Tuesday, January 20, 2015

Amri 10 za kuweka mpangilio mahali unapoishi

1. Weka vinavyofanana pamoja. Hii itasaidia kuleta mantiki na hivyo urahisi wa kuona vitu vilipo. Unaporundika eneo lote linakuwa kama uchafu na vurugu na kukosa mvuto

2. Fikiri kabla hujanunua kitu. Kununua kwa mhemko ni kifo cha mpangilio wowote ule, chochote unachonunua kinahitaji pa kuwekwa. Panga kabla ya kununua: Kitakaa wapi? Nina nafasi ya kukiweka? Kama majibu ni sijui ni na hapana achana nacho (nyongeza ni kuwa utakuwa umesevu hala yako).

3. Kila kitu kina makazi. Kiweke eneo lake.

4. Heshimu kumbukumbu zako – halafu ziage. Ha ha ha haaaa, sikuambii ulitose gauni lako la harusi, kumbukumbu nyingine zinagusa mno kwahivyo zinahitaji eneo kwenye nyumba yako maisha. Lakini CD sijui muvi fulani, inaweza ikawa ni muda wa kufikiri mara mbili ni kumbukumbu gani unayotaka kubaki nayo maisha.

5. Weka nguo mbali. Lakini mmmmh! Najua, najua unaguna, sio kila mahali kila chumba nguo zinazunguka watu. Hapa namaanisha safi ziwe kwake, chafu ziwe kwake, zinazofuliwa ziwe kwake itafanya maisha yako yawe mazuri zaidi kwa muda mrefu. 

6. Tumia vikontena vilivyopo kwa lengo lingine pindi vimalizapo lengo moja. Nimeona watu wanaotumia vi can vilivyoisha biskuti ama chokoleti kwa ajili ya kuhifadhia vitu kama hereni na vipodozi.

7. Weka kituo cha amri . Manake ni kwamba kituo hiki ndicho kinachokaa vile vitu kama funguo, mifuko, yani vile vitu ambavyo vinatumika mara kwa mara kwenye pilika za kila siku na unapovihitaji usipoviona fasta kichwa kinavurugika. Hutakuwa na haja ya kutafuta ama kuanza kuuliza kama utakuwa na kituo cha amri nyumbani kwako.

8. Weka ratiba ya siku. Na hakikisha unaifuata. Ratiba ni uti wa mgongo wa mipangilio. Kama kila siku unatenga muda wa kurudisha vitu pale vinapotakiwa kuwa, faili ripoti za watoto na karatasi zako muhimu, tandika kitanda, nyumba yako itakushukuru. Kumalizia siku na nyumba yenye mpangilio ni kweli kuwa unajisikia vizuri ajabu.

9. Anza kidogo kidogo. Kama huna karama ya kuweka vitu kwenye mpangilio anza kidogokidogo na vitu vidogodogo kama vile hicho kituo cha funguo, taratibu utashika kasi na kufika hadi kwenye kabati za nguo. Furahia kimpangilio kidogo unachoanzia ambapo kitakupa stamina ya kusonga mbele.

10. Usichoke. "Kumbuka kuwa wewe ndio msimamizi wa nyumba na vitu vyako. Kama utaiambia akili yako nataka kuishi mahali penye mpangilio, muda si muda haitajisikia kuchoka. Umesongwa? Sawa, chukua mapumziko kidogo.


No comments:

Post a Comment