii itakuwezesha kuelewa umuhimu wa muda mdogo ulionao kazini na namna ya kuukomboa ili usije kukuathirika baadaye.
Ni vyema ukifahamu ukweli kuwa uko vile ulivyo na jinsi ulivyo kwa kulingana na vile unavyoutumia muda wako.

Tumia muda wako kuwekeza katika busara na ufahamu, mfano; shule na kazi.
Katika  kutafuta kuwa na busara ni  lazima kufahamu kuna wakati wa kila jambo chini ya  jua na  lahitajika kutendeka au kufanywa katika muda wake mwafaka.
Wengi wetu tumepata hasara katika miradi mbalimbali maana tumeshindwa kujua muda mwafaka wa kuanza au kumaliza shughuli fulani au biashara  fulani.


Wiki ijayo tutaendelea na mada hii ya jinsi ya kujijengea mazingira bora kwa maisha ya baadaye kwa kuingia sehemu ya pili ya ‘Jifunze kuongozwa na malengo.’

MAHUSIANO: Tofauti ya kipato baina ya watarajiwa inaweza kusababisha haya mbeleni?

Kisa cha wapenzi wawili waliozua gumzo nchini Kenya
Sarika na mume wake Timothy wameachana baada ya Sarika kudai kwamba mume wake amekuwa akimdhulumu
Msichana mhindi Sarika Patel kutoka familia tajiri na Timothy Khamala mbukusu kutoka familia maskini kutoka Magharibi mwa Kenya kuoana? wakati yao mapenzi yao yalijulikana kama Bukusu Darling, sifa kwa wanakoishi wawili hao.
Taarifa sasa ni kwamba mapenzi yao yamefika kikomo. Familia ya msichana Sarika ililaani sana mapenzi hayo kwani Timothy alikuwa anafanya kazi kwao kama mfanyakazi wa nyumbani.
Na Sarika alipoamua kwenda kuishi na Timothy kama mume na mke familia yake ilimfukuza na kisha kumfuta kazi Timothy.
Wawili hao walioana kinyume na matakwa ya familia ya Sarika ambayo kwao ilikuwa ni kama aibu kubwa sana kwa mtoto wao kutoka familia tajiri kuolea na kijana asiyekuwa na mbele wala nyuma.
Wakati taarifa ya wawili hao ilipogonga vichwa vya habari nchini Kenya, Sarika na mume wake walipata kazi katika kiwanda cha kutengeza Sukari kutoka kwa wahisani.
Lakini sasa kuna madai kwamba ndoa yao imevunjika baada ya Sarika kulalamika kwamba Timothy amekuwa akimdhulumu na kumtusi kila mara hali iliyosababisha wawili hao kutalakiana.
Mtandao wa Standard Digital umemnukuu Sarika akisema: "nilipokuwa mgonjwa , hakuwa hata na muda wa kunipeleka hospitalini badala yake wazazi wake ndio walionipeleka kutafuta matibabu. Mbali na hayo amekuwa akinichapa, '' alisema Sarika huku akibubujikwa na machozi.
Kwa sasa inaarifiwa anajuta sana kwa nini alikaidi amri ya wazazi wake.
''Ninajuta sana kwa nini sikuwasikiliza wazazi wangu na kuolewa kinyume na mapenzi yao. Ninaomba radhi, natumai watanikubali kurejea nyumbani. ''
Sarika ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano, ameamua kurejea nyumbani na kusema kamwe hatawahi kuwa na uhusiano wa kimepenzi tena. Lakini wazazi wake wamempa masharti, mwanzo aishi na rafiki yake huku akifanya uamuzi wa mwisho kuhusu anakotaka kuishi.
Anasema anahofia kwamba jamii ya wahindi haitamkubali tena kwani hakuwasikiliza wakati walipomshauri kutoolewa na mwanamume mwafrika.

MAHUSIANO: Majivu kwa ajili ya kuzuia mimba?! Wanayalamba??


Baadhi ya wanawake wanaamini kwamba wakitumia njia za kisasa wanaweza kuharibu maumbile yao ya mwili ya asilia pamoja na kupata ulemavu.
Wapo wanaoamini kuwa uzazi wa mpango upo kwa ajili ya kupunguza idadi ya watu kwa kuua mayai ya uzazi pindi watakapotumia dawa za kisasa kama kuchomwa sindano, kumeza vidonge, vipandikizi na kuwekewa kitanzi.
Kutokana na kuamini njia za kisasa zina athari kwa afya zao, baadhi ya wanawake hususan waishio vijijini wanatumia majivu kama njia ya kuzuia kupata mimba.
Hali hiyo imekuwa ikichochewa na waume zao kutowaruhusu kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Wapo wengine wanakoroga bluu na kunywa pindi wanapohisi wamepata mimba ikiwa ni imani ya kwamba mimba itaharibika.
Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ina hospitali moja iliyopo Mwadui  maeneo ya mgodini. Wilaya hii pia ina vituo vya afya  vinne, zahanati 45 za Serikali na  nne za  watu binafsi.
 Wanawake katika vijiji vya Ilebelebe, Ikoma na Itilima wanaeleza kuhusiana na mikanganyiko hii ya njia za uzazi wa mpango.
Wanawake wanasema nini?
Mkazi  wa Kijiji cha Ilebelebe, Suzana Mhoja (37) mwenye watoto sita anasema baadhi ya wanaume  wamekuwa chanzo cha wanawake kushindwa  kutumia  uzazi wa  mpango kwa kuhofia kuvunja ndoa zao  kutokana na kutoruhusiwa kwa imani kuwa wataua mayai  ya  uzazi.
Anasema yeye ni miongoni mwa wanawake waliowahi kutumia majivu kama njia ya kuzuia kupata mimba baada ya kupata taarifa kutoka kwa wanawake wenzake.
Anasema licha ya kutumia majivu, alibeba ujauzito kabla ya muda wa miaka miwili aliokuwa amepanga uwe na wa kupumzika ili kutoa nafasi ya kulea aliyetangulia.
“Sitamani tena kuendelea kuzaa lakini wanaume hawataki kabisa kusikia suala hilo la njia za mpango wa kisasa. Ningeweza kutumia kwa siri lakini nahofu ya kuvunja ndoa yangu,” anasema.
Wakazi wa Kijiji cha Ikoma, Sophia Maige (29) na Salume Mshamindi (33) wanabainisha kuwa kama huduma za afya zingekuwa katika kila kijiji, uzazi wa mpango ungefanikiwa vizuri kwani elimu ya uzazi wa mpango ingewafikia wanaume kwa urahisi tofauti na ilivyo sasa.
Chanzo: Mwananchi

Hizi ni mifano ya sofa mbalimbali kwa watu wa lifestyle mbalimbali

Kuanzia kulala wakati unatizama TV hadi "kufanya" kazi zako za ofsini, sofa ni fenicha ambayo inatumika sana nyumbani kwahivyo kununua  ya kudumu na kuendana na maisha unayoishi ni big deal. Kuna vigezo vya msingi vya kutafiti kabla ya manunuzi (fikiria: fremu, spring na cushion, kama utataka kujua zaidi tembelea GoodHousekeeping.com kwani sio lengo la post hii kwa sasa).

Sasa basi lengo ni kuangalia sofa mbalimbali kwa lifestyle mbalimbali:
 Sofa kama hili ni kwa wale wanaopenda rangi, wanaopenda kupamba yani akiona decor item yoyote colorful anasuuzika moyo.
 sofa hii ni kwa couple inayochukua muda mwingi kuangalia TV pamoja, na mara nyingine kunakuwa na argument za hapa na pale, hadi miguu wanaiweka juu ya meza
 Hii ni kwa yule anayependa kupata kiusingizi cha mchana kwenye sofa
 Sofa mfano huu utamfaa mwenye sebule ndogo.
 Kama una wageni wengi sofa ya rangi hii inakuhusu, kuna wageni wanafikia hadi kunyanyulia miguu kwenye sofa, mwingine katoka alikotoka na vumbi limemjaa miguuni lakini kwake sio issue.
Wewe bachelor ambaye hujajua kama mke wako mtarajiwa atapenda ulivyo navyo ama laa sofa kama hii ni sahihi kwako. Yenyewe iko simple kwahivyo hata kama akiidis mwenyewe hutajuatia mnanunua tu nyingine.

Kicheko cha kuanza furahi day

Marafiki zangu wa ukweli wakielekea shule asubuhi hii. Wenyewe wanafurahi kwamba kesho hawaaamki na giza.


Thursday, January 22, 2015

MAKAZI: Mshindi wa BBA Idris Sultan amenunua nyumba, hongera zake




Chandelier hizi ndio taa za kisasa zaidi kwa ajili ya dining room

Huenda uko kwenye harakati za kuwa na kiota chako binafsi (hata ndege wanacho kwanini wewe ushindwe), usiweke tu kibalbu kimoja au viwili kwenye chumba cha dining. Dining ni muhimu iwe na mwanga wa kutosha kwa ajili walaji waone chakula wasije wakalia humo mende.....ha ha haha  ahaaa. Hizi hapa basi ndio chandelier za kisasa zaidi kwa ajili ya dining yako hiyo mpya. Japo vyumba ni vya mamtoni usijali we tazama taa tu halafu wakati wa kununua za kwako utakuwa tayari una idea...






MY ARTICLE FOR NEWSPAPER: Amri 10 za kuweka mpangilio wa vitu mahali unapoishi

worth reading again and again

Umeshawahi kutamani kuona kwa haraka kile unachokitafuta? Je vitu vyako mara kwa mara viko hovyo hovyo vimesambaa kila mahali? Kama ndivyo basi, jifunze jinsi ya kuweka mpangilio wa vitu nyumbani kwako kwa kusoma amri hizi kumi tunavoelekezwa na mjasiriamali na mbunifu wa ndani Bi Alma Said.

1. Weka vitu vinavyofanana pamoja. “Unapopangilia vitu vyako weka vinavyoendana pamoja ili kuleta mtiririko na mantiki. Kwahivyo acha kuweka chochote popote, inaweza kusaidia ndani ya muda mfupi lakini ikafanya eneo lote lionekane mvurugano.

2. Fikiria kabla ya kununua. Kununua kwa mhemko ni kifo cha mpangilio wowote. Unataka kununua kitu? Kinahitaji makazi. Kuwa na uhakika na mpangilio wako kabla hujaleta chochote kipya nyumbani kwako. Inasikika kama msongo eeh? Ndio, panga kabla ya kununua: hiki kitakaa wapi? Je una nafasi, kama majibu ni sijui na hapana  basi acha usinunue (jumlisha na kuwa utakuwa umehifadhi hela yako).

3. Kila kitu kina mahali pake, kiweke hapo. Kwa lugha nyingine ni kuwa na eneo kwa kila kitu. Zaidi ya kuweka vitu mahali pake ni kuwa pia kila kitu kinatakiwa kiwe na mahali pake kabla hujakiweka hapo!

Eneo kwa kila kitu kwa mfano ufuatao, eneo la:
Hiyo kalamu wakati ambapo huiandikii.
Waya za kuchaji kamera na simu wakati ambapo hazitumiki.
Barua ambazo hazijasomwa.
Soksi ambayo mwenzake haonekani anasubiriwa kutafutwa.
Vipeperushi na magazeti ambayo utasoma utakapopata muda, na vitu vingine vingi vingi hapo nyumbani.
Unataka kufahamu ni vitu gani hapo nyumbani vinahitaji eneo lake maalum? Anza kwa kutizama kwenye kaunta yako ya jiko. Kama kuna chombo kipokipo tu ni kwa sababu hujakitafutia eneo maalum.

4. Zishukuru kumbukumbu zako halafu ziage. Hapana, sikushauri ulitose hilo gauni lako la harusi. Kumbukumbu nyingine ni muhimu mno na zinahitaji eneo kwenye nyumba yako maisha (wengine hadi wanazikwa na magauni yao ya harusi). Lakini hizo CD na mikannda ya filamu? Fikiria mara mbili kabla hujabaki na hiyo kumbukumbu unayotaka kuhifadhi maisha.

5. Weka nguo zako mbali. Ndio najua unaguna, lakini fanya hivyo, hakuna msamaha kwa hili. Nguo sio za kuwepo kila mahali. Tundika zilizo safi, kunja za kukunja, fua zinazotakiwa kufuliwa na loweka za kuloweka. Mwisho wa hadithi. Mrundikano wa nguo ni janga la nyumba nyingi. Kutumia muda mchache kila siku kushughulikia swala la kuweka nguo panapotakiwa  itafanya mahali unapoishi paonekane nadhifu na hivyo kurahisisha maisha yako kwa muda mrefu.

6. Tumia vikontena vilivyopo kwa lengo lingine pindi vimalizapo lengo moja. Kwa maana nyingine ni kuwa tumia kile ambacho tayari unacho. Nimeona watu wanaotumia vikopo vilivyoisha biskuti ama chokoleti kwa ajili ya kuhifadhia vitu kama hereni na vipodozi.

7. Weka kituo cha amri . Manake ni kwamba kituo hiki ndicho kinachokaa vile vitu kama funguo, mifuko, yani vile vitu ambavyo vinatumika mara kwa mara kwenye pilika za kila siku. Hutakuwa na haja ya kutafuta ama kuanza kuuliza kama utakuwa na kituo cha amri nyumbani kwako.

8. Weka ratiba ya siku. Na hakikisha unaifuata. Ratiba ni uti wa mgongo wa mipangilio. Hakikisha kila siku unatenga muda wa kurudisha vitu pale vinapotakiwa kuwa, faili ripoti za watoto za shule na karatasi nyingine muhimu, tandika kitanda na kadhalika ni kuwa nyumba yako itakushukuru. Kumalizia siku na nyumba yenye mpangilio ni kweli kuwa unajisikia vizuri ajabu.

9. Anza kidogo kidogo. Kama huna karama ya kuweka vitu kwenye mpangilio anza kidogokidogo na vitu vidogodogo kama vile hicho kituo cha funguo, taratibu utashika kasi na kufika hadi kwenye kabati za nguo. Furahia kimpangilio kidogo unachoanzia ambapo kitakupa stamina ya kusonga mbele.

10. Usichoke. "Kumbuka kuwa wewe ndio msimamizi wa nyumba na vitu vyako. Kama utaiambia akili yako nataka kuishi mahali penye mpangilio, muda si muda haitajisikia kuchoka. Umesongwa? Sawa, chukua mapumziko kidogo.

Sasa msomaji wangu umeelimishwa juu ya amri kumi za kuweka mpangilio wa vitu nyumbani, je wewe ni mmojawapo wa wale wenye vitu ambavyo havina makao bado? Niandikie ukinijulisha ni kwa namna gani umefaidika na makala hii kwa kuvipa eneo vitu hivyo leo!


Makala hii imeandaliwa na Vivi Machange ambaye ana mapenzi makubwa ya muonekano wa nyumba. Kwa maoni au maswali tuma kwenda 0755 200023 au christines.daughter@yahoo.com

MAHUSIANO: 'My wife has become a man but it's made our marriage stronger than ever'

Duniani ni full kuchannganyikiwa walimwengu hata hawajui tena wanachokitaka, wazungu na maisha yao...hebu soma kituko hapa chini:

Most husbands would be shocked and lost for words if their wife wanted to become a man. But for Graham Hopwood it came as no great surprise – and now he’s happy that at the age of 48 the love of his life finally has the body she had always craved. In the past year Catherine has transitioned to become a man called Cathan. And although they no longer have sex, the couple say their 12-year marriage is stronger than ever. Graham, 68, from Bradford, says: “Inside Cathan is still the same person I met and fell for. I always knew that Catherine wasn’t happy with her body so when she opened up to me about wanting to be a man I wasn’t all that surprised. I wanted to help her to be happier in herself. “The only confusion we have these days is knowing what to call him. I can’t say wife any more so I usually say partner.” Cathan says: “My husband is the most wonderful man in the world and we’ve always supported each other. "He’s been so good to me this year as I’ve had my breasts removed and transitioned to a man. People ask us if we’re going to split up but we wouldn’t dream of it. He’s my rock.”
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/

MAHUSIANO: Wema ampeleka Diamond polisi


MKALI wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu ‘Wema’, amemfungulia kesi ya madai mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, kwa kumtapeli kiasi cha Sh milioni 10.

Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la Utangazaji (BBC) idhaa ya Kiswahili, Wema aliripoti madai yake kituo cha Polisi Oysterbay akidai kuwa alimpatia mwanamuziki huyo kiasi hicho kwa makubaliano ya kazi na kuahidi kumlipa, lakini amekwenda kinyume makubaliano yao.
Muhusika mkuu ambaye ni Wema alitoa maelezo kwamba watu wanamtupia lawama kutokana na hatua aliyofikia, lakini amedai kuwa amelazimika kufanya hivyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeingia dhamana na taasisi Focus Vicoba kuchukua fedha hizo.
“Naona watu wengi wananilaumu kwa kuwa nimemfungulia kesi Diamond, pasipo kuelewa kama fedha hizo pia hazikua zangu bali ni mkopo ambao niliingia dhamana katika taasisi ya utoaji mikopo ya Vicoba.
“Kupitia mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia Diamond, ili aweze kuandaa miradi yake tena kwa makubaliano kuwa atazirudisha ili tuweze kufanya marejesho ya mkopo tuliochukua,” alisema Wema.
Mrembo huyo alieleza muda waliiopeana ahadi ya kurudisha fedha hizo umepita na Diamond haoneshi dalili ya kuzirejesha wakati wanatakiwa kuzirudisha kwa wakati .
“Yote haya yasingenikuta, lakini sina jinsi kwani natakiwa kurudisha pesa za watu nimekuwa nikimpigia simu 

Diamond hataki kupokea simu zangu, lakini kama alitaka kunidhulumu ni bora angejiunga mwenyewe na hawa Vicoba ili apate mkopo na kufanya mambo yake au kama aliona hawezi kwa kujishtukia basi angetumia ile tovuti yao, angepata kwa urahisi na hakuna mtu yeyote angejua kama amekopa ila sio kukimbia kulipa deni la watu,” alisema.
Hata hivyo Diamond ambae kwa sasa yupo nchini Burundi kwa ajili ya ziara yake kimuziki, tayari ametumiwa taarifa na jeshi la polisi kwa barua ya wito kufika kituoni pindi atakaporejea nchini, huku mama yake mzazi akifikishiwa ujumbe huo nyumbani kwake.
Wema ambae alimwekea dhamana, yupo katika kipindi kigumu ambacho kinaweza kupelekea kufilisiwa mali zake ambazo aliziandikisha wakati wa kuchukua mkopo huo ili ziweze kufidia deni hilo.
Kwa mujibu wa kiongozi wa taasisi hiyo ambae aligoma kutajwa jina lake gazetini, alisema kuwa ni kweli Wema alifika katika ofisi zao zilizopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ili apewe muongozo lakini alipotakiwa kufuata taratibu za kiofisi kama wanachama wengine wanavyofanya katika vikundi, hakukubaliana na utaratibu, hivyo kushauriwa ajiunge kupitia tovuti .
MTANZANIA ilimtafuta Meneja wa Wema, Martin Kadinda, ambae alieleza hajui chochote kuhusu kufungulia kwa kesi hiyo, akaomba apewe muda kumtafuta msanii huyo ili aweze kupata ufafanuzi juu ya suala hilo, lakini hakueleza nini kilichojiri na kusisitiza asubiriwe.
Gazeti hili halikuishia hapo, lilimsaka Meneja wa Diamond, Babu Tale, ambae alionekana kushtushwa na habari hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote.

Habari hii ni kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania 

MAHUSIANO: Ouch! Eti kujamiiana mwanamke akiwa juu ni hatari kwa mwanaume

Sex with the woman on top is the most dangerous position for men, say scientists - but having him on top is the safest 

Scientists have learned that the 'woman on top' or 'cowgirl' position is the most dangerous one for men to engage in during sexual intercourse.
According to new research, the risky position is to blame for half of all penile fractures that occur during sex. In comparison, 'doggy style' or the woman on all fours is responsible for 29per cent of injuries, while 'man on top' or 'missionary' is only liable for 21per cent. 

In the study published in Advances in Urology, researchers hypothesized that a man is prohibited from quickly stopping a painful movements when a woman has her entire body weight on his erect penis.

"nitavukaje": Umuhimu wa kutunza kumbukumbu katika biashara yako

Wengi wameanzisha biashara kwa nia ya kuvuka kutoka level moja kwenda ya juu, soma hapa upate desa la kuweza kupaa katika biashara yako.

Katika hali ya kawaida siyo rahisi kukumbuka kichwani kila aina ya muamala unaofanyika katika biashara.
Hii inatokana na ukweli kuwa kichwa cha binadamu kina mambo mengi ya kuingia na kutoka kulingana na hali halisi ya maisha ya kila siku. Kwa kuzingatia hali hii, ndiyo maana kuna umuhimu wa kutunza kumbukumbu za biashara ili kuifanya iendeshwe kitaalamu. Kimsingi, utunzaji wa kumbukumbu za biashara una faida zifuatazo:

Husaidia kulipa kodi stahiki kwa taasisi husika kama vile TRA. Ikumbukwe kuwa nchi huendeshwa kwa kodi. Bila kulipa kodi hakuna maendeleo na huduma za jamii. Pia, ili biashara iweze kukua sharti ilipe kodi kulingana na ukubwa wake. Iwapo utalipa kodi kubwa kuliko kipato chake, biashara hiyo itakufa. Hivyo, kumbukumbu za biashara husaidia kuondoa malalamiko ya ulipaji kodi kubwa au ndogo kuliko hali halisi ya biashara.

Pia, kusimamia na kudhibiti kiwango cha bidhaa iliyopo na inayotakiwa kuwapo. Utunzaji kumbukumbu za biashara husaidia kujua muda unaopaswa kuagiza bidhaa husika. Ni makosa katika biashara kuishiwa bidhaa inayohitajiwa na wateja, kwani mjasiriamali anaweza kupoteza wateja hao. Vilevile siyo vizuri kuwa na akiba ya bidhaa nyingi ambayo hainunuliki. Tatu ni kujua kiasi cha fedha kilichopokelewa. Biashara yoyote ile huingiza fedha ambazo hutumika katika kuendeshea biashara husika. Kwa kuweka kumbukumbu sahihi za mauzo ya kila siku kunamsaidia mjasiriamali kujua kiasi cha fedha kinachoingia kila siku, mwezi na hatimaye mwaka mzima.

Hata kujua kiasi cha fedha kilichotumiwa na namna kilivyotumiwa. Fedha inayotokana na biashara hutumika kwa mambo mengi. Baadhi yake ni kununulia/kutengeneza bidhaa zinazohitajika katika biashara husika ikiwa ni pamoja na matumizi ya kawaida.
Kusaidia katika ukokotoaji wa mahesabu. Ili kujua kuwa biashara husika ina faida au hasara sharti kuwapo ukokotoaji wa mapato na matumizi. Kama mapato yatazidi matumizi biashara hiyo itakuwa inaingiza faida. Kama matumizi yatakuwa yanazidi mapato basi biashara husika itakuwa inaingiza hasara na hivyo kuelekea kufa.

Mathalan, kusaidia katika kutoa uamuzi sahihi juu ya kipi cha kununua na kuuza. Uwekaji wa kumbukumbu za biashara husaidia kujua bidhaa inayohitajika na ile inayotakiwa kuuzwa kabla haijaleta hasara. Biashara huna na bidhaa nyingine ambazo hazinunuliwi kwa kasi inayohitajika na hivyo kuzifanya kuwa katika hatari ya kuleta hasara katika biashara. Kwa kutumia utaratibu wa kuweka kumbukumbu mjasiriamali ataweza kuzibaini na kuzitafutia ufumbuzi kwa manufaa ya biashara husika.

Kutunza kumbukumbu ya miamala inayofanyika kwa mikopo husaidia kuepuka udanganyifu wa baadhi ya watu. Pasina kumbukumbu juu ya miamala inayofanyika kwa njia ya mkopo, kunaweza kusababisha kutokumbuka nani anadaiwa na kwa kiwango gani. Pia, husaidia kukomesha tabia ya baadhi watu ambayo hukana madeni pale wanapobaini kuwa mdai hakuweka kumbukumbu yoyote yenye kuwabana. Aidha, kuepukana na matumizi mabaya ya fedha na hali ya kutoaminiana katika biashara. Kama hakuna kumbukumbu sahihi za biashara ni rahisi kutumia pesa vibaya. Biashara inaweza kuwa kama shamba la bibi ambalo ni mali ya kila mtu. Uwazi, kwa sababu kila kitu huwa kiko bayana katika maandishi ambayo pande zote mbili zimehusika.

Kujua kama biashara inaendeshwa kama inavyotakiwa ili kuhakiki hesabu za mwaka.
Imeandikwa na Chiraka Muhura.

Wednesday, January 21, 2015

MAHUSIANO: Hili sijui lina ukweli kiasi gani, soma hapa sentensi 4 ambazo single women hawataki kuzisikia

1. "Kwanini bado upo single?"
Bibie Mary ni single lady na alikuwa na haya ya kusema:
Yani ni kuwa hamna jibu zuri lolote kwa swali kama hili. Kwanini niko single? Sijui. Labda….Kwasababu tu nipo…Kusema kweli sina cha kukujibu.
Na unataka mtu akujibu kwa undani ni nini kinawakimbiza wanaume pale tu wanaponijua kwa undani? Yani unataka nirudi hatua nyuma kwenye mahusiano yangu yaliyopita kuanza kutafuta makosa ambayo yamenifanya nisiwe nimeshavaa shela? Au unaniuliza tu hili swali kwa kudhani kwamba mimi  mwenyewe hajiulizi?
Pengine labda umeniuliza hili swali kwa kutaka kunisifia kuwa nina mvuto au hata pleasing personality (hii ni ile tu kuwa yeyote akikuona hata kama hujaongea au kufanya chochote anavutiwa nawe), basi kama hoja ndio hiyo nisifie tu bila kuuliza swali hili, inatosha.
2. "Muda unakutupa mkono/miaka inaenda."
Unajuaje kama ninatamani kuwa na mtu, kwani inakuhusu?

3. "Unachagua sana."
Hii inatokea kwa wale wanaojidai kuwa wanamjua sana mhusika na kumbe hawamjui hata kivile. Hoja kwamba watu wawili wa jinsia tofauti wako single haiwafanyi kuwa wataweza ku mingle wawe pamoja, moja ongeza moja ni 2 lakini moja mara moja sio 2…vigawe vingine pia vinatumika sio jumlisha tu!

4. "Unatakiwa kujichanganya zaidi."
Mary anakuambia, nimehudhuria chuo, sekondari, kanisani, makongamano na hadi party za singles, nimesaini online site za dating, nilienda kwenye first dates nyingine mwaka uliopita kuliko mtu yeyote anavyoweza kwenda. Tafadhali usiniambie tena eti bado nipo single kwa ajili sijichanganyi.


Utafiti unasema kuwa 63 percent ya wanandoa walikutana kupitia marafiki. Wanandoa wengi walikutana kwa ajili marafiki zao waliwa introduce kwa waliokuja kuwa wenzi wao. Kwahivyo siko single kwa kuwa nimezubaa ila huenda niko single kwa sababu yako. Itasaidia zaidi, badala ya kuwaambia wanawake single wajichanganye zaidi, host nyama choma au dinner nyumbani kwako na uwa introduce warafiki zako wa kike walio single kwa eligible bachelors unaowajua.

MAHUSIANO: Dawa ya wanaotoka nje ya ndoa hii hapa

WASWAHILI husema kwamba siku za mwizi ni arobaini.Msemo huo sasa huenda ukafanikishwa miongoni mwa akina baba ambao huenda kinyume na ndoa zao.

Hii ni baada ya kubuniwa kwa kifaa kinachojulikana kwa jina Semenspy kilicho na uwezo wa kubaini majimaji yaliyosalia katika nguo za ndani, nguo za kulalia na katika maeneo mengine baada ya mtu kuhusika katika tendo la ngono.

Kulingana na gazeti la The Nairobian nchini Kenya, maagizo yake ni kwamba iwapo unamshuku mumeo ama mkeo tafuta majimaji hayo katika chupi ama nguo zilizotajwa hapo awali kisha uyachunguze katika kifaa hicho.

Kulingana na daktari Wachira wa DIY Solutions, kifaa hicho kimetengenezwa Marekani na imebainika kwamba wamefanikiwa kupata majibu sahihi kutoka kwa wanawake waliotaka kujua iwapo waume zao na marafiki zao wa kiume wanawadanganya katika uhusiano baada ya kuyachunguza maji maji hayo.


Mi nadhani mtu kweli kama katoka kusaliti atakuwa mkali kama mbogo sidhani hata hayo majimaji unaanza kuyapataje..

MAHUSIANO: Wengi hawana muda na tendo la ndoa Japan

Asilimia 50 ya watu wazima nchini Japan hawashiriki katika tendo la ngono kulingana na utafiti, swala linalosababisha kupungua kwa idadi ya watu nchini humo.

Ripoti hiyo iliofanywa na shirika la upangaji uzazi nchini humo imebaini kwamba asilimia 49.3 ya watu 3000 waliohojiwa hawakushiriki ngono mwezi uliopita.
Kati ya asilimia 48.3 waliohojiwa walisema kuwa hawakushiriki katika ngono kwa mwezi moja huku asilimia 50.1 ya wanawake wakijizuia kushiriki ngono.Takwimu zote zilipanda kwa asilimia 5 kutoka kwa ufatiti uliofanywa awali mwaka 2012.
Walipoulizwa ni kwa nini hawashiriki katika tendo la ngono, asilimia 21.3 ya wanaume walio katika ndoa walidai kuchoka baada ya kutoka kazini huku asilimia 15.7 wakisema kuwa hawana haja ya kushiriki katika tendo la ngono baad ya wake zao kujifungua.
Kati ya wanawake asilimia 23.8 walisema kuwa tendo la ngono linasumbua na asilimia 17.8 wakidai walikuwa wamechoka.
Swala jengine la kushangaza ni kuongezeka kwa idadi ya vijana ambao hawana hamu na tendo la ngono.Zaidi ya asilimia 20 ya wanaume walio kati ya umri wa miaka 25 na 29 hakuwa na hamu ya kufanya ngono.

Tuesday, January 20, 2015

Amri 10 za kuweka mpangilio mahali unapoishi

1. Weka vinavyofanana pamoja. Hii itasaidia kuleta mantiki na hivyo urahisi wa kuona vitu vilipo. Unaporundika eneo lote linakuwa kama uchafu na vurugu na kukosa mvuto

2. Fikiri kabla hujanunua kitu. Kununua kwa mhemko ni kifo cha mpangilio wowote ule, chochote unachonunua kinahitaji pa kuwekwa. Panga kabla ya kununua: Kitakaa wapi? Nina nafasi ya kukiweka? Kama majibu ni sijui ni na hapana achana nacho (nyongeza ni kuwa utakuwa umesevu hala yako).

3. Kila kitu kina makazi. Kiweke eneo lake.

4. Heshimu kumbukumbu zako – halafu ziage. Ha ha ha haaaa, sikuambii ulitose gauni lako la harusi, kumbukumbu nyingine zinagusa mno kwahivyo zinahitaji eneo kwenye nyumba yako maisha. Lakini CD sijui muvi fulani, inaweza ikawa ni muda wa kufikiri mara mbili ni kumbukumbu gani unayotaka kubaki nayo maisha.

5. Weka nguo mbali. Lakini mmmmh! Najua, najua unaguna, sio kila mahali kila chumba nguo zinazunguka watu. Hapa namaanisha safi ziwe kwake, chafu ziwe kwake, zinazofuliwa ziwe kwake itafanya maisha yako yawe mazuri zaidi kwa muda mrefu. 

6. Tumia vikontena vilivyopo kwa lengo lingine pindi vimalizapo lengo moja. Nimeona watu wanaotumia vi can vilivyoisha biskuti ama chokoleti kwa ajili ya kuhifadhia vitu kama hereni na vipodozi.

7. Weka kituo cha amri . Manake ni kwamba kituo hiki ndicho kinachokaa vile vitu kama funguo, mifuko, yani vile vitu ambavyo vinatumika mara kwa mara kwenye pilika za kila siku na unapovihitaji usipoviona fasta kichwa kinavurugika. Hutakuwa na haja ya kutafuta ama kuanza kuuliza kama utakuwa na kituo cha amri nyumbani kwako.

8. Weka ratiba ya siku. Na hakikisha unaifuata. Ratiba ni uti wa mgongo wa mipangilio. Kama kila siku unatenga muda wa kurudisha vitu pale vinapotakiwa kuwa, faili ripoti za watoto na karatasi zako muhimu, tandika kitanda, nyumba yako itakushukuru. Kumalizia siku na nyumba yenye mpangilio ni kweli kuwa unajisikia vizuri ajabu.

9. Anza kidogo kidogo. Kama huna karama ya kuweka vitu kwenye mpangilio anza kidogokidogo na vitu vidogodogo kama vile hicho kituo cha funguo, taratibu utashika kasi na kufika hadi kwenye kabati za nguo. Furahia kimpangilio kidogo unachoanzia ambapo kitakupa stamina ya kusonga mbele.

10. Usichoke. "Kumbuka kuwa wewe ndio msimamizi wa nyumba na vitu vyako. Kama utaiambia akili yako nataka kuishi mahali penye mpangilio, muda si muda haitajisikia kuchoka. Umesongwa? Sawa, chukua mapumziko kidogo.


Sunday, January 18, 2015

NYUMBANI: Hii herb savor itakusaidia kuhifadhi giligilan zako kwa muda mrefu

Ulishawahi kushangaa ni kwanini giligilani zako fresh unazonunua sikoni zinaharibika ndani ya siku chache sana? Unaweza tu kuzitumia kwa siku moja au mbili basi. Usijali, kwa hii herb savor utaweza kutumia giligilani zako zikiwa bado fresh kwa zaidi ya wiki! Ni kiasi tu cha kuziweka kwenye hiki kidude, tia maji na hifadhi kwenye friji.

NYUMBANI: Vitu hivi vitatu vitakusaidia kuongeza nafasi ya kuhifadhia kwenye jiko lako

Haijalishi unaishi kwenye bangaloo, mansion au chumba na sebule bila shaka ulishajisikia kupungukiwa na eneo la kuhifadhia mahali unapopikia. Ukiweza kuongeza vitu hivi utaweza kuhifadhi zaidi...
kimeza kama hiki chenye matairi kitakuwezesha kuhifadhi vyakula kama matunda, vitunguu na hata nyanya ambazo hazijaiva vizuri

vyombo vyako vya udongo utapenda vionekane, kikabati kama hiki unaweza kukiweka kwenye corridor ama dining.
Njia ya tatu ya kuongeza eneo la kuhifadhia jikoni ni kuongeza ukubwa wa makabati yako ya jikoni ambapo yatachukua eneo lote hadi kwenye ceiling. Kwahivyo ile sehemu ya ukuta ilnayokaa bure inakuwa occupied na makabati.

eti kuna uhusiano kati ya makalio ya mama na akili ya mtoto!

bottoms makes up babies' brains say scientists, with curvy girls producing more intelligent children
  • Scientists found fats in women's behinds were vital for development
  • Researchers claim such cells are routed directly towards baby's brains
  • It helps explain why women find it difficult to shed weight from areas
  • Ladies with larger stores of such fat 'likely to produce smarter children'
Fat supplies found in a woman's thighs and buttocks are needed to develop babies' brains, scientists have claimed. 
The cells were found to contribute directly to brain development during breastfeeding, with a woman's behind acting as a reserve for vital nutrients.  

The claims were made by researchers from the University of Pittsburgh, who added that women with large quantities of such fats in target areas were shown to produce more intelligent children.

Saturday, January 17, 2015

mahusiano: mbunge abwagiwa mtoto kikaoni Dar

Ee jamani... kwanini wazima wachukuliwe aachiwe mlemavu?

Mwananchi linaripoti kuwa....
Hawa Kundani (mwenye vazi jeusi), anayedai kuzaa na kutelekelezwa na mbunge wa Dimani, Abdallah Sharia Ameir, akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kuvamia kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kilichokuwa kikifanyika Dar es Salaam jana. Picha na Beatrice Moses


Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Hawa Kundani amezua taharuki kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, baada ya kuvamia ghafla na kupiga kelele akidai kutelekezwa na mumewe ambaye ni Mbunge wa Dimani (CCM) visiwani Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir.

Tukio hilo la aina yake lilitokea jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, na mwanamke huyo akiwa ameongozana na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio, Joyce Kiria aliingia na kusababisha mshtuko kwa wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa dini ya Kikristo waliokuwa wamealikwa hapo. Wakati huo walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya Kadhi.

Hawa akizungumza na gazeti hili alidai kwamba Ameir ni mume wake walifunga ndoa mkoani Arusha mwaka 1999 na kuzaa naye watoto wanne, lakini mmoja alifariki dunia.
“ Nashangaa amebadilika ghafla amekuwa mtu wa kuoa wanawake na kuacha mara kwa mara, hadi sasa ameshaoa wanawake wanne na kuwaacha mimi nipo tu, alinioa bado mdogo,” alidai Hawa.

Alidai kuwa watoto wengine wawili, mkubwa ana miaka tisa na mwingine miaka sita walichukuliwa na mumewe huyo akawapeleka kulelewa na mwanamke aliyemuoa jambo ambalo alidai linamuuma.
“ Naumia wanangu sijui wanaishi vipi, huyu niliyembeba ni mlemavu, hamtaki amekuwa akininanga kwa maneno mengi sana, mimi nimetoka naye mbali nilibadili dini kwa ajili yake, leo hii ananitesa, hanitaki anipe haki yangu ili niishi mwenyewe,” alisema Hawa.

Kwa upande wa mbunge hiyo Ameir alidai kwamba kesi yao ipo kwenye Mahakama ya Kadhi, akidai kwamba mwanamke huyo amekuwa akimdhalilisha kwa kupitia mtoto huyo mlemavu ambaye alikiri ni mwanaye.
“ Huyu ni mwanangu sishindwi kumhudumia, lakini sitaki fedha ziende kwa huyu mwanamke atazitumia kwa mambo yake mengine, mimi nilimpeleka kwa mama yake mzazi akakae naye huko lakini yeye hataki,” alisema Mbunge Ameir.

Akizungumzia tukio hilo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gosbert Blandes alisema ni tukio ambalo limewafedhehesha kwa kuwa hawakulitarajia.
“Tulivamiwa na wanawake kama wanne na wanaume wawili nafikiri mmoja alikuwa ni mpiga picha, mwanamke mmoja akawa anapiga kelele, tulitaharuki kwa sababu maaskofu walikuwa wameanza kutoa maoni yao,” alisema.

Alisema kwamba waliomba msaada kwa maofisa usalama wa ukumbi na walifika na kuwachukua wahusika hao, kisha kuwapeleka polisi kwa hatua zaidi.


mahusiano: Ney asema ni vigumu kuingia kwenye majukumu ya ndoa kwa sasa.

nimechota kutoka mwananchi..

Huenda ile dhana kwamba wasanii wanaogopa kuoa kwa sababu wanahisi watashuka chati, inaweza ikawa na ukweli ndani yake, kwa mujibu wa msanii nyota wa hiphop nchini, Ney wa Mitego.

Awali nyota wa muziki nchini na barani Afrika, Diamond Platnumz aliwahi kunukuliwa mwaka jana akisema kuwa hawezi kumuoa mchumba wake wa zamani, Wema Sepetu, kauli ambayo baadaye aliikanusha.

Lakini Ney wa Mitego, ambaye kwa sasa ana mtoto wa kiume aliyempata kwa mchumba wake, Siwema Oktoba mwaka jana, ameamua kufunguka akieleza bayana kuwa hana mpango wa kuoa kwa sasa mpaka akamilishe baadhi ya mambo.

“Sijasema kwamba siwezi kuoa, ila kwa sasa siwezi kulizungumzia suala hilo. Kuna vitu nakamilisha na vikiwa tayari watu wote watajua,” alisema rapa huyo. 

“Ni kweli kwamba Siwema ni mchumba wangu ninayempenda sana na nashkuru amenizalia mtoto ila mipango yetu ni baadaye.”

Alipoulizwa kuhusu idadi ya watoto alionao na iwapo ana mpango wa kumhalalisha Siwema au mwanamke mwingine kati ya watatu aliozaa nao, Ney alisema:

“Nina watoto wengi, ila kifupi nitakwambia kwamba ninao watatu na kati ya hawa kila mmoja ana mama yake. Sasa siwezi kulisemea hili moja kwa moja. Maisha ni duara hujui wapi utagota, lakini niseme tu kwamba nampenda sana Siwema.”

Ney wa Mitego, ambaye anasema anamiliki nyumba yenye thamani ya Sh180 milioni, alisisitiza kuwa bado hajamaliza baadhi ya mambo yake katika muziki, hivyo ni vigumu kuingia kwenye majukumu ya ndoa kwa sasa.

Hata hivyo picha alizozitupia katika mitandao wiki hii, zinamwonyesha akiwa amevaa pete inayoonekana kuwa ya ndoa, lakini alipoulizwa alikuwa na jibu jingine.


“Hahaahaaa pete hii naivaa huu mwaka wa sita sasa, tangu nilipopewa zawadi na rafiki yangu anayeishi nje ya nchi. Hii ni zawadi na lazima niitunze kwa kuwa kwanza ninaipenda,” alisema.