Tuesday, March 8, 2016

Milango ya mbao ngumu ndio bora zaidi kwa nyumba yako

Kwa uimara na viwango, milango ya mbao inaipa nyumba muonekano wa mvuto wa kipekee.
Mukhangu Noah ambaye ni fundi milango anasema kuwa kati ya milango inayotengenezwa kwa malighafi mbalimbali ni muhimu kuchagua milango ya mbao ya mkongo, mninga au mnazi ukilinganisha na
mingine yote.

Milango ya mninga na mkongo inaingia kwenye kundi la milango ya mbao ngumu. Tofauti yake ni kwamba mkongo una madoa doa mengi. Pia ni mgumu mno sio rahisi kupinda au kutobolewa na mchwa kwa hivyo wenye kujenga nyumba za kisasa wengi wanapendelea kuutumia mkongo kwenye fremu huku mninga ambao nao ni mbao ngumu lakini ukiwa wa kuvutia zaidi kimuonekano ndio unaotumika kwenye mlango wenyewe hasa kwa watu wa bara, wakati wale wa pwani wakibobea kwenye milango ya mbao ya mnazi.

Mionekano wa aina hizi tatu za mbao za milango moja kwa moja inapendezesha nyumba kwa ajili ni mionekano ya asili. Kimsingi namna nyumba yako inavyoonekana inakusemea wewe ulivyo na ndio maana kila mmoja anatamani kuwa na nyumba yenye muonekano wa kuvutia kwa kuwa na fenicha, vitupio, mapambo, mpangilio na rangi nzuri za ukutani za kuvutia. Kwahivyo kitu kama milango pia ikitengenezwa kwa umakini inaipa nyumba mvuto.

Noah anasema, ndani ya nyumba milango ya mninga au mnazi inaleta hali nzuri ya kimuonekano kuliko milango ya aina nyingine yoyote ile. Hizi ni faida kuu za kuwa na milango ya mbao za mninga:

·         Inatunza na kuweka hadhi ya nyumba yako katika kiwango kilekile ikiwa mpya hata itakapozeeka.
·         Inadumu muda mrefu sana kwani haishambuluwi na wadudu kutokana na ugumu wa mbao yake. Inaweza kudumu hadi miaka 60.
·         Ni rahisi kufanyia marekebisho bila mbao ya awali kuharibika.
·         Haina gharama kubwa ya utunzaji, mkono mpya wa rangi, polishi au mati unatosha bila kupauka au kuharibiwa.
·         Ina toa wigo mpana wa urembo wa kuupendezesha kwa mfano kuweka paneli na kadhalika. Mbao ya mninga haina mwisho wa ubunifu wa urembo.
·         Ni mgumu, mzito na unahimili msukumo wowote wa nyumba na sio rahisi kupinda. Vivyo hivyo kwa mnazi, mbao yake  ni ngumu sana na haipindi ikiwa imeshakauka.
·         Inahakikisha kiwango kikubwa cha usalama dhidi ya mwizi
·         Inaipa nyumba mguso wa asili


Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Piga/whatsapp 0755 200023

No comments:

Post a Comment