Unapohitaji
viti vya meza ya chakula kuna njia mbili, ya kwanza ni kutengenezesha kwa
mafundi na ya pili ni kununua vilivyo tayari ambapo mara nyingi hivi vinauzwa
pamoja na meza yake.
Moja
ya jambo muhimu unalotakiwa kufahamu ni kama unahitaji viti vilivyoshonewa
vitambaa na
sponji au visivyokuwa na vitambaa na sponji. Yani kuna viti ambavyo
kama ni mbao ni mbao yenyewe tu na kuna vile ambavyo kama ni vya mbao ni mbao
pamoja na sponji na kitambaa kilichofunika hilo sponji.. Ni ukweli kuwa viti aina
hii yenye vitambaa na sponji vinaonekana kuwa na mvuto na pia kuvikalia inakuwa
burudani zaidi. Cha muhimu ni kuzingatia kuwa familia yako ina watu wa umri
gani, kwa mfano meza ambayo inatumiwa na familia yenye watoto wadogo, vitambaa
vya viti ni rahisi kuchafuliwa na kuharibiwa ndani ya kipindi kifupi. Kwahivyo
unapaswa kujiuliza je, utaweza hiyo kazi ya kuvisafisha mara kwa mara? Kuna viti
ambavyo havijashonewa sponji lakini vinakuwa na mito pembeni ambayo ni rahisi kubadilisha
foronya na kusafisha wakati huohuo ukizingatia pia rangi ya kitambaa cha mito.
Endapo una familia changa pengine hivi vya aina hii ndio vinakufaa zaidi ambapo
utavibadilisha miaka ya mbeleni watoto wanavyokua wamekua wakubwa.
Jambo
lingine la kuzingatia ni urefu wa viti vyako vya meza ya chakula. Huwa kuna
tofauti ya urefu kwahivyo ni vyema kama unanunua meza kwingine na viti kwingine
ujue kwamba viti unavyotaka kununua vinatosha kwenye meza uliyonayo. Pia kama
viti vya meza ya chakula unavyotaka kununua vina mikono hakikisha kuwa haiko
chini sana au juu sana kiasi cha kukuzuia kuwa karibu na meza pale unapokuwa
umevikalia.
Jambo
ambalo wengi wanaohitaji viti au walishapata tayari, hawajajua ni kwamba
unaweza kuchanganya viti vya meza ya chakula toka kwenye vyanzo tofauti. Kwa
mfano, viti vya mikono vinapendeza vikiwa viwili ambapo kila kimoja kinakuwa
kwenye ule upande mwembamba wa meza. Viti hivi huwa vinafanya meza iwe ya
kifahari kama navyo ni vya kifahari. Kwa maana hiyo kama meza yako ya chakula
ni ya viti 6 kwa mfano, unaweza kununua hivi 4 vya gharama nafuu na vile viwili
vyenye mikono ukanunua vya kifahari. Kuongeza hela kidogo zaidi ili kununua
hivi viti viwili vitaifanya meza yote kuonekana ya daraja la juu!
Natumai
dondoo hizi zitakusaidia wewe uliyeko kwenye mchakato wa kujipatia viti vya
meza ya chakula.
Kwa ushauri njoo 0755200023
No comments:
Post a Comment