Waziri wa maliasili na utalii Mh.
Lazaro Nyalandu amefunguka kuhusiana na taarifa zilizoenea kuwa ana uhusiano wa
kimapenzi na muigizaji wa filamu za Kibongo,Aunty Ezekiel na kwamba ujauzito
alionao msanii huyo ni wa kwake.
Aidha
alisema kuwa habari hizo zilitolewa na gazeti moja la hapa nchini kuwa waziri
huyo alitumia mamilioni ya pesa za umma kuponda raha na msanii huyo,wakati huo
alikuwa nchini Marekani kikazi kwa mwaliko wa ubalozi wa nchini humo ambapo
wasanii wawili wa hapa nchini Aunty Ezekiel na Kassim Mganga nao walikuwa
wamealikwa.
‘’Kwa mara ya kwanza nilimuona
msanii huyo kwenye mwaliko huo na baada ya hapo nikaondoka zangu sikuonana naye
tena hata namba yake sina hapo ndipo habari zikaenea kuwa nimetembea naye mara
mimba aliyonayo ni yangu kwa kweli nilishangaa sana,’’alisema Nyalandu.
‘’Naamini taarifa hizo zilizidi kuzungumzwa zaidi na maadui zangu wa kisiasa
baada ya mimi kutangaza nia ya kugombea urais uchaguzi mkuu ujao,’’alisema
Nyalandu.
Hata hivyo Faraja akizungumzia kuhusiana na taarifa hizo alisema kuwa
hazikumshtua hata kidogo kwa maneno kuhusu mumewe amekuwa akiyasikia sana na
ameshayazoea na anampenda sana mumewe.
(By the way Faraja amependeza na kilemba chake)
No comments:
Post a Comment