Ndugu wa Emmanuel Mpira (katikati) wakimfariji katika nyumba ya jirani
jana, baada ya kupoteza ndugu zake sita walioteketea kwa moto usiku wa
kuamkia juzi Jumamosi, Kipunguni Dar es Salaam.
Mpilla alipoteza ndugu hao sita,
akiwamo mama na baba yake, kaka yake, watoto wake wawili na mjomba wake katika
tukio ya nyumba kuungua moto lililotokea usiku wa kuamkia Februari 7, Kipunguni
A, Dar es Salaam.
Familia ya kijana Emmanuel Mpilla (27),
aliyepoteza ndugu sita katika ajali ya moto, imepanga kumpa tiba ya
kisaikolojia ili kuirudisha akili yake katika hali ya kawaida.
Mpilla alipoteza ndugu hao sita,
akiwamo mama na baba yake, kaka yake, watoto wake wawili na mjomba wake katika
tukio ya nyumba kuungua moto lililotokea usiku wa kuamkia Februari 7, Kipunguni
A, Dar es Salaam.
Tangu kutokea kwa msiba huo, Mpilla
hakutaka kuzungumza lolote, hali inayoonyesha ameathirika kisaikolojia.
Akizungumza kwa niaba ya familia,
baba mkubwa wa Emmanuel, Merikioli Mpilla alisema uamuzi wa kumpa tiba ya
kisaikolojia kijana huyo ulifikiwa katika kikao cha wanandugu kilichofanyika
jana.
“Kuna mambo mengi ya kifamilia,
tulipaswa tuyajadili, lakini kwa kifupi yanayomuhusu Emmanuel ndiyo yalitawala
kikao,” alisema Mpilla. CHANZO Mwananchi
|
No comments:
Post a Comment