"Uchunguzi wa awali
umebaini marehemu alifariki baada ya kubakwa, kunyongwa na kutupwa
porini na mtuhumiwa aitwaye Ramadhani Omari (28), mkazi wa Maweni,"
alisema.
Aliongeza kuwa,
uchunguzi huo pia umebaini mbinu ambayo ilitumiwa na mtuhumiwa ni
kumvizia marehemu akiwa anachuma matunda hivyo alimkamata kwa nguvu na
kumfanyia unyama huo.
Kamanda Sedoyeka
alisema licha ya marehemu kupiga kelele na wananchi kukimbilia eneo hilo
ili kumwokoa, walipofika walikuta tayari amefariki na mtuhumiwa
kakimbia lakini alikamatwa baada ya saa mbili.
"Jeshi la Polisi
linamshikilia mtuhumiwa kwa upelelezi zaidi na baada ya kukamilika,
atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili, mwili wa marehemu
ulifanyiwa uchunguzi na daktari na baadaye kukabidhiwa ndugu zake,"
alisema.
No comments:
Post a Comment