Friday, September 16, 2016

Jinsi ya kuchagua mtindo sahihi wa wallpaper

 
Tunaweza kusema kuwa wallpaper ndio habari ya mjini kwa sasa kwa ajili ya kupendezesha vyumbani kwenye nyumba nyingi za kisasa hasa chumba che sebule. Tatizo lililopo ni changamoto ya mtindo upi ndio sahih kutokana na
uwepo wa wallpaper za rangi na michoro mingi mno. Hadi zile flati yaani zisizo na mchoro wowote.

Nimehojiana na Bi Phides wa Phides DΓ©cor kama mtaalam wa wallpaper ili kupata dondoo zake za ni kwa namna gani mnunuzi anayetaka kupamba kwa pambo hili anavyoweza kununua ya mtindo sahihi kwa chumba sahihi.
Anasema pale unapokuwa umefikia uamuzi wa kwamba unataka kupendezesha chumba fulani kwa wallpaper kuna maswali kadhaa ya mitindo ya  wallpaper unatakiwa uweze kujijibu. Je chaguo zuri kwako ni wallpaper yenye michoro au iliyo flati? Jibu hapa linategemea na ladha binafsi ya mwenye kutaka kupamba. Wallpaper yenye michoro hata kama ni ya rangi sawa na ya wallpaper yenyewe, kwa kawaida inasaidia kuficha makosa yoyote yaliyopo ukutani.

Wallpaper flati inakupa wigo mpana wa muonekano wa kung’aa na metaliki. Lakini kwa ujumla mimi Phides kama mpambaji na muuzaji wa wallpaper nimeona wateja wangu wengi zaidi wakipendelea wallpaper zenye michoro kuliko zile za flati.

Zingatia kiasi cha mwanga kwenye chumba husika. Pata jibu kuwa je chumba hicho kinahitaji wallpaper ya rangi nzito au nyepesi  ili kiwango cha mwanga kisiathirike iwe ni asubuhi, mchana au usiku.

Je ni ukuta wa chumba gani unaotaka kuubandika wallpaper?
-Kama ni chumba cha kulala cha wanandoa, wallpapaer zenye maua ndiyo inafaa zaidi kwani inaleta hisia ya mahaba.
-Kama ni sebule yenye mapambo ya mtindo wa kisasa (rejea makala ya mitindo minne za kupamba ndani), wallpaper yenye michoro ya rangi nzito, metaliki, ya kung’aa na ya mguso wa mtelezo  ndio inafaa zaidi kwani ndiyo inayoonekana  ni za kifahari.

Swali lingine la kujiuliza upate majibu ni kwamba je ni kwa staili gani unataka kubandika hiyo wallpaper yako. Staili zote hazileti muonekano unaofanana, sawa eeh? Kwa mfano kubandika wallpaper kwenye ukuta mmoja tu kati ya nne za chumba sio sawa na kubandika kwenye kuta zote nne. Chagua wallpaper yenye rangi nzito kama unabandika kwenye ukuta mmoja tu kwa mfano ule wa luninga kwa sebuleni au wa tendego kama ni chumba cha kulala. Staili ya wallpaper yenye rangi za namna hiyo, metaliki na mtelezo itatoa muonekano wa kiwango na kuvutia. Vilevile wallpaper za mtindo huu zinapendeza pia kwenye dari.

Chumba kidogo kinapendeza kikibandikwa wallpaper isiyo na michoro au maua laa kama inayo basi yawe ni yale madogodogo. Wakati huohuo chumba kikubwa kikipendeza kwa wallpaper yenye michoro na maua makubwa.

Kwahivyo ukishakuwa na vigezo hivi kichwani, ni rahisi kwako kwenda dukani na kuchagua wallpaper sahihi.

No comments:

Post a Comment