Friday, February 13, 2015

Madirisha yako ungependa kuyavalisha curtains au blinds? Fahamu faida na hasara zake


Teknolojia imeshika kasi na hivyo kuwezesha viwanda kuwa na suluhisho mbalimbali kwa mambo mengi. Hata kwa kuvalisha madirisha vilevile, unaweza ukachanganyikiwa uweke nini hasa kama uko kwenye finishing ya nyumba yako na hivyo umeanza kufikiria kuipamba. Kwa mfano chumba hiki niweke pazia ama blinds?
Dondoo hizi zitakupa kwa uchache faida na hasara ya kila moja, halafu utaweza kuamua mwenyewe.

Wengi watakuambia na ni ukweli kuwa pazia ni rahisi kusafisha. Fikiria kwa mfano unaishi maeneo yenye vumbi na umeweka blinds utakuwa na kazi ya kuzisafisha kila siku laa watu wa nyumbani kwako wahataisha kuugua mafua . Kusafisha blinds si kazi ya kitoto ni kazi kubwa na inayochukua muda mwingi.

dirisha lililovalishwa blinds
Kama dirisha ni la juu ghorofani na liko wazi, na upepo ni mkali blinds zinaweza kungoka moja moja wakati kwa pazia sio rahisi.

Blinds ama pazia itategemea ni chumba gani, kwa mfano blinds zinazuia mwanga kabisa kwahivyo kama ni bedroom zinabembelezea usingizi.

Pazia zinaongeza décor ya chumba kuliko blinds, kwa hivyo ukicheza na rangi na maua yake zinasaidia kubadili muonekano.


Kwa pazia mara nyingine unaweza kuweka nzito na nyepesi kwenye dirisha moja, wakati kuna watu hawataki kuvalisha sana madirisha kwa hivyo kwao blinds zinawafaa zaidi. 

Na mwisho ni kuwa kibongobongo wengi wanaweka blinds ofsini kuliko nyumbani, labda kuna sababu ya ziada.

No comments:

Post a Comment