Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la Utangazaji (BBC) idhaa ya Kiswahili,
Wema aliripoti madai yake kituo cha Polisi Oysterbay akidai kuwa
alimpatia mwanamuziki huyo kiasi hicho kwa makubaliano ya kazi na
kuahidi kumlipa, lakini amekwenda kinyume makubaliano yao.
Muhusika mkuu ambaye ni Wema alitoa maelezo kwamba watu wanamtupia
lawama kutokana na hatua aliyofikia, lakini amedai kuwa amelazimika
kufanya hivyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeingia dhamana na taasisi Focus
Vicoba kuchukua fedha hizo.
“Naona watu wengi wananilaumu kwa kuwa nimemfungulia kesi Diamond,
pasipo kuelewa kama fedha hizo pia hazikua zangu bali ni mkopo ambao
niliingia dhamana katika taasisi ya utoaji mikopo ya Vicoba.
“Kupitia mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia Diamond, ili aweze kuandaa miradi yake tena kwa makubaliano kuwa atazirudisha ili tuweze kufanya marejesho ya mkopo tuliochukua,” alisema Wema.
“Kupitia mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia Diamond, ili aweze kuandaa miradi yake tena kwa makubaliano kuwa atazirudisha ili tuweze kufanya marejesho ya mkopo tuliochukua,” alisema Wema.
Mrembo huyo alieleza muda waliiopeana ahadi ya kurudisha fedha hizo
umepita na Diamond haoneshi dalili ya kuzirejesha wakati wanatakiwa
kuzirudisha kwa wakati .
“Yote haya yasingenikuta, lakini sina jinsi kwani natakiwa kurudisha pesa za watu nimekuwa nikimpigia simu
“Yote haya yasingenikuta, lakini sina jinsi kwani natakiwa kurudisha pesa za watu nimekuwa nikimpigia simu
Diamond hataki kupokea simu zangu,
lakini kama alitaka kunidhulumu ni bora angejiunga mwenyewe na hawa
Vicoba ili apate mkopo na kufanya mambo yake au kama aliona hawezi kwa
kujishtukia basi angetumia ile tovuti yao, angepata kwa urahisi na
hakuna mtu yeyote angejua kama amekopa ila sio kukimbia kulipa deni la
watu,” alisema.
Hata hivyo Diamond ambae kwa sasa yupo nchini Burundi kwa ajili ya ziara
yake kimuziki, tayari ametumiwa taarifa na jeshi la polisi kwa barua ya
wito kufika kituoni pindi atakaporejea nchini, huku mama yake mzazi
akifikishiwa ujumbe huo nyumbani kwake.
Wema ambae alimwekea dhamana, yupo katika kipindi kigumu ambacho
kinaweza kupelekea kufilisiwa mali zake ambazo aliziandikisha wakati wa
kuchukua mkopo huo ili ziweze kufidia deni hilo.
Kwa mujibu wa kiongozi wa taasisi hiyo ambae aligoma kutajwa jina lake
gazetini, alisema kuwa ni kweli Wema alifika katika ofisi zao zilizopo
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ili apewe muongozo lakini alipotakiwa
kufuata taratibu za kiofisi kama wanachama wengine wanavyofanya katika
vikundi, hakukubaliana na utaratibu, hivyo kushauriwa ajiunge kupitia
tovuti .
MTANZANIA ilimtafuta Meneja wa Wema, Martin Kadinda, ambae alieleza
hajui chochote kuhusu kufungulia kwa kesi hiyo, akaomba apewe muda
kumtafuta msanii huyo ili aweze kupata ufafanuzi juu ya suala hilo,
lakini hakueleza nini kilichojiri na kusisitiza asubiriwe.
Gazeti hili halikuishia hapo, lilimsaka Meneja wa Diamond, Babu Tale, ambae alionekana kushtushwa na habari hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote.
Gazeti hili halikuishia hapo, lilimsaka Meneja wa Diamond, Babu Tale, ambae alionekana kushtushwa na habari hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote.
Habari hii ni kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania
No comments:
Post a Comment