Zamani
ilikuwa kawaida kwa familia kuwa na nyumba kubwa ya kulala na nyingine dogo
pembeni ya jiko. Uwepo wa nyumba za kisasa zenye chumba cha jiko ndani yake unapelekea
kupotea kwa dhana ya kuwa na jiko la nje.
Iwe
unajenga nyumba mpya au unaifanyia marekebisho hiyo ya zamani, kwenye makala
haya nitakuonyesha faida kadhaa za
kuwa na jiko la nje:
1. Linakufaa
sana wakati wa sherehe nyumbani
Faida kuu ya kwanza ya kuwa na jiko
la nje ni kwamba linakufaa sana wakati wa sherehe nyumbani. Chakula kinapokuwa
kinaandaliwa huku ukiwa na wageni wako bustanini utashangaa ni kwa namna gani
unavyoweza kumburudisha kila mmoja bila ya kuwa na sababu ya kuingia kwenye
nyumba kubwa. Kumbuka hii ni nzuri kwani nyumba inabaki safi na kwenye mpangilio
kama ilivyokuwa awali hivyo kuepuka kero ya kusafisha baada ya sherehe.
Pia wakati wa burudani watu
wanapenda kuwa karibu na jiko, kuona ni nini kinachopikwa au kuchomwa. Ni sawa
na hulka ile ile ya wengi kupendelea kukaa kwenye mabaa. Unachotakiwa kufanya
tu ni kuwa na viti vya kutosha wageni wako, mwanga na mziki!
2. Linaongeza
thamani ya nyumba
Unapokuwa
na jiko la nje lililokamilika kwa kuwa na vifaa vyote vya msingi utagundua ni
kwa namna gani hata msaidizi wako wa nyumbani anaweza kulitumia kuandaa chakula
pale ambapo haupo nyumbani na pengine hutaki au humuamini kwa matumizi ya jiko
la ndani.
3. Linarahisisha
mapishi
Kuna wakati unahitaji mapishi ya
aina mbalimbali labda ni chomachoma, kukaanga samaki na vyakula vingine vya
baharini, ambapo mapishi haya yanazalisha harufu kali. Unapokuwa na jiko la nje
unahamishia mapishi ya namna hiyo kule.
Pia jiko la nje linasaidia kuepusha
uzalishaji wa joto ndani kama tujuavyo kupika kunazalisha joto. Fahamu kuwa
jiko la nje kama lile la ndani linaweza kuwa na vifaa vyote muhimu jikoni.
4.
Linaongeza ukubwa wa makazi
Unapokuwa na jiko la nje unajikuta
kuwa kama familia mnatumia zaidi eneo la nje ya nyumba kwa matukio mbalimbali
kama vile ya siku ya kuzaliwa, sikukuu au hata kufurahia mandhari ya nje tu
badala ya kufanyia kila tukio ndani.
5. Linahamasisha
mapishi ya vyakula bora
Sio tu
kwamba vyakula vya mapishi ya kuchoma vina ladha nzuri, ni kwamba mapishi ya
namna hii ni mazuri pia kwa afya bora kwani wakati wa kuchoma mafuta mengi
yanaondoka kwenye nyama kwahivyo kile kinacholiwa kinakuwa kina kiasi kidogo
sana cha mafuta. Kama una mkakati wa kupunguza unene bila shaka mapishi ya
kuchoma ndio mazuri zaidi kwako.
Choma
mwenyewe nyama nyumbani badala ya kuzifuata kwenye mabaa, siku zote chakula cha
kuandaa mwenyewe kinaaminika kuliko cha sehemu za biashara.
Kwa ushauri piga 0755 200023
No comments:
Post a Comment