Kwa
wengi wenye makazi ya kisasa duveti limekuwa sehemu muhimu ya matandiko yao.
Sio tu linapendezesha kitanda na chumba kwa ujumla, lakini pia linamsaidia
mlalaji kupata uzingizi murua. Unapotaka kununua duveti utashangazwa na aina
nyingi na za kuvutia zilizopo sokoni ikiwa ni pamoja na mapya na ya mitumba
ambapo inaweza kukuchanganya kuwa ni lipi hasa ununue.
Bi
Eve Moshi wa kampuni ya Eve Beddings Mwenge simu namba 0713 681 261 ambao ni
wauzaji wa mashuka na
maduveti anatujuza kuwa maduveti yanakuja kwa mitindo mbalimbali, ukubwa,
rangi, uzito, malighafi ya kitambaaa ambavyo vyote hivi vinachangia kwenye
kupata lililo sahihi. Mnunuzi usisahau kuzingatia yote haya wakati unapochagua
duveti la kununua kabla hujafikia uamuzi wa mwisho.
Ukubwa
Siku
zote unapotaka kununua tandiko hasa duveti, ukubwa ni kitu muhimu mno cha
kuzingatia. Duveti la ukubwa sahihi kwa kitanda sahihi unakupa usingizi sahihi
kwani linakupa ukubwa sahihi wa kuufunika mwili wako wote. Eve anasema mara
zote inatakiwa kuchagua duveti ambalo ni kubwa kuliko ukubwa wa kitanda unachoenda
kulitandika. Inalipa kitanda muonekano safi na nadhifu.
Kitambaa
Kitambaa
kinachukua nafasi muhimu katika utengenezaji wa duveti. Aina ya malighafi
iliyotumika inaamua hisia ya mvuto kati ya ngozi ya mlalaji na duveti. Ni ukweli kuwa
maduveti yaliyotengenezwa kwa kitambaa chenye kiwango kikubwa cha pamba
yanapendwa zaidi japo kuna ya vitambaa vingine pia kama hariri na mchangayiko
wa hariri na pamba. Ingawa maduveti yenye kitambaa cha pamba ndio yako juu
haimaanishi kuwa huwezi kununua ya vitambaa vingine kwani nayo yana faida zake.
Kwa mfano, duveti la hariri linakauka mapema zaidi kuliko la pamba. Kwahivyo
hapa ni wewe uamue mwenyewe baada ya kufahamu haya.
Uzito
Maduveti
yaliyojazwa malighafi za ndani kwa jinsi ambayo yanaonekana ni manene
yanapendwa kuliko yale yaliyo nyepesi. Wanunuzi wengi hawaonekani kujali kama
ni mazingira ya baridi au joto wao wanachotaka ni duveti liwe zito na hisia za
kunesa kiasi.
Rangi na michoro
Wakati wowote unapotaka kununua duveti ni vyema uzingatie
mandhari ya chumba unachotaka kuliweka ili michoro na rangi iendane na ya vitu
vingine ili kukifanya chumba kivutie. Pia katika dondoo hii fahamu kuwa kuna
maduveti yenye michoro ambayo yanafaa zaidi kwenye vyumba vya watoto wadogo
kuliko vya watu wazima. Vilevile rangi na michoro
mbali na nia ya kuongeza mvuto wa chumba, ni kwa swala la usafi endapo
kimiminika chochote kitadondokea kitandani kwa bahati mbaya. Sasa kutokana na
maisha yako ndipo unaamua rangi na michoro fulani ndio itakufaa zaidi.
Mara
zote unapotaka kununua duveti zingatia mambo hayo manne ili usijekuchagua ambalo
ni la kiwango cha chini ukawa umetumia vibaya hela yako.
No comments:
Post a Comment