Wapenzi, zaidi ya kukinga meza isikwaruzwe na vyombo, table mats pia zinapendezesha maandalizi ya meza kwa chakula. Kuzinunua pamoja na bidhaa nyingine nyingi tembelea link ya vinavyouzwa hapo juu. Asante
Wednesday, March 30, 2016
Tuesday, March 29, 2016
Kanuni 10 za mpangilio wa sebule
Iwe ni chumba kitupu yaani sebule
mpya au ni ya zamani lakini unataka muonekano mwingine, kupanga fenicha
sebuleni inaweza kuwa ni changamoto. Unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua hizi
zenye kanuni za mantiki na ndipo utagundua kwamba kumbe mpangilio huo ni jambo
rahisi tu.
Chagua eneo la kivutio cha chumba
Kamwe usidharau nguvu ya eneo macho
yanapoelekea mara wewe au mgeni wako aingiapo sebuleni. Kuna wakati eneo hili
linajitengeneza lenyewe kwa mfano eneo lenye dirisha kubwa au usanifu mwingine
wowote uliofanyika wakati wa ujenzi. Vinginevyo unaweza kulitengeneza kwa mfano
eneo ambalo luninga na miziki itakaa. Popote pale penye eneo hili la kivutio
ndipo unatakiwa upange fenicha kupazunguka.
Usigusishe fenicha na ukuta
Ukubwa wa chumba ndio unaamua ni
eneo kiasi gani libaki ukutani bila kugusana na fenicha, ingawa hata kwenye
sebule ndogo kabisa unapaswa kuacha
Monday, March 28, 2016
Jinsi ya kutumia rangi ya kijivu kupendezesha nyumba yako
Kwa
wengi tumezoea kuona rangi ya kijivu ikiwa imepakwa kwenye maeneo kama kuta za
viwandani, mahospitalini, shuleni na zile sehemu nyingi ambazo kuzipendezesha
sio muhimu. Wengi hawafikirii kuwa rangi hii inaweza kupambwa nyumbani na
ikavutia sana. Kijivu mara nyingi inaendana na mazingira na kuna njia nyingi unazoweza
ukaitumia kupendezesha nyumba bila kuzidisha au kuigeuza kama eneo lililofifia.
Vilevile kijivu
Mambo ya kuzingatia unaponunua shuka
Shuka
zinachukua nafasi kubwa ya kuwa kivutio cha kitanda. Unapoamua kuzinunua kuna
mambo kadhaa ya kuzingatia. Mara nyingi wanunuzi wanaangalia rangi, michoro,
ukubwa na bei. Hata hivyo vitu hivi
pekee havitoshi kuthibitisha ubora wa shuka hizo unazotaka kununua.
Kuchagua
kitambaa cha shuka chenye ubora wa hali ya juu ndio jambo muhimu zaidi. Kwa
kuzingatia hili zifuatazo ni
Saturday, March 26, 2016
HERI YA PASAKA WAPENZI!
Nimetumia hii picha ya taa ya mezani kukutakia heri ya pasaka kwa ajili nataka tujifunze jambo. Tunaponunua taa za mezani tuangalie muundo na sanaa zilizobeba. Kwa mfano hii yenye kitako cha jogoo, bila shaka itamvutia yeyote atakayefika nyumbani kwako. Sikukuu njema kwako!
Tuesday, March 22, 2016
Faida za kumhusisha mtaalam kufremu picha unazotaka kutundika ukutani
Huenda
ndio umetoka fungate na umepokea picha zako za harusi, kwahivyo wewe na mume
wako mnaanza kufikiria na kuchambua ambazo mngependa kukuza na kutundika
ukutani. Au labda umepata mtoto na ni wakati wa kumuongeza kwenye hazina ya
picha za familia ulizotundika ukutani. Vyovyote vile, kufremu picha ni sanaa
inayohitaji msanii anayeijua vizuri kazi hiyo.
Fremu
za picha iwe ni za mbao, plastiki au chuma huwa zinahusisha miundo ambayo picha
inapowekwa ndani yake inaruhusu kuwa kivutio kwa wale wanaoitazama. Fremu yenyewe
tu ni sanaa ambapo utakapochagua ya rangi na muundo sahihi bila shaka
inajisimamia yenyewe kabla hata haijawa na picha ya ndani!
Ingawa
ni ukweli kwamba wapo watu wanaonunua fremu na kuweka picha peke yao, ni vyema
kufahamu kuwa msanii wa picha na fremu ana uzoefu na utaalam wa kujua ni fremu
ipi inafaa kwa picha ipi. Na pia anajua hatua sahihi za kupitia ili kufremu
picha katika ubora unaokubalika. Fikiria thamani ya picha zako kwa
Vigezo vya pazia za chumba cha kulala
Katika
chumba chochote ndani ya nyumba, pazia linachukua sehemu kubwa ya muonekano kwa
kivyo linaweza kuwa kivutio au likaharibu. Habari njema ni kwamba kuna aina
nyingi za mitindo ya mapazia kuendana na kila nyumba na kila gharama. Yapo
mapazia ya kifahari sana na yapo ya gharama nafuu kabisa.
Ili
kupata matokeo unayoyataka, kuna baadhi ya
Monday, March 21, 2016
Zingatia haya unapojiuliza uchague kitambaa cha sofa chenye michoro au cha rangi moja.
Kuna
vingi vya kuchagua pale ambapo unaamua
kupamba nyumba yako kwa jinsi unayotaka wewe. Aina na mitindo mbalimbali ya fenicha, pazia
na mazulia zipo sokoni za kumfaa kila mmoja na vivyo hivyo kwa vitambaa vya
sofa.
Baada
ya kusema hayo, kutokana na kuwa na machaguo mengi inaweza kukuwia vigumu
kuchagua kitambaa sahihi cha sofa kwa ajili ya
Thursday, March 17, 2016
Hatua sahihi za kusafisha meza ya kioo
Meza ya kioo
inaweza kutumika kwenye nyumba yako katika vyumba ambavyo ni pamoja na sebuleni,
chumba cha chakula na hata chumba cha kulala. Wapo wanaozitumia kwenye varanda
na bustanini pia. Bila kujali ni wapi ilipo
meza yako ya kioo, ni wajibu wako kuhakikisha kuwa ipo katika hali nzuri kwa
kuisafisha kwa kina kila inapochafuka.
Meza safi ya
kioo ni pale inapokuwa na kioo kinachong’aa bila uchafu wowote. Vifaa
unavyohitaji kusafishia ni dawa ya kusafishia vioo au maji mepesi kwa maana ya
yasiyo na chumvi kwani huwa chumvichumvi zinaacha alama kwenye kioo, kitambaa
kikavu na gazeti.
Fuata hatua hizi
za jinsi ya kusafisha meza ya kioo ili ionekane kama mpya kila wakati.
1. Hatua ya kwanza katika kusafisha meza ya
kioo ni kuondoa kila kitu juu ya meza. Viweke pembeni na ukishamakiza kusafisha
utavirejesha.
Tuesday, March 15, 2016
Namna ya kuweka mpangilio kwenye kabati la nguo
Kabati
la nguo kwenze chumba cha kulala ni fenicha muhimu. Ingawa linajulikana kama
kabati la nguo, linahifadhia vitu vingi mbali na nguo. Vitu hivyo ni pamoja na
nguo zenyewe, viatu, masanduku, mabegi, vitupio vya urembo na vitu vingine
vingi ndani za chumba chako hicho hivyo kukuwezesha kuwa na mpangilio wa vitu
chumbani.
Kuna
miundo miwili mikuu ya milango ya makabati ya nguo ambayo kutokana nayo unaweza
kuongeza au kupunguza maeneo ya kuhifadhia. Makabati ya nguo yenye milango ya
kufungua kwa kutelezesha ni mazuri pale ambapo chumba ni kidogo na hakuna eneo
kubwa kuruhusu milango ya kufunguka kwa nje.
Wewe mwenye chumba cha hivi utafurahia zaidi kabati lenye milango ya
muundo huu kwani utabakiwa na eneo kubwa chumbani. Kwa muundo wa pili wa makabati
yenye milango ya kufunguka kwa nje yanakupa wigo mpana zaidi wa eneo la
kuhifadhia ndani ya kabati hilo. Cha msingi kwa aina hii ya kabati ni chumba
kuwa na nafasi ya kutosha kuruhusu milango kufunguka kwa nje na bado wewe au
mwingine akaweza kupita na kupishana vizuri
kwa uhuru chumbani.
Kimsingi
pangilia ndani ya kabati lako la nguo kama ifuatavyo:
·
Kwakuwa ndani ya kabati kuna
vyumba/maeneo mbalimbali kama vile mashelfu ya juu na chini, madroo, fimbo ya
kutundikia nguo na kulabu za kuning’iniza vitu. Kwenye shelfu za chini
utahifadhia viatu endapo hujatundika mfuko wa viatu mlangoni mwa kabati hala
pale milango ya kabati inapokuwa ni ile ya kufungua kwa kutelezesha. Tumia
mashelfu ya juu kuhifadhia masanduku, mabegi na vile vitu ambavyo havitumiki
mara kwa mara.
·
Jitahidi kutumia henga zinazofanana
kwenye nguo zote ulizotundika. Lengo kuu ni matumizi sahihi ya nafasi na kufanya
mpangilio uvutie.
·
Kama hazipo, weka kulabu (hooks)
kwenye milango ya kabati kwa ajili ya kutundika mikanda, kofia, tai, skafu na
mikoba. Hii ni kwa yale makabati yenye milango ya kufunguka kwa nje.
·
Panga nguo ndani ya kabati kwa
makundi: Kundi la blauzi, jaketi, sweta, makoti,shati, suruali, suti, sketi,
gauni, kaptula, fulana na kadhalika.
·
Tumia droo ndogo kuhifadhia soksi na
nguo za ndani.
Kwa mpangilio huu hakika
utalifurahia kabati lako la nguo kwani licha ya kuvutia ni kwamba
litakurahisishia kupata kwa haraka na wepesi kile unachohitaji ndani ya kabati.
Vivi
anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755200023
Monday, March 14, 2016
Jinsi ya kuchagua muundo wa ngazi za nyumba
Ngazi
ni eneo muhimu la nyumba ambalo linawasaidia wakaaji wa nyumba hiyo kwenda
maeneo mengine ndani ya nyumba husika, hasa pale nyumba inapokuwa ni ya
ghorofa. Mbali na hilo, muundo wa ngazi pia unahusika kwenye kupendezesha
nyumba.
Mhandisi
David Sembuyagi anasema kuna aina nyingi za ngazi. Ngazi ni gharama na pia ni
ngumu kuzijenga. Kwahivyo ni muhimu ukafahamu hayo wakati unapochagua muundo wa
ngazi. Kama upo kwenye mchakato wa kujenga nyumba itakayohusisha ngazi basi
makala haya yatakusaidia kuamua muundo wa ngazi ambao utakufaa. Dondoo hizi
zitakufanya uje na uamuzi wenye uzito:
1.
Bajeti
Miundo
mbalimbali ya ngazi ina gharama tofauti. Bajeti yako itaamua mtindo, muundo na
malighafi ya kutengenezea ngazi zako.
2.
Nafasi
Nafasi
iliyopo ndani ya nyumba inayohusika kwa ajili ya kuweka ngazi inatakiwa
kuangaliwa kwani ndio inaamua muundo wa ngazi utakaofaa. Kama nyumba ni ndogo,
ni vyema kuchagua muundo wa ngazi ambao hautachukua nafasi kubwa. Na kwa upande
mwingine kama nafasi ni kubwa basi unaweza kuchagua ngazi ya muundo wa kuvutia
na kubwa, au pia unaweza unaweka mbili upande huu na ule.
3.
Usalama
Kwenye
usalama wa ngazi ni lazima kuzingatia mlalo na mwinuko wa hatua usiwe mkali, na
pia kizuizi cha pembeni ni muhimu hasa ngazi inapokuwa ni ndefu na ni lazima
kwa ngazi ya kupanda ghorofani. Usalama
wa ngazi pia uzingatie uwepo wa watoto na wazee ndani ya nyumba. Upana uwe wa
kutosha kuweza kupishana watu wawili,
anayeshuka na anayepanda.
4.
Malighafi
Malighafi
kwa ajili ya kutengenezea ngazi zipo za aina kadhaa. Mwenye nyumba anaweza
kuchagua ngazi ya malighafi ya chuma, mbao au tofali kwa ajili ya nyumba za
kisasa. Kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa malighafi zinazochaguliwa zitaendana
na muonekano mzima wa nyumba, ubora uzingatiwe kwani malidhafi dhaifu hazifai
kwa kutengenezea ngazi.
Vivi anakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Simu 0755200023
Thursday, March 10, 2016
Tuesday, March 8, 2016
Milango ya mbao ngumu ndio bora zaidi kwa nyumba yako
Mukhangu
Noah ambaye ni fundi milango anasema kuwa kati ya milango inayotengenezwa kwa
malighafi mbalimbali ni muhimu kuchagua milango ya mbao ya mkongo, mninga au
mnazi ukilinganisha na
Monday, March 7, 2016
Faida 4 za wallpaper ambazo huwezi ukazidharau
Ubunifu
ni sanaa, na namna ambavyo unapendezesha mahali unapoishi ndio mfano hai wa
jambo hili. Wakati unapoamua kupendezesha ukuta wa nyumba yako unaweza kuchagua
kati ya rangi na karatasi za ukutani zijulikanazo zaidi kama wallpaper. Vitu
vingi kama rangi, mguso, michoro na maua unaviangalia wakati huo. Ila ukiamua
kuweka wallpaper unapata vitu hivi vyote kwenye kifurushi kimoja.
Kubandika
wallpaper ndio hata rahisi zaidi ukilinganisha na mchakato mzima wa kupaka
rangi.
Hapa
naorodhesha faidia 4 utakazopata kutokana na kubandika wallpaper kwenye ukuta fulani wa
nyumba yako. Faida hizi ni za msingi na si za kudharau:
·
Zinadumu
muda mrefu - Zinafaa kwa matumizi yoyote na kwa mtu yeyote katika chumba chochote
iwe ni bafuni, chumba cha kulala au cha chakula. Wallpaper inaweza kudumu hadi
miaka 15 na hata ukuta ukipata alama ndogo za nyufa, kwenye wallpaper hazitokezi.
·
Rahisi
kusafishika - Ni rahisi mno kusafisha wallpaper kwa kitambaa kilicholoa. Hii
inakusadia kuondoa vumbi au uchafu mwingine kwa haraka mno bila kuacha alama
yoyote ukutani. Na nzuri zaidi unaweza kuchagua aina ya wallpaper ambayo ni
ngumu kiasi kwamba unaweza hata kusafisha kwa sabuni na brashi.
·
Ni
rahisi kubandika na kubandua - Huenda nawe ni mmoja wa wanaohofia kuwa
kubandika au kubandua hizi karatasi za ukutani kutasababusha uharibifu wa
ukuta. Sii kweli, nyingi ni rahisi tu kubandua na kubandika tena kama umeamua
kubadili muonekano kwa kubandua za zamani na kubandika mpya.
·
Gharama
nafuu - Endapo utaamua kubandika wallpaper ni kwamba baada ya muda utagundua
kwamba ingekuwa ni kupaka rangi ungetumia gharama kubwa zaidi. Hii ni kwasababu
wallpaper zinadumu miaka mingi ukutani kinyume na rangi. Pia kama unataka dunia
zote mbili yaani ya wallpaper na ya rangi basi kuta fulani za chumba unabandika
karatasi wakati zile nyingine unapaka rangi.
Uamuzi
wa kuingia kwenye ulimwengu wa wallpaper ni wako wewe mwenye nyumba!
Ninakuwezesha kupendezesha nyumba yako. Piga/whatsapp 0755
200023
Dondoo za namna ya kuchagua fimbo za pazia
Ni rahisi kutozingatia namna pazia na fimbo zake
zinavyofanya chumba kionekane. Ila pale unatapoziondoa ndipo unagundua umuhimu
wake. Zifuatazo ni dondoo chache za namna ya kuchagua fimbo kwa ajili ya pazia unazotaka
kutundika.
Weka fimbo ambazo zinaendana na mapambo mengine ya chumba
husika. Hapa ni muhimu kuangalia rangi ya fimbo. Usijeukanunua fimbo za rangi
ya dhahabu kwa mfano, isioane na
VIATU HIVI VYA SHANGA VIPO
Usijali juu ya kwamba una mguu mpana au mnene. Iwe iwavyo utatengenezewa kiatu cha kukufaa. Viatu vyetu ni vya ngozi kamili na shanga original. Bei ni elfu 25. Kununua piga au whatsapp 0755200023
Saturday, March 5, 2016
PICHA NZURI ZA UKUTANI SET YA PISI 3
Picha za ukutani moja kubwa na mbili ndogo. Bei ya zote tatu ni sh laki moja. Kununua njoo 0755 200023
unaweza kuzitundika kwenye level moja kama hivi na umbali kati ya picha na picha usizidi inchi 2
Au unaweza kunyanyua kubwa ya kati juu na hizi ndogo zikakaa level moja fasheni hii.
CAR SHADE, MIAVULI YA BUSTANI NA TURUBALI ZA KUZUIA JUA
Usikubali rangi ya gari lako iharibiwe na jua. Tujulishe tukusimikie net ya car shade kama hii
Weka mwavuli bustanini ufaidi mahali pa kupumzikia kupunga upepo
Hii ni kwa ajili ya sehemu ambapo jua linaingia ndani na kuwa kadhia kwa kuwachoma waliomo.
Kwa mahitaji tuwasiliane 0755 200023
PICHA NZURI ZA UKUTANI ZINAPATIKANA
Hey friend, natumai jumamosi ni njema kwako. Wewe unayehitaji picha nzuri za ukutani sasa zinapatikana, zina sehemu ya kutundikia kwa nyuma (naamaanisha sio za mezani) na ukubwa wake ni upana wa cm 28 kwa urefu wa cm 35. Ziko chache. Simu 0755 2000 23
Inafaa kuwekwa kwenye corridor
Inafaa dining
Inafaa bedroom juu ya ubao wa kichwani
Maua sebuleni na kwenye corridor yanapendeza
Thursday, March 3, 2016
VMC:....MITO MIDOGO YA KWENYE MAKOCHI YA ORANGE SASA IPO
Rafiki, hivi unajua kubadilisha mito au foronya ndio njia nyepesi na gharama nafuu kuliko zote ya kupendezesha sebule yako?
Mito hii ya orange inafanya kazi kubwa ya kuongeza rangi kwenye makochi, na ubora wa kitambaa chake ni wa uhakika. Kununua nijulishe. Bei ya mto pamoja na foronya yake ni elfu 25. Bei ya foronya pekee ni elfu 20. Karibuni..
PICHA: Mpangilio wa stoo ya vyakula
Mpangilio ni kiini cha usafi ndani ya nyumba. Mara utakupoweza kupangilia utakuwa umejikomboa jumla.
Wednesday, March 2, 2016
TRAY NZURI ZA MBAO ZINAPATIKANA
Tray nzuri za mbao sasa zinapatikana. Zina muonekano wa kuvutia wa asili na finishing yake maji yanateleza. Set moja ina tray 3. Zipo chache na endapo unahitaji karibu. Piga/whatsapp 0755200023
HOME DECOR HAPA NA PALE.....TABLE RUNNER, PAZIA, TAA ZA JIKONI
Nimependa hii meza ambapo table runner zimetandikwa kwa upana. Just kuwa mbunifu usitandike kwa urefu tu saa nyingine unabadili muonekano. Watu wanapenda mabadiliko!
Chumba ni pazia, vilevile tazama utundika wa zile sanaa za ndege ukutani. Pata idea za utundikaji wa picha pale sehemu kubwa ya chumba inapochukuliwa na pazia.
Wengi wanapojenga jiko wanazingatia zaidi makabati na kutotia maanani vitu vidogo kama taa. Hizi taa za kuning'inia kwenye housing lake (pendants) zinapendezesha jiko kwa mwanga wa kutosha.
Msisahau kushea na mimi picha za majumbani mwenu ili tujifunze pamoja. Ukishea ujuzi unajisikia vizuri!
Mambo matano unayotakiwa kufahamu kabla ya kuanza mradi wa kupendezesha nyumba yako
Hongera!
Umeamua kuanza kuipa nyumba yako muonekano wa kuvutia. Kwa binadamu yeyote
nyumba ni mali muhimu na ambayo iko karibu zaidi na moyo wake. Kila mwenye
nyumba anatamani nyumba yake ionekane nadhifu na ya kuvutia bila shaka kuliko sehemu yoyote ile nyingine
kwenye ulimwengu huu. Hii ndio maana dhana ya kupendezesha nyumba iko kwa kila
mtu.
Kama
tujuavyo kupendezesha nyumba kunahitaji muda na fedha, hivyo unatakiwa kuwa
makini sana na maamuzi yako. Mara tu unapoanza kufikiria jambo hilo, kuna mambo
muhimu ya kuzingatia kabla ya
Tuesday, March 1, 2016
Namna ya kubadilisha muonekano wa nyumba na kuleta mvuto kwa gharama nafuu
Baada
ya miaka kadhaa ya kuishi kwenye nyumba hiyo hiyo, nyumba wengi wanatamani kubadilisha mionekano
ya nyumba zao hizo. Na mara nyingi wazo linalowajia ni marekebisho ya jengo na
kubadilisha fenicha. Hata hivyo hii inamaanisha gharama kubwa na kushirikisha
wataalam wa kutekeleza jambo hilo.
Lakini
je, kwanini mwenye nyumba asifikirie kufanya mabadiliko ya gharama nafuu kama
vile badala ya kununua fenicha mpya akafanya maboresho kidogo ya zilizopo na zikaleta
mvuto kabisa.
Makala
zangu nia yake ni kukupa mawazo lukuki ambayo unaweka kutumia kuboresha maisha
ya nyumbani kwako kwa gharama nafuu. Endapo mwenye nyumba utaamua kufanya
utafiti kidogo na kufuata ushauri unaweza kufanikisha kazi yako kirahisi na kwa
gharama nafuu sana. Kwani utakuwa umeshaelewa picha nzima ya unachotakiwa
kufanya na kwa wewe kushirikiana na watendaji wachache utafanikisha lengo lako.
Matumizi
tofauti ya rangi, karatasi za ukutani, vitambaa na malighafi nyingine
zilizotengenezea fenicha zako vinaweza kubadilisha kabisa muonekano na kukupa
wa kuvutia.
Zipo
rangi za kung’aa kama polishi na zipo zisizong’aa za mati unazoweza kutumia
kuboresha fenicha zako. Kwa mfano kupaka rangi upya kabati la luninga, miguu ya kiti au meza kunabadilisha kabisa
muonekano wake. Vile vile bila kusahau kubadilisha kitambaa kilichotengenezea
viti au sofa endapo kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Dondoo
nyingine ni kubadili vitu kidogodogo kama vile tai na fimbo za pazia. Ni ukweli
kuwa vitu vya nymbani vinabadilika kila baada ya kipindi kifupi. Huenda tai
zako za pazia za miaka mitano iliyopita ni tofauti kabisa na zilizopo kwenye
mitindo sasa. Cha muhimu ni kuangalia hivi vitu vidogo visivyo vya gharama
kubwa ambavyo ukivibadili vinapendezesha nyumba yako zaidi.
Eneo
lingine ni la kwenye mito ya makochi. Kuwa na foronya mbalimbali na badilisha
mara kwa mara. Vilevile kwa upande wa bakuli la taa, balbu siku zote ni
hiyohiyo kinachobadilika ni jumba lake. Endapo utabadili jumba la taa kama vile
taa ya jikoni au chumba cha chakula na kuweka ya kisasa zaidi bila shaka
utakuwa umeboresha muoneakno kwa gharama nafuu kabisa.
Tukienda
kwa upanda wan je ya nyumba huenda ukataka kuboresha kwa kupaka rangi upya na
pia kuongeza taa za ulinzi. Unapopaka rangi zingatia kuboresha zaidi yale
maeneo yaliyomeguka meguka. Kwa mfano nimeona watu wakitengenezea mikanda
kuzunguka madirisha ambapo mwanzoni haikuwepo. Matokeo ya hii mikanda ni kufanya
nyumba kuwa ya kisasa zaidi kwa nje na vilevile kuficha zile kona zilizokuwa
zimemeguka.
Kwa
upande wa bustani huenda mwanzoni miaka ya nyuma uliweka njia ambazo sasa
huzihitaji tena kwa maana ya kwamba hazitumiki. Ni wakati wa kuziondoa na
kufanya eneo lote liwe na ukoka. Pia kuna wakati vitofali vinakuwa vimemeguka
aidha kwa sababu ya maji ya chumvi au ni kwamba tu vimekaa muda mrefu. Kutokana
na hali yake unaweza kuvipaka rangi au laa kuviondoa na kuweka sakafu ya malighafi nyingine bora zaidi
iliyopo sokoni kwa kipindi hicho. Wakati huohuo usisahau kuboresha stendi
na vyungu vyako vya maua aidha kwa
kuvipaka rangi (kazi ambayo unaweza kufanya mwenyewe) au kuotesha maua mazuri
zaidi.
Hizi
ni dondoo za maeneo kadhaa unayoweza kuangalia ili kuboresha muonekano wa
nyumba yako uwe wa kisasa zaidi na mahali pazuri pa kuishi. Na kama wewe ni
mpenzi wa vitu vizuri hii inaweza kuwa ni tabia yako kila baada ya miaka
kadhaa.
Vivi
anakuwezesha kupendezesha nyumba yako kwa gharama nafuu kabisa, atakushauri na aidha utatekeleza wewe mwenyewe au atakuunganisha na watendaji wa maeneo hayo. Kwa maelezo zaidi simu 0755200023
Subscribe to:
Posts (Atom)