Ngazi
ni eneo muhimu la nyumba ambalo linawasaidia wakaaji wa nyumba hiyo kwenda
maeneo mengine ndani ya nyumba husika, hasa pale nyumba inapokuwa ni ya
ghorofa. Mbali na hilo, muundo wa ngazi pia unahusika kwenye kupendezesha
nyumba.
Mhandisi
David Sembuyagi anasema kuna aina nyingi za ngazi. Ngazi ni gharama na pia ni
ngumu kuzijenga. Kwahivyo ni muhimu ukafahamu hayo wakati unapochagua muundo wa
ngazi. Kama upo kwenye mchakato wa kujenga nyumba itakayohusisha ngazi basi
makala haya yatakusaidia kuamua muundo wa ngazi ambao utakufaa. Dondoo hizi
zitakufanya uje na uamuzi wenye uzito:
1.
Bajeti
Miundo
mbalimbali ya ngazi ina gharama tofauti. Bajeti yako itaamua mtindo, muundo na
malighafi ya kutengenezea ngazi zako.
2.
Nafasi
Nafasi
iliyopo ndani ya nyumba inayohusika kwa ajili ya kuweka ngazi inatakiwa
kuangaliwa kwani ndio inaamua muundo wa ngazi utakaofaa. Kama nyumba ni ndogo,
ni vyema kuchagua muundo wa ngazi ambao hautachukua nafasi kubwa. Na kwa upande
mwingine kama nafasi ni kubwa basi unaweza kuchagua ngazi ya muundo wa kuvutia
na kubwa, au pia unaweza unaweka mbili upande huu na ule.
3.
Usalama
Kwenye
usalama wa ngazi ni lazima kuzingatia mlalo na mwinuko wa hatua usiwe mkali, na
pia kizuizi cha pembeni ni muhimu hasa ngazi inapokuwa ni ndefu na ni lazima
kwa ngazi ya kupanda ghorofani. Usalama
wa ngazi pia uzingatie uwepo wa watoto na wazee ndani ya nyumba. Upana uwe wa
kutosha kuweza kupishana watu wawili,
anayeshuka na anayepanda.
4.
Malighafi
Malighafi
kwa ajili ya kutengenezea ngazi zipo za aina kadhaa. Mwenye nyumba anaweza
kuchagua ngazi ya malighafi ya chuma, mbao au tofali kwa ajili ya nyumba za
kisasa. Kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa malighafi zinazochaguliwa zitaendana
na muonekano mzima wa nyumba, ubora uzingatiwe kwani malidhafi dhaifu hazifai
kwa kutengenezea ngazi.
Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755200023
No comments:
Post a Comment