Kaunta
ya jiko lako inatakiwa kuwa eneo muhimu sana la kuzingatia katika harakati za
kuwa na jiko linalopendeza, sio tu kwa ajili ya muonekano wake bali pia kwa
ajili ya gharama za kununua na pia kuisimika. Kama tujuavyo wenye kujenga
nyumba za kisasa wengi wanapendelea kuweka kaunta ya marble ambapo gharama yake
si ndogo. Unapokuwa umechagua kuweka malighafi hii ambayo ni jiwe la asili basi
kinachofuata ni
kuangalia uweke la rangi gani.
Marble
zinakuja kwa michoro na rangi nyingi mno kwahivyo kuchagua iliyo sahihi inaweza
kuwa changamoto kubwa. Rangi utakayochagua
itakupa mwelekeo wa rangi za vifaa vingine utakavyonunua kwa ajili ya jikoni
huku ukijua kuwa ni rahisi kuvibadilisha kuliko kubadilisha rangi ya marble
kwani ni gharama kuondoa kaunta moja na kusimika ya rangi nyingine. Ni kazi
ndogo tu kupaka makabati rangi nyingine au kubadili mikono ya makabati au hata
kubadilisha microwave nyeupe na kuweka ya silva au nyeusi.
Unapochagua
rangi ya marble kwa ajili ya kaunta ya jiko, anza kwa kuchagua rangi ya jiwe
ambalo unaipenda. Chagua marble ambayo unaona kuwa ina mvuto, bila kujali kama
inaendana na rangi ya makabati au ukuta. Mwishoni utaridhika zaidi kwa kuchagua
kitu ambacho unakipenda badala ya kuchagua rangi au mtindo ambao unadhani
utaoana na vitu vingine.
Wakati wa kuchagua rangi ya kaunta,
kumbuka kuwa rangi nzito kama vile nyekundu au nyeusi zina muonekano wa ukisasa
lakini zinaweza kufanya chumba kipooze. Marble za rangi hizi hazina michoro
inayoonekana kwahivyo ni kawaida kupitwa na wakati mapema zaidi kwani inakuwa
haina ushirikiano na rangi nyingine jikoni. Ni bora ukapeleka rangi hizi kwenye
vifaa vya kuhamishika. Kaunta yenye michoro inayoonekana wazi ni rahisi
kuoanisha na rangi nyingine bila kusababisha jiko kuonekana kama limezidiwa
rangi.
Unapochagua rangi ya marble ya
kutengenezea kaunta ya jiko zaidi ya kuzingatia rangi ya kuta na sakafu pia ni
vyema kufahamu kiasi cha mwanga kinachoingia jikoni kutokana na upande dirisha
lililoko.
Ukiwa
unachagua rangi ya kaunta yako angalia ambayo itafanya vyema ukutani pia.
Kanuni namba moja ya rangi ni kwamba weka pamoja rangi zilizo kwenye familia moja
kwani zinasababisha ujirani ambao unaleta muonekano wa kuvutia. Kwasababu
marble ni jiwe la asili ni kawaida kuwa na rangi kadhaa ndani yake. Ni vyema
kuzishirikisha rangi hizo kwenye maneneo mengine ya jiko iwe ni ukutani au
sakafuni.
Vilevile
ni vyema kufahamu kuwa rangi inavyozidi kuwa nzito/nyeusi, ndivyo na chumba
kinavyozidi kuwa kidogo na inavyozidi kuwa nyepesi/mwanga ndivyo chumba
kinavyozidi kuonekana kikubwa.
Unapochagua
rangi ya kaunta uwe umeshakusanya mawazo ya rangi za maeneo mengine pia, kama
vile makabati, sakafu, kuta, dari na mwanga wa taa.
Ushauri 0755 200023
No comments:
Post a Comment