Saturday, January 24, 2015

Nyumba safi ni ipi?



Naulizwa hili swali mara nyingi. Nyumba safi ni ipi? Na acha nianza kwa kusema kuwa hakuna jibu sahihi!

Kila nyumba ina upekee wake na mahitaji tofauti kuendana na wakaaji.

Kwa mimi najibu kuwa nyumba safi ni ile ambayo hakuna vyombo vinavyoachwa vichafu iwe ni kwenye sinki, karo, beseni, ndoo, popote pale pa kuoshea vyombo kuendana na maisha unayoishi na nguo chafu hazijazagaa kila mahali sakafuni. 

Nina ratiba yangu ya mambo ya kufanya kwa siku kwa wiki na kwa mwezi kufanya mazingira yaonekane safi, maridadi na nadhifu bila kufanya kazi kubwa kwa wakati mmoja.

Kuna usafi wa kufanya kwa kipindi (sio kila siku) kwa mfano ndani ya friji na microwave. Najitahidi kupambana na uchafu palepale unapotokea ikiwa ni pamoja na kupitisha fagio na kushughulikia doa hasa palepale linapotokea. 

Hata kama sipo nyumbani huo ni utaratibu uliopo na unaeleweka kwahivyo sitegemei kuja nikute doa kwa mfano kwenye carpet.

lla ukweli ni kuwa hakuna aliyekamilika. Kwangu mimi nyumba safi ni nyumba nadhifu. Kila kitu kina eneo na kimerudishwa eneo lake mara baada ya kutumika. Haimaanishi kuwa sakafu zinadekiwa tena baada ya chakula cha usiku – hapana sina muda huo kwakweli. 

Tafuta ratiba ambayo itawezekana kwako. Na kama una mwezni au watoto set “house rules” na mshirikishe kila mmoja hapo nyumbani.


Kadri ninavyopata muda nitakuwa nawashirikisha vidondoo vya jinsi ya kusafisha mahali unapoishi.

No comments:

Post a Comment