Kubadilisha
muonekano wa nyumba yako kila baada ya kipindi sio tu kwa ajili ya umaridadi
bali pia ni katika kukabiliana na matakwa ya familia yako inayokua. Kama ni
mtoto mchanga anakua kuelekea kuwa mtoto mdogo na hatimaye “tineja”.
Kadri
familia inavyokua ndivyo mabadiliko yanavyohitajika, mahitaji ya nyumba inabidi
yabadilike kuendana na mahitaji ya familia iliyokua. Na hapa ndipo swala la
kwenda na wakati kutokana na staili na mitindo ya mapambo ya nyumbani
linaingia.
Kupamba kwenda na wakati inafanya nyumba yako kuzidi kuwa mahali
pazuri pa kuishi na kukuza vipaji vilivyoko ndani ya familia. Pia nyumba
inakuwa na muonekano wa mahali pa amani na patakatifu panaporuhusu familia yako
kuburudika baada ya siku ndefu wakiwa nje ya nyumbani.
Mwenye
nyumba anaweza kuenda na wakati wa mapambo ya nyumbani bila kutumia gharama
kubwa. Anachotakiwa kuwa nacho ni ubunifu, kufanya utafiti mwingi na kutia
bidii kutengeneza mazingira ambayo familia yake inaweza kuishi na kukua.
Zifuatazo ni njia ambazo wewe mwenye nyumba unazoweza kuzifuata na kwenda na
wakati katika mapambo ya nyumbani bila nguvu wala gharama kubwa.
Peleleza
uwezekano uliopo. Kuna chaguzi na mitindo mingi ya kuchagua linapokuja swala la
kupamba nyumba yako. Usibanwe na manthari iliyopo kwenye nyumba yako kwa wakati
husika. Kupaka rangi mkono mmoja tu kunaweza kubadili muonekano wa chumba, hata
hivyo mabadiliko madogo kama hayo hayawezi kuleta matokeo yote unayotataka.
Angalia ndani ya nyumba yako na utashangazwa na maeneo mengi ambayo yamebaki
bila kuguswa na pia maeneo ambayo yakibadilishwa yatabadilisha jinsi
unavyoishi. Nyumba yako ni hazina na ina sehemu nyingi sana ambazo
hazijafanyiwa kazi. Zipeleleze na ufanye jambo.
Kuwa
mbunifu kwa kupamba kwa chochote. Kwa mfano kuna watu wameweza kupamba bustani
za nyumba zao kwa kutumia matairi yaliyochakaa. Matairi haya yamekuwa yakipakwa
rangi kali kama vile za nyekundu au chungwa na kuwezesha kubadili kabisa
muonekano wa bustani.
Katika hili mwenye nyumba anafanikiwa kuleta matokeo
makubwa kwa gharama na nguvu ambayo bila shaka ni ndogo sana.Kuna vitu
vinazunguka nyumbani kwako kwa mfano chupa na vingine vingi ambavyo vinasubiri ubunifu na kipaji chako
cha kuvitumia kwa kupamba.
Soma
makala kama hizi na tembelea mitandaoni kupata mawazo mapya juu ya mabambo ya
nyumbani. Kila mara nenda na wakati kufanhamu juu ya nini kipya kwenye mapambo
ya nyumbani. Utashangazwa na jinsi wenye nyumba wengine wanavyoweza kuwa
wabunifu kwa kazi za mapambo ambazo wanaweza kufanya wenyewe bila kushirikisha
mtaalam.
Shirikisha
familia yako kwenye upambaji. Watie moyo watoto wako washiriki, wanaweza kuwa
na mawazo mazuri sana juu ya muonekano wa vyumbani mwao na sebuleni. Hii ni
kwasababu wao ndio wanakaa humo kwa hivyo wanajua wanahitaji kuongeza au
kupunguza nini. Pia huenda wametembelea kwa marafiki zao na kukutana na vitu
vipya walivyovipenda. Utapata nafasi pia ya kugundua vipaji vya sanaa walivyo
navyo wanafamilia wako ambavyo pengine vilijificha. Kufanya kazi na familia
nzima kwa shuhuli za kupamba nyumba ni uzoefu wa kumbukumbu nzuri.
Je, unauza bidhaa au huduma inayohusu nyumba
na bustani ambayo unataka Watanzania waijue? Nijulishe simu/whatsapp 0755200023
No comments:
Post a Comment