Kuanzia kwenye kuchagua rangi ya makabati, kuta, sakafu na dari jiko ni chumba
chenye maeneo mengi ya kutumia ubunifu wako wa kuchagua rangi. Ila tatizo wengi
wanajiuliza ni kwa namna gani wanaweza kuchagua rangi ambazo zitafanya chumba
hiki kionyeshe mshikamano wa rangi hizo. Kutokana na uwepo wa
rangi lukuki
sokoni, hakika hii inaweza kuwa ni changamoto kwa wengi.
Uzuri
ni kwamba hata kama utaamua kwenda na makabati meupe bado hukosi fursa ya
kutambulisha rangi katika maeneo mengine ya jiko.
Wengi
wanaanzia siku zao jikoni, kwahivyo nyeupe ina uwezo mkubwa wa kukipa chumba
hisia ya nguvu ya kuanzia siku. Pia ina hisia ya kitu freshi na safi. Jiko
lenye rangi nyeupe kote lina mvuto wa aina yake.
Chagua
muonekano wa makabati kwanza. Watu wengi wanapendelea makabati ya mbao ngumu
kwani ndio imara yanayoweza kukabiliana na majimaji ya jikoni. Hivyo basi
kutokana na makabati kuwa ya mbao vilevile wengi wanapendelea kuyapaka
finishing ambazo zitayaacha na rangi zake za asili.
Baada
ya kuamua rangi ya makabati kinachofuata ni kuchagua rangi za kaunta, kuta,
dari na sakafu. Kwavile jikoni kipaumbele ni kuwa na mwanga wa kutosha ni vyema
ukatumia rangi nyepesi. Uzuri ni kwamba kila chumba ndani ya nyumba kina rangi
inayokifanya kipendeze kuliko nyingine.
Rangi
kama nyekundu inaaaminiwa kuleta hamu ya kula na inafanya vizuri kwa chumba cha
jiko. Kuna jamii nyingi za nyekundu na huwa inachomoza vyema kwenye
makabati na baadhi ya sehemu za ukuta.
Kijivu
ni rangi isiyoegemea upande wowote ambayo imeonekana kushika kasi siku za
karibuni kwenye nyumba nyingi. Jamii nzuri ya kijivu inaweza kufanya maajabu
jikoni huku ikioanishwa vizuri na ile ya kaunta na makabati.
Bluu
ni rangi nyingine pia ambayo inapendeza jikoni. Bluu nyepesi inapotumika,
inaleta muonekano nadhifu wa usafi na inashauriwa kwenye kuta, makabati na hata
dari. Siku zote tumia bluu nyepesi jikoni kwani kwa kawaida ile nzito inaweza
kukizidi nguvu chumba. Bluu inaendana na nyeupe (kumbuka mawingu), kijivu na
nyingine ambazo haziegemei upande wowote.
Kama
miale ya jua ilivyo, njano inaweza kuongeza mwanga chumbani kwa haraka mno.
Ingawa inaaminiwa kufanya watu wasikie njaa, lakini pia ina hisia ya utulivu kwahivyo kuwafanya watu wawe na
furaha wawapo jikoni. Njano ni chaguo zuri kwa jiko dogo kwani inalifanya
lionekane kubwa na inaendana vyema na nyeupe.
No comments:
Post a Comment