Apambana na mamba aliyemla mkewe,Uganda
BBC wanaripoti kuwa:
Miezi minne iliyopita, Demeteriya
Nabire aliliwa na mamba alipokwenda mtoni karibu na makazi yake kuchota maji.
Mnyama huyu alirudi tena baaae katika eneo lilelile na kumkuta mume wa Nabire
anasubiri, tayari kwa kulipa kisasi.
Demeteriya Nabire alikuwa kwenye kingo
za mto akiwa na wanawake wengine kutoka kwenye Kijiji anachoishi, walikuwa
wakichota maji kutoka katika Mto Kyoga nchini Uganda, Mamba alifika na
kumnyaka.alimburuza kisha mwanamama huyu hakuonekana tena.
Mumewe, Mubarak Batambuze, aliingiwa
na hofu sana,Nabire alikuwa mjamzito.hivyo Mubarak hakupoteza mkewe tu bali
kiumbe kilichokuwa tumboni.alijihisi kukosa nguvu, lakini Mwezi uliopita
akasikia kuwa Mamba amerejea.
''Mtu mmoja akaniita 'mubarak nina
habari kwa ajili yako, Mamba aliyemchukua mkeo amerudi, tena'
Mvuvi huyo mwenye umri wa miaka 50
akaelekea mtoni na marafiki zake .''alikuwa mkubwa, na tulijaribu kupambana nae
kwa mawe na fimbo lakini hatukufanikiwa''.alisema.
Hivyo Batambuze alienda nyumbani kwa
muhunzi.
''nikamweleza kuwa napambana na Mamba
ambaye amenichukulia mke wangu na mtoto aliyekuwa tumboni.ninataka sana kulipa
kisasi,kisha nikamwambia anitengenezee silaha ambayo ingeweza kumuua mamba
huyo.
Mtu huyo alitaka nilipe kiasi cha
pauni 3.20 ili atengeneze Mkuki.
Akiwa na mkuki wake mkononi
alielekea kwenye mapambano.
Lakini alipofika kwenye maji, Mamba
alikuwepo eneo hilo, lakini Marafiki wa Batambuze waliingiwa hofu na kumsihi
asimshambulie kwa kuwa alionekana mkubwa sana na angeweza kumla,wakamwambia
kuwa Mkuki huo hautafaa.
Batambuze akasisitiza waendelee
kubaki, ''nilishindwa kumuua mwanzo, alisema, ''sioni tatizo nikifa wakati
namuua Mamba natatumia mkuki huu, na nitahakikisha amekufa''.
Ofisa wa wanyama pori Oswald
Tumanya, amesema kuwa Mamba alikuwa na urefu wa zaidi ya mita nne na uzito wa
kilo 600.
Mubarak Batambuze akimshuhudia mamba
aliyemuua mkewe
''nilikuwa na wasiwasi sana lakini
kilichonisaidia ni Mkuki''alisema Batambuze.
Alifunga kamba kwenye kwenye mkuki
kwenye sehemu iliyotengenezwa mithili ya kisu kikali, ''niliweka silaha yangu
eneo Mamba alipo huku marafiki zangu wakinisaidia kurusha mawe na kumchapa
mamba mgongoni kwake wakitumia fimbo, Alijaribu kunyanyua mdomo wake juu ili
anishambulie.''
alishikwa na hasira sana, kisha
kulikuwa na hofu sana katika eneo hilo, lakini nilikuwa na nia, na sikuhofu
kufa, nilitaka kumuua hivyo nilirusha silaha yangu alipo mamba kisha nikavuta
kamba. Mamba alianza kuwa matatani''.
Ilichukua saa moja na nusu mwa
Batambuze na marafiki zake,wakipambana na Mamba, hatimaye alikufa.
Wakiwa wamechoka walirejea kijijini
kwao ''kulikuwa na mshtuko mkubwa, kilichomshangaza kila mtu ni ukubwa wa
Mamba, hakuwa mamba wa kawaida, alikuwa mkubwa sana .Na Watu wakatuita mimi na
marafiki zangu mashujaa''alisema.
No comments:
Post a Comment