Hata kama hupendi kutandika kitanda
lakini hakuna ubishi kuwa unapenda muonekano wake kikiwa kimetandikwa, na kwa
namna yoyote ile utapenda kitanda kiwe kimetandikwa pale mtu mwingine
anapoingia chumbani.
Kitanda kilichotandikwa vizuri ni
kile chenye muonekano wa kuvutia, kikiwa hakina makorokoro mengi na pia ni
rahisi kutandua wakati unapohitaji kulala. Ifuatayo ni mitindo mitano niliyokuandalia ya kutandika kitanda. Nina imani baada ya kusoma makala hii utahamasika kuanza kutandika kitanda chako kwa kutumia mtindo mmjowapo kati ya hii.
rahisi kutandua wakati unapohitaji kulala. Ifuatayo ni mitindo mitano niliyokuandalia ya kutandika kitanda. Nina imani baada ya kusoma makala hii utahamasika kuanza kutandika kitanda chako kwa kutumia mtindo mmjowapo kati ya hii.
Kunjia tandiko la juu kuanzia pale mito inapoishia
Tandiko la juu ya kitanda ni lile la
mwisho wakati wa kutandika. Tandiko hili linaweza kuwa ni blanketi au duveti.
Kutandika kwa kukunjia tandiko la juu pale mito inapoishia ni kwamba
huenda una mito mizuri ambayo ungependa
ionekane. Kama ndivyo, unachotakiwa
kufanya ni kuipanga kuanzia kichwani kushuka chini hadi itakapoishia kwa idadi
uliyo nayo. Eneo lote hilo la mito liache wazi na anza kukunjia tandiko lako la
juu pale mito hiyo inapoishia. Kumbuka
kuwa usitandaze mito kwa jinsi ambayo itafunika ubao wa kichwani kwani ubao huu
ndio fahari ya kitanda na pia unautumia kuegemea pale unapokaa kitandani ukiwa
unasoma kitabu.
Kunjia tandiko la juu eneo la miguuni
Huenda unaona kama vile tandiko la
juu linakaba au kuzuia mito isonekane vizuri au labda umetandika shuka nzuri
ambazo nazo ungependa zionekane. Kama ndivyo basi, kunjia tandiko lako la juu
eneo la chini kabisa karibu na miguuni na ndipo utaziwezesha shuka kuonekana
pia. Muonekano huu ni rahisi na unavutia kwani kipande cha tandiko la juu ambacho
huwa ni rangi tofauti na ile ya shuka ndicho kinachoonekana kwa sehemu ndogo tu
mwishoni mwa kitanda huku kwingine kukiachia mito na shuka kupata wasaa wa
kuonekana.
Utepe wa kitandani
Muonekano wa utandikaji kitanda kwa
kushirikisha utepe wa kitandani unakaribia kufanana na wa kukunjia tandiko la
juu miguuni ila tofauti yake ni kwamba kunakuwa na ongezeko la huo utepe.
Huenda umesafiri maeneo mbalimbali na ukakutana na vitambaa ambavyo vina rangi
na michoro ya kipekee na ukavipenda. Badala ya kuvinunua na kuvifungia kabatini,
vitumie kwenye kuremba kitanda chako baada ya kukitandika. Kwa namna hii utakifurahia
kila siku na kitadumu muda mrefu sana kwani hakitumiki/hakilaliwi zaidi ya
kutandikwa mwishoni baada ya kumaliza kutandika kitanda na kuondolewa wakati wa
kulala.
Tandiko la juu kufunika kote na kuchomekewa
Kwa ujumla huu ndio mtindo rahisi
zaidi wa kutandika kitanda kwa kusambaza tandiko la juu kuzunguka kitanda
kizima huku ukilichomekea kila upande. Unahakikisha limeonyooka kila mahali halafu
unatupia mito juu unaondoka zako. Huu ni utandikaji mwepesi sana, huhitaji
kukunja popote kwahivyo hupotezi muda wa kujua kama mkunjo umenyooka ama laa.
Tandiko la juu kufunika kote bila kuchomekewa
Huenda michoro ya duveti lako ni
mizuri sana na ungependa yote ionekane kwa ukamilifu wake au labda fremu ya
kitanda chako si nzuri kivile, pengine imeshakwaruzika sana unasubiria ukikaa
vizuri uipake rangi upya. Ikiwa ndivyo basi hutataka ionekane sana badala yake utapendelea
ukishatandika uache duveti au blanketi likining’inia ili lisaidie kuificha. Huu
pia ni utandikaji mzuri, unachotakiwa kufanya ni kusambaza tandiko la juu kwa
uwiano huku ukihakikisha kuwa kipande kinachoning’inia kina urefu sawa kila
upande, halafu unatupia mito ya kulalia
pamoja na ya mapambo juu yake umemaliza.
Kwa maoni yangu ni kwamba kila
mtindo wa utandikaji unapendwa zaidi na mtu fulani, chagua unaokufaa.
Karibu kwa ushauri simu 0755 200023
No comments:
Post a Comment